Kwa kuanza kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, nitakuwa natoa hapa elimu juu ya marekebisho ya simu(phone repair) aina zote, mafunzo yangu yakuwa yanaegemea zaida kwenye katika matatizo ya hardware.
Nitatoa ufafanuzi wa matatizo mbali mbali katika simu na kuyatolea maelekezo ya amna ya kuyatatua.
Lengo ikiwa ni kukupa elimu kuhusu matatizo ya simu, na kupata mwanga zaidi, hata linapotokea tatizo katika simu yako ule wasi wasi unakuwa haupo tena sababu tayari utakuwa unalitambua tatizo na unajua nini cha kufanya.
Na utakapo peleka kwa fundi unajua nini simu yako inaenda kurekebishwa itakusaidi pia kuepuka gharama zisio na ulazima kwa vile unajua tatizo, hivyo itakupa uwezo wa kukabiliana na zile longo longo za mafundi.
Kwa leo nitaanza na simu ya nokia 1280 hii ni aina ya simu ambayo ni nzuri sana kwa wale ambao wameshaitumia wanajua, ni simu ambayo imepata umaarufu sana hapa Tanzania, ina watumiajia wengi, binafsi ni simu ambayo ninayo japokuwa nini smartphone,kwa sasa kuna wajanja wamesha toa aina hiyo ya simu ambazo sio imara kwa hiyo inakupasa kuwa makini unapoenda kununua...
Mic ni kifaa kinachotumika kunasa sauti yako na kusafirisha kwenda kwa yule unaewasiliana naye.
Simu inapokuwa na tatizo la mic yule unaempigia anashindwa kukusikia, utaishia kumsikia akisema hallo hallo huku yeye hakusikia hata kidogo unapo ongea.
Katika hii simu mic inakuwa katika muonekano huu ndani ya simu
RED YENYE MDUALA:MIC
RED YENYE UMBO MRABA:
NJIA ZA MIC( MIC WAY)
MAREKEBISHO
kawaida mic huwa hazi rekebishwi kinachofanyika ni kuitoa na kuweka nyingine.
Kuna kifaa maalumu(brower) kinacho tumika tuyeyusha hapo na kuitoa hiyo mic na kupachika nyingine kwa kuichoma.
NB;
Kwa kawaida mic ni tatizo ambalo limekuwa likitokea sana, hasa kwenye simu za kichina tofauti na simu nyingine.
Hapa nitajibu maswali yote anayohusiana na mic kwa upande wa simu nokia 1280 tu, kutokana na maelekezo hayo mafupi..
Nitajitahidi kutoa soma kawa simu mbali mbali na matatizo yake kulingana na muda utakavyo ni ruhusu kupitia hapa hapa, utaratibu utakuwa ni kila baada ya siku mbili nitakuwa nakuja kujadiliana na nyie hapo.
Baada ya kuhitimisha hili zoezi nitakuja na matatizo yafuatayo kutoka katika hiyo simu;
1
.Speaker
2.
mwanga wa batani na kioo
Haya ndo matatizo makuu ya hizi simu..