Somo kwa wazazi wote

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
KAMA WEWE NI MZAZI USIACHE KUSOMA

Nyakati na Technology zimeharibu mambo mengi sanad Tanzania.Wanawake wenye akili wasio na elimu walizaa na kulea ma Professors .

Nyakati hizi wanawake wasomi wanashindwa kuzalisha vizazi bora vya watoto wenye adabu,hekima na maarifa.

Nyakati hizi mwanamke jinsi anavyozidi kuelimika ndivyo anazidi kupoteza vinasaba maridhawa vya mke mwema na mama bora .

Uadirifu,unyenyekevu,lugha nzuri na majukumu ya mwanamke kwa mume imekuwa misimiati kwa asilimia kubwa kwa wanawake wasomi mwenye ndoa zao.

Mzazi anafurahia mtoto kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha,lakini mtoto hana adabu,ni mjeuri na mwenye kiburi,social media wazazi tunapost picture za watoto wetu kwa ubora wa mavazi na uzuri wa sura lakini hatujivunii haiba na tabia njema za watoto.

"She is my happines" mwingine utasikia "He is my handsome" lakini mtoto anamjua vyema house girl kuliko Mama.Wengi wamejificha kwenye kazi inachukua muda wangu mwingi nashindwa kukaa na mwanangu.

Wengine tumelelewa na wazazi ma -Nurse anaingia night lakini,tulisoma na kuimba table ya 1-12 ndio tulipewa ruhusa ya kwenda kucheza,tulifundishwa kufua na kupiga pasi na bado mzazi alikuwa busy na kazi.

Mtoto ni wa mama ,mama akikosa busara na hekima ya kulea watoto anaharibu kizazi chake,ukweli mchungu Tanzania divorce rate kubwa ni ya wanawake wasomi na wanaume wasomi,ndoa za watu ambao sio wasomi kuna ushirika na upendo mkubwa sana.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanamke mwenye akili asiye na elimu na mwanamke mwenye elimu asiye na hekima na busara.

Busara ina unyenyekevu,uvumilivu,adabu na utu, wanawake waliokosa busara utawagundua kwa show off na kauli zao.Jiulize mtoto wa kike wa miaka 8 anafuliwa chupi,anaandaliwa chai,kumiminiwa chain na anawekea sukari baba na mama wanaona ni haki.

Mtoto wa kike anasoma kidato cha nne anatumia IPhone 6 ,baba anatumia Techno ,mama anatumia Techno, mtoto anaongea na simu usiku kucha ,hakuna anayehoji simu kapata wapi,na pesa ya kununua airtime anapewa na nani?

Wazazi huwa wanahoji mimba ya nani na sio simu kakununulia nani?Mabinti wanapenda kusema,"Nataka mwanaume mrefu aliyejazia "baba yake mfupi na ana kitambi ,mama yako sio mjinga binti.

Wanaume wanapenda kuoa mwanamke mwenye kazi nzuri na elimu nzuri ,baba yako hakuwa mjinga kuoa mama yako darasa LA saba na kwenye ndoa miaka 40 na hakuna picture ya anniversary ya ndoa miaka 40 kwenye social media.

Vijana ambao hamjao wala kuolewa ,kigezo cha mke/mume mwema ni akili yake na sio elimu yake. Mungu humpa mtu kilicho bora.

Tujifunze kulea watoto kwa adabu,unyenyekevu na nidhamu na kukemea na kuadhibu kwa haki,tusijifiche mwenye kivuli cha kazi na ubusy.Binti anayefuliwa chupi miaka 10 anawezaje kuwa mke mwema?

Jiulize ni Mara ngapi umesali na mwanao kila aendapo shule? Ni Mara ngapi umeosha vyombo na binti yako? Ni Mara ngapi umemwambia mwanao baba/mama yako ni mtu bora kwangu na kwako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna haja ya wanajopo kukaa chini na kutafuta tafsiri sahihi ya neno "MSOMI"
Nimeshuhudiwa wapumbavu wengi wakiitwa wasomi kitu ambacho sio sahihi
 
Back
Top Bottom