Sophia; CCM's ' Old Good Girl' Anatufundisha Nini?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Habari Kubwa Kisiasa Wiki Hii:

Sophia; CCM's ' Old Good Girl' Anatufundisha Nini?

Ndugu zangu,

Bila shaka, Sophia Simba ni moja ya habari kubwa kisiasa katika juma lililomalizika. Niliziona ishara za Sophia kufanya kama alivyofanya. Niliandika kwenye ukurasa wangu wa fb, na ikawa hivyo.

Sophia Simba kafukuzwa uanachama CCM na kabaki mkereketwa wa chama. Hilo neno mkereketwa linadhihirisha kuwa Sophia ni mwanasiasa. Kwamba alikerwa, akafanya makosa kwa chama, kaadhibiwa, kakubali adhabu na kubaki mkereketwa.

Wanahabari walipomfuata, hakuwakimbia, alijua cha kuwaambia, kwa vile kilitoka moyoni mwake.

Sophia hakuondoka na Lowassa kwa kuwa alijua, kuwa alikokwenda Lowassa siko alikolelewa na kukulia. Angekwenda asikokujua.

Sophia ameonyesha pia ukomavu kwa kukiri kitendo alichokifanya Dodoma mwaka jana ni makosa. Kwamba adhabu aliyopewa anatahili. Ushujaa wa Sophia utatokea kwenye hili. Wakati utatwambia.

Nilipoandika kuwa Sophia hatoondoka CCM niliamini hivyo kwa kurejea historia. Siku zote naandika, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri.

Historia inatuambia, kuwa kuongoza Jumuiya ya Wanawake ni heshima kubwa katika nchi yenye vyama aina ya TANU na baadae CCM. Sophia aliaminika na Chama chake kwa vile ameingia kwenye chama tangu usichana wake, mwaka 1971. Sophia amekuzwa kwenye utamaduni wa TANU na CCM. Amelelewa kwenye misingi ya kiitikadi. Hata baada ya kufukuzwa uanachama, akiongea na watangazaji wa habari, tumeona, kuwa rhetoriki, kwa maana namna ya uzungumzaji wa Sophia, ni wa Ki-TANUTANU na Ki- CCMCCM.

Sophia anajua nguvu za chama tawala Afrika, na hususan Chama cha Kiitikadi- Ideology Party. Sophia sio tu amesoma habari zao, amekutana na kufundwa na akina mama wa shoka kupata kutokea nchi, ni wanawake aina ya Bibi Titi Mohammed na Sophia Kawawa. Wawili hao wamekuwa viongozi kwenye jumuiya ya wanawake TANU na CCM kitaifa.

Wawili hao wamepata kutofautiana na wenyeviti wao, lakini, hawakupata kuhama chama chao. Mmoja wao alipata hata kutiwa gerezani. Na alipotoka akakaa kimya hadi kuanza kuitwa kwenye shughuli za chama miaka ya 80.

Bibi Titi Mohammed na Sophia Kawawa wote wana mitaa iliyoitwa kwa majina yao kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Yumkini, Sophia, CCM ' Old Good Girl', aliteleza kisiasa, nani asiyeteleza?

Maggid Mjengwa.
 
Attachments

  • 2.jpg
    2.jpg
    6.7 KB · Views: 35
Ana deny unabii uliofanywa na wengi ndani ya chama tu, its about time...... she will teach them a lesson the hard way...
Polepole ajitokeze afukuzwe na " ukereketwa wake"... otherwise, she is there to stay and do her job quite well, very well.

Anachofanya anatafuta sympathy ya loyal members ionekane ameonewa alaf game inaanza round 1..... she is so fxsf@ng smart.
 
Kila kitu kina mwisho, kwahiyo hata uongozi wa chama uliopo sasa hivi unapita tu, na huyo mama analijua hilo.
 
Hivi huyu Bibi Titi ni nani hasa? Mwenye japo kawasifu na kapicha (najua video zilikuwa bado) twake turushieni humu.
 
Mkereketwa - mtu anayesumbuliwa na kitu kisicho cha kawaida.... Mathalan: kikohozi kinakereketa Koo...
 
Habari Kubwa Kisiasa Wiki Hii:

Sophia; CCM's ' Old Good Girl' Anatufundisha Nini?

Ndugu zangu,

Bila shaka, Sophia Simba ni moja ya habari kubwa kisiasa katika juma lililomalizika. Niliziona ishara za Sophia kufanya kama alivyofanya. Niliandika kwenye ukurasa wangu wa fb, na ikawa hivyo.

Sophia Simba kafukuzwa uanachama CCM na kabaki mkereketwa wa chama. Hilo neno mkereketwa linadhihirisha kuwa Sophia ni mwanasiasa. Kwamba alikerwa, akafanya makosa kwa chama, kaadhibiwa, kakubali adhabu na kubaki mkereketwa.

Wanahabari walipomfuata, hakuwakimbia, alijua cha kuwaambia, kwa vile kilitoka moyoni mwake.

Sophia hakuondoka na Lowassa kwa kuwa alijua, kuwa alikokwenda Lowassa siko alikolelewa na kukulia. Angekwenda asikokujua.

Sophia ameonyesha pia ukomavu kwa kukiri kitendo alichokifanya Dodoma mwaka jana ni makosa. Kwamba adhabu aliyopewa anatahili. Ushujaa wa Sophia utatokea kwenye hili. Wakati utatwambia.

Nilipoandika kuwa Sophia hatoondoka CCM niliamini hivyo kwa kurejea historia. Siku zote naandika, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri.

Historia inatuambia, kuwa kuongoza Jumuiya ya Wanawake ni heshima kubwa katika nchi yenye vyama aina ya TANU na baadae CCM. Sophia aliaminika na Chama chake kwa vile ameingia kwenye chama tangu usichana wake, mwaka 1971. Sophia amekuzwa kwenye utamaduni wa TANU na CCM. Amelelewa kwenye misingi ya kiitikadi. Hata baada ya kufukuzwa uanachama, akiongea na watangazaji wa habari, tumeona, kuwa rhetoriki, kwa maana namna ya uzungumzaji wa Sophia, ni wa Ki-TANUTANU na Ki- CCMCCM.

Sophia anajua nguvu za chama tawala Afrika, na hususan Chama cha Kiitikadi- Ideology Party. Sophia sio tu amesoma habari zao, amekutana na kufundwa na akina mama wa shoka kupata kutokea nchi, ni wanawake aina ya Bibi Titi Mohammed na Sophia Kawawa. Wawili hao wamekuwa viongozi kwenye jumuiya ya wanawake TANU na CCM kitaifa.

Wawili hao wamepata kutofautiana na wenyeviti wao, lakini, hawakupata kuhama chama chao. Mmoja wao alipata hata kutiwa gerezani. Na alipotoka akakaa kimya hadi kuanza kuitwa kwenye shughuli za chama miaka ya 80.

Bibi Titi Mohammed na Sophia Kawawa wote wana mitaa iliyoitwa kwa majina yao kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Yumkini, Sophia, CCM ' Old Good Girl', aliteleza kisiasa, nani asiyeteleza?

Maggid Mjengwa.

Umenena vyema. Huyu ni Kada anaeamini katika chama chake. CCM imeundwa kikada tangu miaka ya chama kimoja kwani kilikua ni chama dola. makada wa rika mbali mbali walitengenezwa uraiani na jeshini. Ndio maana leo mjeshi akistafu anakuwa ccm.
na Umri wake nao pia unamfanya kuacha kuhangaika na vyama vingine. Lakini kwa kawaida wana siasa haastaafu kihivyo hata kama amefukuzwa na kuamua kupumzika. anaweza kuwa mshauri mzuru uchaguzi ujao kwa kusapoti japo kwa maneno tu kuwa fulani ni bora hata kama hatoki ccm...haya tumeyaona kwa akina Powell kule US amekua mwana chama wa Republican lakini alimsapoti Obama n.k
hivyo akina Sophia watumie uzoefu wao kutusaidia kuchagua viongozi wazuri bila ya ukereketwa
 
Alijua akienda kule itakuwa ni "wrong turn" and she will be "left for dead"..huyu anatupa sign nzuri kuwa mwisho wa kina lowassa ni kurejea ccm..time will tell
 
Habari Kubwa Kisiasa Wiki Hii:

Sophia; CCM's ' Old Good Girl' Anatufundisha Nini?

Ndugu zangu,

Bila shaka, Sophia Simba ni moja ya habari kubwa kisiasa katika juma lililomalizika. Niliziona ishara za Sophia kufanya kama alivyofanya. Niliandika kwenye ukurasa wangu wa fb, na ikawa hivyo.

Sophia Simba kafukuzwa uanachama CCM na kabaki mkereketwa wa chama. Hilo neno mkereketwa linadhihirisha kuwa Sophia ni mwanasiasa. Kwamba alikerwa, akafanya makosa kwa chama, kaadhibiwa, kakubali adhabu na kubaki mkereketwa.

Wanahabari walipomfuata, hakuwakimbia, alijua cha kuwaambia, kwa vile kilitoka moyoni mwake.

Sophia hakuondoka na Lowassa kwa kuwa alijua, kuwa alikokwenda Lowassa siko alikolelewa na kukulia. Angekwenda asikokujua.

Sophia ameonyesha pia ukomavu kwa kukiri kitendo alichokifanya Dodoma mwaka jana ni makosa. Kwamba adhabu aliyopewa anatahili. Ushujaa wa Sophia utatokea kwenye hili. Wakati utatwambia.

Nilipoandika kuwa Sophia hatoondoka CCM niliamini hivyo kwa kurejea historia. Siku zote naandika, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri.

Historia inatuambia, kuwa kuongoza Jumuiya ya Wanawake ni heshima kubwa katika nchi yenye vyama aina ya TANU na baadae CCM. Sophia aliaminika na Chama chake kwa vile ameingia kwenye chama tangu usichana wake, mwaka 1971. Sophia amekuzwa kwenye utamaduni wa TANU na CCM. Amelelewa kwenye misingi ya kiitikadi. Hata baada ya kufukuzwa uanachama, akiongea na watangazaji wa habari, tumeona, kuwa rhetoriki, kwa maana namna ya uzungumzaji wa Sophia, ni wa Ki-TANUTANU na Ki- CCMCCM.

Sophia anajua nguvu za chama tawala Afrika, na hususan Chama cha Kiitikadi- Ideology Party. Sophia sio tu amesoma habari zao, amekutana na kufundwa na akina mama wa shoka kupata kutokea nchi, ni wanawake aina ya Bibi Titi Mohammed na Sophia Kawawa. Wawili hao wamekuwa viongozi kwenye jumuiya ya wanawake TANU na CCM kitaifa.

Wawili hao wamepata kutofautiana na wenyeviti wao, lakini, hawakupata kuhama chama chao. Mmoja wao alipata hata kutiwa gerezani. Na alipotoka akakaa kimya hadi kuanza kuitwa kwenye shughuli za chama miaka ya 80.

Bibi Titi Mohammed na Sophia Kawawa wote wana mitaa iliyoitwa kwa majina yao kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Yumkini, Sophia, CCM ' Old Good Girl', aliteleza kisiasa, nani asiyeteleza?

Maggid Mjengwa.
Mkereketwa maana yake nini hapo,mama asijipe moyo eti akibaki kuwa mkereketwa hawa jamaa watamuheshimu hakuna lolote wameshakivunjia heshima hao,kama utaki tena siasa kaaa kimya tu,mamangu.
 
Hiv huyu mama ni jambo gani amelifanya kwa taifa hili, ushawishi wake mbona siuoni kwa jamii.
Mnamkuza tu ila hakuna chochote alichokifanya kwa taifa zaidi ya U-ccm wake.
 
Back
Top Bottom