pole mkuu,
kuna ndugu yangu alikuwa anatatizo kama lako. alifanya kila ishu ya ku factory na hata ku root.
tatizo hapo ni wewe uliweka line (sim card vibaya), vipini vya kusomea line havigusi bati ya dhahabu ya sim card vizuri.
nilimtengezea ndugu yangu kwa kunyanyua vipini vya simu (sim card slot reader) na ishu ikasoma network.
sikushauri ufanye wewe mwenyewe, lakini hebu chunguza kwanza sehemu ya kuweka sim card uone kama vipini vipo sawa. kawaida vipini vipo vitatu ukiona viwili ujue kimoja kimelala au kimekatika. kama bado kipo kazi ni rahisi ya kukiinua tu na network itasoma.
hope nimekusaidia.