Special Thread kwa uchaguzi mkuu ujao 2020.

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Salaam wakuu,

Ni mapema mno kuanza kuzungumzia uchaguzi mkuu ujao 2020, lakini pia siyo vizuri kuchelewa sana kuzungumzia suala hili, ikiwa ni pamoja na kujiandaa.

Mawazo yako hapa pengine kwa namna moja au nyingine yanaweza kuonesha mwelekeo wa uchaguzi huu mkuu ujao.

Unachotakiwa kufanya, ni kuelezea mtazamo wako kuhusu namna unavyohisi uchaguzi huu utakavyokua.

Unaweza pia kueleza ni unahisi ni nani ataibuka kidedea na kwanini.

Unaweza kueleza pia unahisi ni nani atakayeshindwa na kwa nini.

Unaweza pia kueleza ni mabadiliko gani ungependa yafanyike ili kuufanya uchaguzi huu mkuu ujao uwe murua kushinda zilizopita.

Katika hili, tuweke itikadi zetu za vyama vya siasa na tujadili kama WATANZANIA.

Tuendelee kujadili kila leo kulingana na matukio mbali mbali yanayotokea nchini ambayo tutahisi kwa namna moja au nyingine yataathiri upande fulani ktk uchaguzi ujao 2020.

Tukijadili hadi 2020, basi itasaidia kuona mwelekeo mzima wa uchaguzi huo kwa mawanda mapana.

Karibuni..
 
UCHAGUZI KUELEKEA 2020 CCM ITASHINDA KWA KISHINDO .

PILI UCHAGUZI WA 2020 UPINZANI WATAANGUKA SANA KATIKA NGAZI YA UBUNGE NA UDIWANI.

TATU IDADI YA WAPIGA KURA WATAKAOJITOKEZA ITAKUWA NI NDOGO SANA
 
1.Wapinzani tusijidanganye kabisa 2020 bila tume huru na katiba mpya CCM itashinda kwa zaidi ya 80%..... tukikosa tume huru bora tususe tu maana hata ubunge na udiwani tutaporwa hata haya majimbo tulionayo na tutaambulia machache sana......

2. Pili tuhakikishe tunalazimisha serikali iheshimu sheria ya vyama vya siasa kma mwaka 2017 utaisha na mikutano imezuiwa huku kwenye majukwaa anaonekana magufuli tu then kwan namna yoyote ile 2020 hatutoambulia chochote. Hata kma watatupa tume huru ila kma mikutano ya kukagua uhai wa chama hairuhusiwi watanzania hasa wa vijijini watatusahau na hivyo nguvu zote zile za M4C na operation sangara vitakuwa ni wastage of time.

3. Tuwekeze nguvu majimbo tulionayo na ambayo tunataka tuyachukue kwa jinsi magu alivyo sioni kma NEC inaweza mtangaza mpinzani mshindi nafasi ya rais hta kma tutamsimamisha OBAMA...... tujijenge kwenye halmashauri na majimbo tulionayo itakuwa kampeni tosha kwa ajili ya 2020.

MUHIM NI TUME HURU NA MIKUTANO KWANZA
 
Wapinzani wana imani ya ajabu sana. Wanaamini kuwa chini ya sheria hii ya uchaguzi na tume hii wanaweza kushinda uchaguzi. Hadi sasa hawana mkakati wowote wa kudai Katiba mpya. Nadhani wamelogwa!
 
UCHAGUZI KUELEKEA 2020 CCM ITASHINDA KWA KISHINDO .

PILI UCHAGUZI WA 2020 UPINZANI WATAANGUKA SANA KATIKA NGAZI YA UBUNGE NA UDIWANI.

TATU IDADI YA WAPIGA KURA WATAKAOJITOKEZA ITAKUWA NI NDOGO SANA
Kwanini umeyasema haya yote mkuu?
 
Ccm inashinda tu Ukawa hawawezi kushinda kwasababu wameshindwa kupingania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Mkuu kasema hili halipo ktk mipango yake.

Wapinzani watumie kitu gan kumshawishi akubali hiki kitu?
 
1.Wapinzani tusijidanganye kabisa 2020 bila tume huru na katiba mpya CCM itashinda kwa zaidi ya 80%..... tukikosa tume huru bora tususe tu maana hata ubunge na udiwani tutaporwa hata haya majimbo tulionayo na tutaambulia machache sana......

2. Pili tuhakikishe tunalazimisha serikali iheshimu sheria ya vyama vya siasa kma mwaka 2017 utaisha na mikutano imezuiwa huku kwenye majukwaa anaonekana magufuli tu then kwan namna yoyote ile 2020 hatutoambulia chochote. Hata kma watatupa tume huru ila kma mikutano ya kukagua uhai wa chama hairuhusiwi watanzania hasa wa vijijini watatusahau na hivyo nguvu zote zile za M4C na operation sangara vitakuwa ni wastage of time.

3. Tuwekeze nguvu majimbo tulionayo na ambayo tunataka tuyachukue kwa jinsi magu alivyo sioni kma NEC inaweza mtangaza mpinzani mshindi nafasi ya rais hta kma tutamsimamisha OBAMA...... tujijenge kwenye halmashauri na majimbo tulionayo itakuwa kampeni tosha kwa ajili ya 2020.

MUHIM NI TUME HURU NA MIKUTANO KWANZA
Katiba mpya ni dhahiri kabisa haiwez kupatikana kwa sasa.

Hapa wapinzani watafute plan B labda
 
CCM nmeanza kuingiwa na roho ya uasi kwa chama changu cha mapinduz japo nakipenda lkn sioni kama kinauhalali wakuendelea kuiongoza hii nchi chin ya huyu m.kit...
Fikra kama hiz naamin siko nazo mm peke yng kuna kundi kubwa tu na lenyew limeshajikatia tamaa na chama chao wakiwemo viongiz wakubwa esp wale ccm maslah ambao walikua wakiish kwa posho na migao ya ujanja ujanja kitu ambacho m.kiti mpya amezuia kwa kupunguza posho pamoja na idad ya wajumbe wa vikao na pia idad ya vikao kwa mwaka...
Hvyo kwa sasa wanaona kuwa kiongz ndan ya ccm ni kujinasibisha na njaa tu ni bora kuwa mwanachama wa kawaida huku ukisoma mchezo kwa mbaaaaali
 
Katiba mpya ni dhahiri kabisa haiwez kupatikana kwa sasa.

Hapa wapinzani watafute plan B labda
Sawa katiba mpya haiwezekani maana dikteta kaamua kuipa kisogo..... solution ni minimal reforms kma ilivyokubaliwa kati ya serikali iliopita na TCD.... bunge maalum liitishwe ili lipitishe hizo minimal reforms zitakazozaa tume huru, mgombea binafsi,matokeo ya urais kupingwa mahakamani, vyama kuungana n.k

Ikiwezekana wakinukishe bungeni kma alivyofanya mnyika kipindi kile cha kura ya maoni iliposua sua yaani shughuli zisiendelee mpaka tushinikize serikali iheshimu makubaliano ya TCD
 
Salaam wakuu,

Ni mapema mno kuanza kuzungumzia uchaguzi mkuu ujao 2020, lakini pia siyo vizuri kuchelewa sana kuzungumzia suala hili, ikiwa ni pamoja na kujiandaa.

Mawazo yako hapa pengine kwa namna moja au nyingine yanaweza kuonesha mwelekeo wa uchaguzi huu mkuu ujao.

Unachotakiwa kufanya, ni kuelezea mtazamo wako kuhusu namna unavyohisi uchaguzi huu utakavyokua.

Unaweza pia kueleza ni unahisi ni nani ataibuka kidedea na kwanini.

Unaweza kueleza pia unahisi ni nani atakayeshindwa na kwa nini.

Unaweza pia kueleza ni mabadiliko gani ungependa yafanyike ili kuufanya uchaguzi huu mkuu ujao uwe murua kushinda zilizopita.

Katika hili, tuweke itikadi zetu za vyama vya siasa na tujadili kama WATANZANIA.

Tuendelee kujadili kila leo kulingana na matukio mbali mbali yanayotokea nchini ambayo tutahisi kwa namna moja au nyingine yataathiri upande fulani ktk uchaguzi ujao 2020.

Tukijadili hadi 2020, basi itasaidia kuona mwelekeo mzima wa uchaguzi huo kwa mawanda mapana.

Karibuni..

Fanya kazi wewe ujenge maisha yako na wanaokutegemea, ndo kwanza tumemamliza uchaguzi unawaza uchaguzi mwingine? Si uhamie Kenya tayari wako kwenye campaign mode!
 
Mkuu, hivi kwako wewe 2020 ni mbali?

Hii thread itadumu hadi 2020
 
Back
Top Bottom