Sote tutakufa lakini tanzania itabakia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sote tutakufa lakini tanzania itabakia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Nov 13, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  TBC- 1: Prof.Palamagamba John Kabudi, Mtaalamu wa sheria za Katiba, Mazingira na Sheria za Kimataifa akiwapiga msasa wabunge.

  PROF KABUDI; SOTE TUTAKUFA LAKINI TANZANIA ITABAKIA: SEMINA YA WABUNGE: SHERIA YA KATIBA  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Prof Palamagamba Kabudi wa Chuo Kikuu Dar es salaam amewataka wadau wote wa katiba Mpya kuweka maslahi ya Taifa mbele kipindi hiki cha mchakato wa Katiba Mpya. Prof. kabudi amesema "ikumbukwe kwamba sote tutakufa lakini Tanzania itabaki". Alikuwa akiendesha semina ya marekebisho ya katiba mpya mjini Dodoma jana.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Wajumbe wa semina wakimsikiliza Prof Kabudi
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Waziri Mkuu na Mweneyekiti wa Semina Mhe. Mizengo Pinda akifungua semina ya mchakato wa marakebisho ya Katiba Mpya mjini Dodoma jana
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  PRINCE MINJA


  Muswada wa katiba moto kwa serikali
  MUSWADA wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, umeendelea kuilemea serikali baada ya wasomi na wabunge kuupinga wasipelekwe bungeni kesho kujadiliwa badala yake urejeshwe kwa wananchi.Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma ya Mwalimu Nyerere wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji amesema muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba unatakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza.

  Amesema ukisomwa kwa mara ya pili kama ilivyopangwa na serikali, wananchi hawatapata fursa ya kutoa maoni yao.Profesa Shivji alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Nchini (TCD).Kongamano hilo lilihusu uchambuzi na mapendekezo kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba mpya.

  Shivji alisema katika muswada huo umefanyiwa mabadiliko makubwa tofauti na ule wa kwanza." Muswada huu wa sheria ulifanyiwa marekebisho na kupitishwa na serikali usomwe kwa mara ya kwanza ili watanzania wapate nafasi ya kuujadili kwani una mabadiliko makubwa na hii ndio sauti yetu" alisema Profesa Shivji.Alisema Katiba si mali ya viongozi ni ya wananchi hivyo wanapaswa kushirikishwa katika kuiandaa.

  Tume ya Katiba
  Profesa Shivji alipendekeza Tume ya Katiba kuwa na wataalam wasiozidi 20 badala ya 30, kwani idadi hiyo ni kubwa mno.Alisema majina ya wanaotakiwa kuunda Tume hiyo wapendekezwe na vyuo vikuu na vyama vya kitaalum na Rais ateue majina yanayotokana na mapendekezo hayo.

  Profesa Shivji alisema baada ya hapo sekretarieti ya Tume ya Katiba iundwe na tume yenyewe itakayochaguliwa.
  " Lakini kwa utaratibu huu wa rais kuteua mwenyekiti wa Tume ya Katiba na wajumbeunaonyesha wazi kuwa kuwa tume hiyo haitakuwa huru," alisema Profesa Shivji.Kauli ya Shivji iliungwa mkono na wadau wa Katiba ambao waliwataka wabunge kutopitisha muswada huo kwa mara ya pili kwa kuwa watakuwa wanawasaliti wananchi.

  Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba pia alisema muswada huo wa sheria unatakiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mara ya kwanza ili baada ya hapo wananchi wapate fursa ya kuujadili.Alisema kwa ratiba zilizopo wiki ijayo muswada huo wanataka kuuwasilisha Bungeni kwa mara ya pili hatua ambayo itawanyima wananchi fursa ya kuujadili." Muswada huo uliwasilishwa kwa mara ya kwanza kukawa na kasoro, zimefanyiwa marekebisho sasa upelekwe kwa mara ya kwanza ili wananchi wapate fursa ya kuujadili," alisema.

  " Muswada huo ulikuwa na kasoro ya kuandikwa kwa kiingereza wananchi wakapinga, sasa umeandikwa kwa Kiswahili, wananchi wapate fursa ya kuujadili kwa sababu wataelewa kilichoandikwa," alisema Kibamba.Alisema kwa kawaida muswada huwasilishwa Bungeni kwa mara ya kwanza ndipo wananchi baada ya hapo hupata fursa ya kuujadili.

  " Hii ina maana ukiwasilishwa kwa mara ya pili na kupitishwa na wabunge wetu, Katiba inaweza kupatikana bila ya wananchi kuchangia maoni yao tatizo ambalo limekuwa likilalamikiwa katika Katiba ya sasa," alisema Kibamba.

  Naye Isaac Cheyo wa UDP alisema makosa yanayolalamikiwa na wananchi katika Katiba iliyopo yasirudiwe katika Katiba tunayoiandaa." Tumekuwa tukilalamika kwamba Katiba iliyopo haikutokana na wananchi, iliandikwa na kikundi cha watu wachache, hii ya sasa wananchi washirikishwe," alisema.

  Naye Fred Hatie wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kwa kitendo cha kuwakwepa wananchi, serikali inaonyesha haina nia ya dhati ya kupata Katiba mpya." Mnakumbuka Waziri wa Sheria na Katiba aliwahi kusema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, Mwanasheria Mkuu naye akaunga mkono, rais ndiye akaamua kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, wanaonyesha hawana nia ya dhati," alisema.

  Naye Kizitto Noya na Habel Chidawali,wanarioti kutoka Dodoma
  kuwa serikali jana ililazimika kuwaita wataalamu wa Katiba kuwapiga msasa wabunge kabla ya kuanza kujadiliwa bungeni kesho kwa muswada wa katiba.

  Semina hiyo ambayo mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, iliendeshwa na maprofesa wa vyuo vikuu; Palamagamba Kabudi (UDSM) na Romwald Haule (Ruaha), ikiwashirikisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na watalaamu wengine wa masuala ya Sheria na Katiba kutoka visiwani Zanzibar na Tanzania bara.

  Semina hiyo inatafsiriwa kuwa ni mbinu ya serikali kuwalainisha wabunge ambao tayari baadhi yao wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, wameonyesha msimamo wa kuupinga muswada huo na kutaka ukasomwe bungeni kwa mara ya kwanza badala ya kwenda kusomwa kwa mara ya pili.

  Kwa muda wa siku tatu mfululizo, kamati hiyo ya Katiba, Sheria na Utawala, imekuwa ikijadili muswada huo bila kufikia mwafaka kutokana na kutokea mgawanyiko mkubwa baina yake na serikali kuhusu mambo kadhaa, ikiwamo ama muswada huo usomwe kwa mra ya kwanza au mara ya pili.

  Mbali na wabunge hao, kada nyingine inayopinga muswada huo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Jukwaa la Katiba ambalo limeenda mbali na kueleza kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani ameuchakachua.
  Wanaopinga muswada huo kusomwa kwa mara ya pili wana hoja kwamba bado una upungufu mwingi, ikiwamo rais kupewa madaraka makubwa na hoja ya muungano kutojadiliwa.

  Akitoa mada katika semina hiyo, Profesa Paramagamba Kabudi alianza kueleza historia ya Tanzania na tunu ya amani, akisema imetokana na watu waliotambua utu wao na thamani ya taifa lao na kulilinda kwa gharama yoyote.

  "Mimi nitazungumzia muktadha na mawanda, sitaingia kiundani kuchambua kifungu kimoja kimoja cha muswada huo. Nimeona nianzie hapo kwa sababu hauwezi ukajadili katiba wakati hujui state (taifa) na vyombo vyake vinafanyaje kazi," alisema Profesa Kabudi.

  Aliendelea," fursa ya kutunga katiba sio fursa ya kuiacha. Wengi wamekufa bila kupata fursa hiyo na hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kufanyia marekebisho katiba yake, huu ni mchakato tu, ambao kila watu watafanya kwa wakati wao na kuwaachia wengine."

  Profesa Kabudi aliwataka wanasiasa kutotumia fursa hiyo kuleta machafuko bali kutumia ari na hamasa waliyonayo wananchi katika mchakato huo, kuongeza umoja na amani katika taifa.

  "Hamasa na ari ya wananchi ni dalili njema kama tutakuwa na mwelekeo chanya kwenye mchakato huo.. Ipo hatari ya hamasa na ari hii kutumika kwa njia hasi na kufanya mchakato huo wa kuandika katiba, kuwa wa kibaguzi. Hili ni jambo jema likitumiwa kwa mtazamo chanya, lakini ni balaa kama mchakato huo utapokewa kwa mtazamo hasi," alisema.

  Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, Katiba sio maandiko yaliyowekwa kwenye kitabu, bali ni watu na utu wao katika taifa hivyo, mchakato huo wa kutungwa katiba mpya, hauna sababu ya kuleta machafuko katika jamii bali unatakiwa kuwaunganisha wanajamii.

  "Watu wanasahau kwamba taifa ni muhimu kuliko wao, sote tutakufa, lakini Tanzania itaendelea kubaki na sio kweli kwamba Katiba inayopatikana baada ya maoni ya wananchi, haina makosi. Tujue tu kwamba sasa hii ni fursa yetu na tufanye kwa uaminifu badala ya kulumbana," alisema.

  "Leo tunaingia kwenye mjadala wa Katiba. Watu wazima tuko hapa. Hii sio mara ya kwanza kujadili maswala hayo kwa joto kali kama linavyotaka kutokea, haya yamekuwa tangu zamani, lakini cha msingi ni uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema.

  Profesa Kabudi alitolea mfano wa nchi za Checslovakia, Yugoslavia alizosema kuwa zimegawanyika na kuunda mataifa mengine kutokana na watu kutoaminiani kama inavyoanza sasa katika mchakato huo wa katiba.

  "Kwa nini tupoteze wakati kujadili jambo ambalo historia inaonyesha kwamba halijawahi kutupa shida. Tatizo sio tume w2ala kutoa maoni. Rais wetu ni mtu mwenye good will (mapenzi mema), Jamani Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.'

  Naye Profesa Romwald Haule alihoji mantiki ya wabunge kulumbana katika kupitisha muswada wa kuanza kwa mchakato, wakati bado wana fursa ya kujadili tena suala hilo wakati wa kura za maoni na baadaye kwenye bunge la Katiba.

  "Kwa nini tunalumbana na huu ni mchakato tu. Tofautishe muswadea wa kuanza mchakato na kutungwa kwa sheria yenyewe. Baada ya kuupitisha muswada huo, watu watapigta kura na wabunge mtakuwa na fursa ya kujadili tena jambo hilo katika bunge la Katiba," alisema Profesa Haule na uendelea:
  "Mimi nadhani muswada ukifikia hatua hiyo ndio tuanze kuvutana, mwenye shati alikunje vizuri na hapo ndipo tuanze kupambana, lakini sio wakati huo wa kupitisha muswada wa kuanza kwa mchakato wa marekebisho ya katiba."

  Awali akifungua semina hiyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema semina hiyo imelenga kuwapa uelewa wabunge juu ya muswada huo wa marekebisho ya katiba kabla ya kuanza kuujadili Jumatatu ijayo.

  "Semina hii ni mwanzo wa majadiliano na wakati inaendeshwa hapa Tanzania Bara pia inafanywa Zanzibar kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Lengo letu ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu suala hilo, uelewa huo utatusaidia katika kuchangia vizuri huo huu."

  Waziri Mkuu Pinda alizungumza baada ya kukaribishwa na mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala, Pinda Chana.
  Wakichangia maoni yao katika semina hiyo baadhi ya wabunge walionekana kupingana na namna wasomi haop walivyowasilisha maoni yao huku jambo lililoonyesha wazi kuwa kesho bunge litakuwa na mielekeo tofauti katika kujadili muswada.

  Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema katija jambo hilo kila mtu hawezi kumuamini mwenzake na akataka wananchi washirikishwe kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchakato huo.

  "Kwanza tulikubaliana kuwa muswada utaandikwa kwa lugha ya Kiswahili, lakini kilichotokea katika muswada ni kwamba umeandikwa Kingereza na tafsiri ndogo ndizo zipo kwa Kiswahili, hili ni kosa lakini pia nataka tuvumiliane humu ndani sio kuzomeana hovyo,''alitahadharisha Mnyika.

  Kwa upande wake Tundu Lissu alionyesha mashaka makubwa juu ya wasomi walioingia katika kuujadili muswada huo na kusema kuwa hakuna kitu walichokifanya kwani hawakuweza kujadili juu ya jambo lolote lililotarajiwa.

  Naye Christopher Ole-Sendeka alitaka maelezo ya kina kuhusu kifungu kinachomtambua mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mwanasheria wa Zanzibar ambavyo alisema vinapingana.

  Hata hivyo Kabudi alipotakiwa kutoa majibu ya maswali ya wabunge hao wote alikwepa na kusema "Nimezungumza juu juu tu lakini ninaloliamini mimi nitalisema mahali pengine, lakini pia nikikosa nafasi ya kulisema nitakufa nalo moyoni.''

  Naye Talib Ussi anaripoti kutoka Zanzibar kuwa Wajumbe wa Baraza la Wakilishi Zanzibar wameziomba Wizara za Katiba na Sheria za Serikali za jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar kusitisha kupeleka bungeni mswada wa mabadiliko ya Katiba kutokana na kuwepo mapungufu mengi.

  Hayo waliyasema wakati wakichangia katika Semina iliyo andaliwa na Wizara hizo hapo katika ukumbi wa Wizara ya Habari ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziliopo kikwajuni leo.

  Wakiyataja mapungufu hayo ni pamoja na mamlaka makubwa aliyo nayo Rais katika kusimamia mchakato mzima.

  Miongoni mamlaka ni lile la Rais kuteuwe bunge la katiba na tume itakayo simamia kura hiyo wakati ukifika.

  Katika suala hilo Wajumbe hao waliomba wananchi waachiwe kuchaguwa bunge hilo la katiba kwani suala hilo ni lao wachiwe wachaguwe wanaye mtaka awe mjumbe katika bunge hlo.

  "Bunge tulilo nalo lina saini ya siasa, lichaguliwe jengine jipya"alifahamisha Rashid Seif ambaye nu mwakilishi Ziwani

  Walisema haiwezekani Tume ya uchaguzi ya Zanzibar iandae kura ya maoni halafu matokeo yatangazwe na tume ya serikali ya Mungano."Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu kwamba tume yetu iandae kura ya maoni halafu matokeo atangaze mwene kama haaminiwi ba asipewe" Alisema Hamza Hassani Juma.

  Ama kwa wa maeneo matakatifu ambayo rasimu hiyo imeomba yasguswe walisema kifungu hicho kifutwe waachiwe wananchi wajadili cjhochote wanacho kataka katika nchi yao kwani wao ndio walengwa.

  Kasoro nyengine ni wapiga kura kwa upande wa Zanzibar watatumia buku la Vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi badala ya lile la kura."Wananchi waachiwe wajadili mungano wanavyotaka wa wasibugudhiwe na matu yeyote kwani hiyo ni haki yao "walisema.

  Naye Spika wa baraza la wakilishi Pandu Amer Kificho aliziomba Serikali zote mbili kuondoa hitlafu zliopo kwanza na baadae wafikirie mabo mengine."Hakuna haja ya kuharakisha katiba wakati kuna matatizo tele mabyo hayaja patiwa ufumbuzi" alifahamisha Kificho.

  kuja kwa mswda huo ni baada ya maoni ya Wananchi mbalimbali Tanzania walioukosoa hapo awali na kufanyiwa marekebisho.  http://www.mwananchi.co.tz/mwananchi-jumapili/40-habari-mwananchi-jumapili/17451-muswada-wa-katiba-moto-kwa-serikali.html
   
Loading...