Somo la ndoa na maisha ya ndoa

Somo la ndoa na maisha ya ndoa

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,758
Reaction score
39,494
Habari wandugu na jamaa....natumaini nyote ni wazima na wenye afya njema na wale wenye kuumwa Mungu awafanyie wepesi katika kipindi hicho kigumu.......

Kwanza kabisa tunatakiwa tujue Ndoa ni nini na misingi ya ndoa nini.....!!

-Ndoa ni muunganiko wa watu wawili mwanamke na mwanaume waliounganishwa na upendo wa dhati mioyoni mwao...maana yake ni kwamba muunganiko wowote unaoenda kinyume na tafsiri hiyo huo ni batili

Kufunga ndoa na mtu mliyependana ni jambo lingine na kudumu kwenye ndoa ni jambo lingine

Ndoa inayodumu inakuwa imejengwa kwenye msingi imara na muhimu kwa ajili kuishi watu wawili......

-Misingi ya ndoa imara
Kama nilivyoainisha mwanzo kuwa ili ndoa idumu inatakiwa iwe kwenye misingi imara ambayo itafanya sio tu ndoa iwe yenye kudumu bali pia iwe yenye furaha baina ya wanandoa....

Ifuatayo ni misingi ya ndoa imara

~ Uvumilivu
Huu ndio msingi wa kwanza na mkuu kwa sababu pamoja na kuwa na upendo kati yenu lakini vile vile nyie ni wanadamu na kila mmoja sio mkamilifu na kuna muda mnakengeuka , Kwa hiyo ukishayatambua haya unapaswa kumvumilia mwa ndani wako na huku ukimuweka sawa.....

~ kuheshimiana
Haijalishi huyo mtu atadai anakupenda kwa kiwango gani ikiwa hakuheshimu basi huyo atakupa wakati mgumu sana kwenye maisha ya ndoa.....wanandoa wanapaswa kuheshimiana ili kujenga maelewano yenye furaha baina yao......huku kila mmoja akijua mipaka yake kwenye muunganiko huo.....

~Kuthaminiana
Kumthamini mtu ndio kunakodhihirisha upendo wako kwa mtu huyo....usiyempenda kamwe huwezi kumthamini na asiyekupenda hawezi kukuthamini...kuthaminiana kunadumisha ndoa kwa kuwa kila mmoja atajiona ana umuhimu kwenye muunganiko huo....

~Kufarijiana
Kila mwanadamu anapenda Faraja hasa akiwa kwenye nyakati ngumu....hasa pale faraja hiyo inapotoka kwa mtu wako wa karibu kama mume au mke ni jambo linalogusa mpaka uvungu wa moyo.....

~ Kuliwazana
Hili halina haja ya kulijazia maneno mengi kwa kuwa liko wazi....

NB;
Ndoa ni muunganiko wenye furaha kwa wawili waliopendana.....

Nawasilisha......
 
Tusiruke ukuta (tusionje nje), 15." Unywe maji ya birika lako mwenyewe,
Na maji yenye kububujika katika kisima chako.
16.Je, Chemchemi zako zitawanyike mbali,
Na mito ya maji katika njia kuu?

17.Yawe yako mwenyewe peke yako,
Wala si ya wageni pamoja nawe.

18.Chemchemi yako ibarikiwe;
Nawe umfurahia mke wa ujana wako. =>MITHALI 5:15-18, *BHN (BIBLIA YA HABARI NJEMA), GOOD NEWS BIBLE.
*UNION BIBLE VERSION.
 
Na kwenye ndoa msipelekane kijeshi. It is not a death sentence.

Chezeni michezo ya pamoja, not just sex. Pillow fights, bebaneni mtekenyane.... just be silly.

Be friends... be each others best company. Look out for each other and stay away from negative energy that emanates from friends who are either single or have broken marriages.
 
You have nailed it
Bravo
 
Take it, Take another like!
 
Back
Top Bottom