Somo kwa uvccm

Somo kwa uvccm

Joined
Feb 26, 2013
Posts
30
Reaction score
47
TAARIFA KWA UMMA NA ELIMU KWA UVCCM.

Bavicha Mkoa wa Arusha unatoa taarifa kwa umma wa watanzania na Elimu bora ya bure kwa Uvccm

1. Arusha ndio eneo pekee lenye Azimio lenye Tumaini kwa Watanzania, Azimio la Arusha. Ukombozi wa wauchumi wa watanzania ulinzia hapa, hivyo basi Bavicha Mkoa wa Arusha Unaunga Mkono "UKUTA" azimio lililotolewa na Kamati Kuu ya Chadema tar 27/7/2016.

2. Elimu kwa umma, ni vema Vijana wote wa Mkoa wa Arusha kujua nini maana ya UKUTA na Umuhimu wake.

OPERESHENI UKUTA NI KIFUPI CHA OPERESHENI YA UMOJA WA KUPAMBANA NA UDIKTETA TANZANIA

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika utangulizi kuna maneno yameandikwa na ambayo yamekaziwa na sheria namba 15 ya mwaka 1984 ibara ya 3 na sheria namba 1 ya mwaka 2005 ibara ya 3. Katika utangulizi huo wa katiba yetu imeandikwa kama ifuatayavyo;

“KWA KUWA Sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani” “NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia, ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
Aidha kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana ibara ya 3 (1) inasema kuwa “Jamhuri ya Muungano ni Nchi ya Kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”

Ni dhahiri kuwa kama BAVICHA tuna wajibu na haki ya kuilinda na kuitetea Katiba ya Nchi na kuhakikisha kuwa haivunji na yeyote na misingi ya Kidemokrasia ambayo ilijengwa kwa miongo mingi inaendelea kuimarika, kulelewa na kukuzwa mara dufu.

KWANINI TUNAUNGA MKONO UKUTA

Kwanza tunakupongeza sana Mh Mwenyekiti (T) Freeman Mbowe na Kamati kuu kwa kuja na operesheni UKUTA, Kiukweli mmedhihirisha Chadema ndio Tumaini pekee la watanzania.

Bavicha Mkoa wa Arusha tumefurahi na tunaahidi hatutakuangusha kwani hili ndilo jambo pekee tunaloweza kufanya kwa maslahi mapana ya taifa letu, pia sisi ndio tunaotarajiwa kubadili hali mbaya ya uminywaji wa Demokrasia ambayo kimsingi tunaona viashiria vya kumsababisha kijana kuwa fukara, bila demokrasia hakuna maendeleo.

3. Elimu Bora ya bure kwa UVccm, kiukweli tumesikitishwa na tamko la vijana hawa wa Mkoa wa Arusha na Arusha Mjini kimsingi ni aibu na fedheha kwa Vijana kumtukana Mbunge wa Arusha Mjini kwa kigezo cha kumtetea DC.
Tunashangazwa vijana wasio na nidhamu na adabu kama nyie kuwa viongozi. Tunapenda kuwaelimusha kuwa Viongozi wakuu wanapotofautiana kwa namna yoyote, vijana si kazi yenu kutumia fursa hiyo kutafuta posho ya vikao haramu vya hujuma na shutuma kwa viongozi wa wananchi kama Mh Mbunge wa Arusha Mjini.

Uvccm mmeendelea kuthibitisha kuwa hamjui ni kwa kiasi gani vijana wa Arusha wameathiriwa na maamuzi ya awamu ya tano. Basi tuwaeleze jinsi vijana wamekwamishwa

1. Wasomi maelfu waliohitimu mwaka jana 2015 hawakuajiriwa na watakaohitimu mwaka huu 2016 hawatajirajiwi kuajiriwa, wengi wao ni vijana wanaendelea kuwa tegemezi na mzigo kwa taifa.

2. Serikali ya viwanda niya nadharia isiyotekelezeka, Arusha viwanda vingi vimekufa mfano General Tyre n.k vingeweza kuajiri maelfu ya vijaña wakitanzania ila nyie Uvccm hamuoni umuhimu wa kuwatetea vijana bali kutukana viongozi kwa maslahi ya posho ya kikao.

Hivyo basi Bavicha Mkoa wa Arusha unawaonya na kuwakanya Uvccm kuacha kabisa kutukana viongozi wetu hasa Mh Mbunge wa Arusha Mjini ambaye ni shujaa wa kutete demokrasia nchini.

Tunawataka nyie kama wapinzani mkoa huu mjikite kwenye kujenga demokrasia na maendeleo ya watanzania na chama chenu kilichopoteza dira na mwelekeo na kukataliwa wa asilimia 90 uchaguzi mkuu 2015.

Hitimisho.
Ni hakika na kweli kuwa UKUTA UTAJENGWA tokea Arusha, ni ahadi yetu kwa Chama kuwa ni UKUTA utafanikiwa kwa ufanisi na kiwango cha juu, tunaomba kumtia moyo Mbunge wa Arusha Mjini kuendelea kuitetea demokrasia nchi hii, nasi kama nguvu ya mabadiliko tutaitetea UKUTA kwa ufanisi wa demokrasia na maendeleo ya taifa letu Tanzania.

TUKUTANE SEPTEMBA MOSI

(UKUTA- 2016)

BAVICHA MKOA WA ARUSHA
 
Bahati Mbaya BAVICHA wengi hakuna familia. Kamateni UKUTA ili tuwe tunawasoma wakati mkiwa hamna miguu hata kufa pia.

Siasa za kibabe tu sa hivi hakuna kulemba.
Kuja mfahamu kwamba huu ni uongozi mwingine mshajaza orodha ya wafungwa, majeruhi wa siasa na marehemu pia.

Mlimtukana JK mlinzani hiyo dhambi inakomea hapo wacha msomeshwe namba hamkujua kesho itakujaje?

Acha watukanwe akina Lema ili wawe na adabu, tena sasa hivi mashambulizi wapeleke na Singida kwa Lisu atukanwe ndo ajue maumivu.

Septemba Mosi ni kuandaa Ambulance ili kujishaua
 
Bahati Mbaya BAVICHA wengi hakuna familia. Kamateni UKUTA ili tuwe tunawasoma wakati mkiwa hamna miguu hata kufa pia.

Siasa za kibabe tu sa hivi hakuna kulemba.
Kuja mfahamu kwamba huu ni uongozi mwingine mshajaza orodha ya wafungwa, majeruhi wa siasa na marehemu pia.

Mlimtukana JK mlinzani hiyo dhambi inakomea hapo wacha msomeshwe namba hamkujua kesho itakujaje?

Acha watukanwe akina Lema ili wawe na adabu, tena sasa hivi mashambulizi wapeleke na Singida kwa Lisu atukanwe ndo ajue maumivu.

Septemba Mosi ni kuandaa Ambulance ili kujishaua
Kilichoandikwa hapo juu ni msaada kwa taifa zima kukiwa na hoja za msingi kabisa zenye manufaa makubwa tu hata kwa uvccm lakini kwa mshangao mkubwa umejibu mipasho isiyo na tija hata kwa mwendawazimu
 
Safi lakini je kila mwaka wanafunzi waliokuwa wakihitimu walipata ajira wote,kuhusu viwanda ukilia arusha tanga nafikiri wao walitakiwa wagaregare kwenye vumbi,cha msingi hapa ni ukuta!
 
Back
Top Bottom