Songombingo ya uke wa fisi

Songombingo ya uke wa fisi

juma sal

Senior Member
Joined
Dec 18, 2011
Posts
156
Reaction score
88
Kuna mengi yakustajabisha na kushangaza kuhusu wanyama, hasa tabia, hulka, mionekano hata mienendo yao.

Kuna ambao wanaguswa na kuwapenda simba kunakutokana na muonekano na tabia za simba, wapo wanauguswa na mamba, tembo, nyati, faru, nyoka, lakini binafsi naguswa mno na fisi madoa (spotted hyena).

Mapenzi yangu kwa fisi yanatokana na mengi sana, moja likiwa ni ukweli kua fisi ni mnyama pekee mwenye kinga madhubuti dhidi ya magonjwa inayompa jeuri ya kula mizoga bila kuugua kizembezembe.

Na haikua ajabu sana wakati wanyama wengi wala nyama yaani carnivores walipokumbwa na magonjwa (Canine) miaka ya 90 barani Afrika, ni fisi pekee ambao hawakuathirika.

Ukiacha hilo fisi anatambulika kama mnyama aliezivunja kanuni kadhaa za mammals (Violets mammals's rules) Kwa kawaida inajulikana kua

1. Wanyama wengi madume wanakua wakubwa kimaumbile kuliko majike
2. Madume wanakua wakali kuliko majiki
3. Madume ndio watawala wakati majike yanafata mkumbo.

Sasa ukija kwa fisi kanuni zote hizo hapo amezivunja na yupo kinyume nazo, kwa maana kua majike ni makubwa, wakali na watawala kuliko madome, madume ya fisi ni dhaifu kuliko majike. Wanaume gani hawa (wa Dar?)!!! Haah!

Eneo lengine linaloshangaza sana ni jinsia yake hasa uke (vigina, nyabe) whatever you call it, it's up to you.

Huwezi kutambua jinsia ya fisi kwa kumuangalia sehemu za siri, Kwasababu zinafanana utaishia kusema hakuna majike bali wote ni madume. Ugumu huu umefanya hata jamii nyingi kuamini hakuna fisi jike na hata wengine kumuhusisha na imani za kishirikina.

Kama tunavyojua wanyama wengi majike uke (vigina) unakua nyuma ya mkia chini ya njia ya haja kubwa na bidhaa za kiume zinakua katikati ya miguu katika mafungu mawili ya uume (penis/dushelele) na kifuko cha pum.b.u (scrotum au kwa lahaja ya kimafia zinaitwa kodo). Ukimuangalia fisi jike kwa nyuma hana hiyo bidhaa ya kike kwa nyuma kama wanyama wengine ispokua utaona wote majike na madume wana bidhaa za kiume yaani uume na kifuko cha pum.b.u (penis na scrotum)

Sasa ndugu msomaji utakua ujiuliza je ni kweli fisi ni madume pekee? Wanazaanaje na Wanapandanaje?

Nianze kwa kusema kinachoonekana kama kifuko cha pum.b.u kwa fisi jike sio pum.b.u kabisa bali ni sehemu za nje za uke (vulva, mashavu?) zilijikunja na kufanya zionekane kama pum.b.u. kwahiyo fisi jike hana Kodo!! Sawa sawa?

Pili kinachoonekana ni kama uume kwa fisi jike sio uume ( ni pseodo penis). Huu ndio uke wa fisi unaofanya kazi kama uke mwengine wowote zikiwepo kukojolea (urinate), kufanyia mapenzi ( sex) na kuzalia (birth giving). Uke huu wa fisi unaonekana kama uume mnene wenye urefu wa nchi saba (7inches). Na kitaalamu inatajwa hiki cha fisi jike kinembe (clitoris) kilichorefuka ambapo shimo la uke linakua katikati yake.

Kufanya mapenzi kwa fisi (tendo la jimai) ni sawa na kusema uume unaingia kwenye uume mwengine. Hili linawezekana kwa kua uume halisi wa dume ni mwembamba ukilinganisha uume feki wa jike ambao ndio uke ndani ya kinembe(ashakum si matusi). Sawasawa?

Mpendwa msomaji unaweza ukajiuliza inawezenaje na ni ngumu kiasi gani?

Suala la fisi kupandana ni mtihani mzito hasa kwa fisi dume kwakua inahitaji mahesabu makali ya kulenga shimo la uke ndani ya kitu kama uume mwengine. Mara nyingi fisi dume na jike hufanya mazoezi ya mwezi mpaka kuweza kufanikisha kutumbukizana dudu sehemu husika!!!

Ugumu huu wa kuilenga dudu ya jike ambayo mwenye anaamua aininginize au arudishe ndani ndio inayofanya kua kufanya mapenzi kwa fisi kua tendo la hiari kwa jike na haiwezekani kwa fisi jike kubakwa, akifanywa basi ujue kapenda!, sawasawa?

Ugumu huu wa kutambua jinsia ya fisi umewahi kuwapelekea wafanyakazi wa zoo mmoja nchini Japan kwa miaka minne kuwapandisha fisi wawili ili wazaane bila mafanikio mpaka walipogundua kua wote kua ni vidume banaa!!!

HITIMISHO
Fisi jike kua na tabia za kidume kama ukali, misuli, mwili mkubwa, ubabe pamoja na kua na uke na kinembe kirefu kama uume (dushelele) kunatajwa kuchangiwa na kiwango kikubwa cha uwepo wa hormone za kiume aina ya testosterone kwa fisi jike kinyume kabisa na mamalia wengine.
 
umenikumbusha mbali sana!!nilisha wahi kula 20,000 ya mtu kisa ni kubisha kuwa fisi wote ni madume!!tena walikuwa wanabisha hasa hadi mapovu nikawaambia kweli mnabisha?nikamchukua rafiki yangu GOOGLE,malaa paa maelezo ya kutosha na picha kabisa!!nikachukua wekundu wangu wawili huyo hadi kwa mdudu!!!hadi leo wananiita BWANA MIFUGO!!!
 
Wakati fulani nilikuwa mkoa akafa mbwa jirani, wakati najishauri jinsi gani kesho yake nitamtafuta mwanakijiji afukie mzoga, usiku wakapita fisi wakamtafuna bila kuacha masalia huku wakichekelea!
 
Fisi ni mnyama wa ajabu sana anaweza kimbizwa vibaya sana na mtoto wa miaka 6-7 lakini anamla mbwa! Ambaye ni hatari kuliko mtoto au mtu mzima.
 
Kingine ulichosahau ni kwamba jamaa wananusa vibaya sana na ku cheka ovyo.
Wanachekeleaga mazaga, au wanatekeny'ana yaani ni sawa na mlevi aone balimi lazima akene usoni au moyoni.
 
Tofauti na watu wanavyofikiri,fisi na mbwa mwitu ndio wanyama ambao wana jeuri ya kuwakimbiza simba,fisi anaweza kufanya rabsha kwenye karamu ya simba hadi simba akaacha kula windo lake lote.nguvu za fisi na mbwa mwitu ni umoja wao wanapomkabili au kuwakabili simba,ikumbukwe kuwa jeuri ya simba ni umoja wao,simba peke yake hawezi kuwinda na kuua mnyama kama nyati ndio maana akizeeka na kutengwa hukimbilia kula watu.Tatizo la fisi ni kuwa yeye anasubiri chakula kwenye poti,yeye hatafuti anasubiri msosi mezani ndio avamie.
 
Back
Top Bottom