Sophia Simba : UWT ifutwe hapa nchini ianzishwe nyingine na jina Tofauti vinginevyo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia Simba : UWT ifutwe hapa nchini ianzishwe nyingine na jina Tofauti vinginevyo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Jan 27, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Huu Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) siuungi mkono maana nimeshtuka baada ya kufatilia wanachama wake. Kihistoria Umoja huo ulianzishwa enzi za TANU mpaka hivi sasa CCM na majukumu yao ni kulinda maslahi ya CCM. Kwa vile sasa tuko kwenye mfumo wa vyama vingi ni vizuri jina libadilike na kuwa UWCT yaani Umoja wa Wanawake wa CCM wa Tanzania au Umoja wa wanawake wa CCM basi. Swali najiuliza hivi watu kama Halima Mdee......au........Josephine Mushumbusi.......au mke wangu ambaye ni mwana CDM hastahili kuitwa mwamake wa Tanzania? Umoja huu unaweza kutumia jina hili kuwadanganya hata mataifa ya nje kuwa ni ya wanawake wote walioko Tanzania kumbe ni ya wanawake wa MAGAMBA!!!

  Kwenye website ya CCM imeelezwa wazi kuwa
  "Katiba ya Kwanza ya TANU (1964) ilitambua nafasi ya wanawake, "Kutakuwa na upande wa Wanawake katika Chama, Mwanamke akishaingia katika Chama papo hapo atakuwa amekwisha kuwa mwanachama kuwa upande wa wanawake …. Kila Tawi la Chama litakuwa na upande wa wanawake na litakuwa katika Chama chini ya Uongozi wa Halmashauri ya Tawi. Wanachama wanawake na wanaume wote watakuwa sawa". Sehemu ya Wanawake iliundwa katika TANU 1955 chini ya Uongozi wa Bibi Titi Mohamed.

  Majukumu yaliyotekelezwa na Sehemu ya Wanawake yalikuwa:


  (1) Kuhamasisha wanawake kujiunga na TANU;

  (2) Kueneza TANU mijini na vijijini kwa njia ya kujitolea;

  (3) Kulinda Viongozi wa TANU: Katika hali ya kulinda Chama dhidi ya maadui, wanawake walijipenyeza kwenye vyama vya siasa na vikundi vya upinzani.

  (4) Kuimarisha TANU kifedha kupitia shughuli halali mbalimbali ikiwa ni pamoja na dansi.(my take : Ndio maana kampeni zote za Magamba midundiko na dansi muhimu, haikuanza leo maana ni sehemu ya kipato)

  (5) Kuendeleza wanachama wanawake kijamii na kiuchumi. Wanawake walianzisha madarasa ya kushona na kufuma, elimu ya watu wazima, biashara ya maduka na migahawa na vikundi vya ushirika"

  Ukitoa neno TANU liite sasa hivi CCM. Kwa hiyo wanawake wanaozungumziwa hapa ni wanawake wa Tanzania ila wale wa CCM. wale wote ambao ni wanawake kwenye vyama vya upinzani si wanawake wa Tanzania!!!!! Na kazi ya umoja wa wanawake wa sasa kama nilivyoweka RED hapo juu ni kudeal na maadui vikiwemo vikundi vya upinzani.

  Itabidi iundwe tume ichunguze ione ma -proposal yenu huwa yanaandikwa vipi na kujitambulisha vipi kwa wafadhili wenu. Msijekuwa mnapata shavu kwa jina la wanawake wa Tanzania kumbe ni wa magamba tu. Nimeishtukia hii.

  Kwa hiyo msisitizo wangu ni kuwa, Jina hilo libadilishwe ili itambulike kuwa hao ni wanawake wa CCM au Umoja huu uvunjwe na uundwe utakaoweza kuacommodate wanawake wote wa Tanzania kama inavyosomeka sasa. Nawasilisha.
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  Things Falling Apart --TFA

  Jua linachanua wana CDM meli hiyo!!!!
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Akina mama wa CDM, TLP, CUF(japo hapa nina mashaka), NCCR, CHAUSTA, nk fuatilieni hili UWT ni CCM tu jamni
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  haya members wa UWT haooooooo
  [​IMG]

  [​IMG]
  Kama nilivyoeleza hapo awali dansi ni sehemu mojawapo ya Kipato ya UWT baada ya hapo unapewa kitambaa, wali, khanga, kushney
   
 5. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,854
  Likes Received: 4,523
  Trophy Points: 280
  Hakika hii taasisi ni moja ya taasisi ambayo inaashiria ni kiasi gani wanawake wa Tanzania walivyolala na wanaosubiri "kuwezeshwa" ili wafanikiwe. Walikua wapi siku zote hizo kudai mabadiliko ya taasisi hii? Yaani wanawake wote wa Tanzania walio wanachama wa vyama vingine vya siasa na wasio wanachama wa vyama vyote, wameridhika kujuimuishwa na kudhalilishwa katika mkundo wa UWT mpaka sasa?

  Ta Muganyizi nakubaliana na wewe kabisa katika jumuisho lako.
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Tumuombe Mungu labda wataamka
   
 7. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kama wakinamama walivyooea kutuangusha.................hata kwa watakaaa kimya. Baaae watakuja kulalamika kuwa wanaonewa.
  Au kina mama toeni tamko kuwa wote nyie ni CCM
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli kitanda usichokilala haujui kunguni wake.kwenye hayo malengo ya kuwainua kiuchumi nawaungamkono but hayo mengine hayana jita sana kwa wanawake tz labda wale wanawake wa ccm
   
 9. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni nhilo ntu kuwa wanawake wepi? Wa magambatu
   
 10. m

  mussamutagaiwa Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ndomaana wakina mama wengi wana mawazo ya ki CCM kumbe haya mambo yanatokana na historia
  nakuunga mkono Ta muganyizi huu umoja ubadilishwe.
   
 11. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  ''Hata mkininyima wake zenu watanipa'' mwisho wa kunukuu! Hii ni moja ya kauli zinazotolewa na watu wa magamba wakati wa kampeni! Wanajua wanachokisema ndo maana wenzangu wa Mara waliamua kwenda na wake zao vituoni ili kupiga kura na wakifika huko wanasema hajui kusoma wala kuandika! Wote tufuate nyayo za Mara!
   
 12. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mwulizeni Prof Tibaijuka juu ya BAWATA. Alilambishwa kitumbua chenye sukari harakati zote zikaishia hewani. Bahati mbaya hata kuwaita wakina mama waliokuwa viongozi wa mikoa na wilaya akawaaga hakufanya. Leo wamebaki na makabraha ya BAWATA katika nyumba zao hawajui hata wamkabidhi nani. Ama kweli ametumia hekima ya Suleimani hata akakwaa post ya juu ndani ya serkali.
   
 13. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
Loading...