SIMULIZI YA KWELI
USIOLEWE SHANGAZI
EPSODE YA KWANZA
KIBOSHO MOSHI 2013
Joan binti wakichaga na mhitimu wa stashahada ya ualimu katika chuo cha ualimu Butimba akiwa nyumbani kwao na wazazi wake huku akisubiria ajira ya serikali kama utaratibu wa nchi ulivyokuwa.
Jioni hii ilimkuta Joan na wazazi wake katika mjadala mzito sana mara baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku.
"Mwanangu nafikiri ulipata elimu uliyonayo ili ikusaidie kujikomboa kutokana na ujinga na sio ikusaidie kupata kazi"
"Nalifahamu sana hilo babangu"
"Na wakati mnasoma huwa mnakutana sana na msemo usemao asiyesikia la mkuu huvunjika mguu na ule mwingine wa lisemwalo lipo na kama halipo basi laja"
"Nafaham pia baba lakini katika hili langu mimi naomba msitumie hiyo misemo tafadhali"
"Unahisi kwanini wewe hutaki misemo hii ifanye kazi kwako na kwa wengine uamini inawezekana?!"
"Baba hiyo ni misemo tu, na naamini tukiishi kwa kufata kila msemo na methali basi hatutafika popote pale baba,ngoja nikupe mfano mdogo tu hapa! sisi wachaga huko nje makabila mengine wanaamini kuwa sisi wanwake wa kichaga tukishaolewa na waume zetu wafanikiwe sana basi tunawaua na kurithi hizo mali, je hilo ni kweli? "
"Lakini si lina ukweli ndani yake mwanangu?"
"Ukweli upi baba? wamachame pekee sindio wanaofanya hivyo na tena sio wote! kwa kuangalia huo msemo basi naomba muamini kuwa sio kuwa kwa sababu mchumba wangu huyo kwa sababu kabila lake lina sifa mbaya ya unyanyasaji kwa wanawake basi hata mimi lazima ataninyanyasa,kumbuka sio wote baba na pia kumbuka kuwa huyu ni msomi baba hivyo hizo tabia hawezi kuwa nazo kabisa"
"Mwanangu!!"
"Mama hebu jaribuni kuwa waelewa na waungwana jaman!! kwanini mnapenda kishikiria imani zisizo na uhakika wowote? hebu nioneni kama mtu mzima kwa sasa na sio mtoto tena"
"Kwahiyo mwanangu umeshakuwa mtu mzima ambaye anaweza kufanya maamuzi yake mwenyewe?"
"Ndio baba"
Ukimya ukapita kwa muda eneo lile huku kila mmoja akijaribu kufikiria ya kwake, Joan alimpenda sana mchumba wake waliyekutana wakati wakiasoma wote chuoni na alihitaji ndoa pekee ili ajira itakapotangazwa wawe tayali ni mke na mme
Lakini pia alihitaji kuolewa mapema na Matinyi ili wapate cheti cha ndoa na kukiwasilisha Tamisemi ili waweze kupangwa eneo moja wakati wa ajira.
Hawakutaka kupangwa sehemu tofauti ili baadae ije kuwasumbua kwenye swala la uhamisho ambalo kwa wakati huu wa sasa limekuwa gumu kutokana na kufutwa kwa utaratibu wa mtu kumfata mme wake bali mpaka apate mtu wa kubadilishana naye.
Upande wa pili wazazi wake nao waliona ugumu kulipitisha hili jambo kutokana na taarifa mbaya ambazo wamewahi kuzipata kwa wanawake wachache ambao waliwahi kuolewa na vijana wa kabila hili.
"Naomba tukalale jamani na hili swala tuachie tukajadiliane mimi na mama yako kisha tutakupa majibu kesho" akasema baba mtu.
"Ahsante baba naomba msinikatalie tafadhali"
Wazazi hawakujibu kitu zaidi ya kuangaliana kwa muda kisha wakakusanyika na kufanya maombi kisha wakatawanyika na kila mmoja akaelekea sehemu yake ya kupatia usingizi.
Usiku huu ulikuwa mgumu kwa wazazi wa binti huyu kutokana na kupishana sana maamuzi juu ya kile binti yao anachokitaka.
"Mme wangu,mimi naona tumruhusu tu kwa sababu kataka mwenyewe jaman"
"Lakini mke wangu si unajua kabisa tabia za kabila hili jaman? hivi mwanetu akipata matatizo makubwa huko tutafanyeje?"
"Tumuombee mme wangu,unajua kubisha tunakobisha huku kunaweza kupelekea tuwe tunamtengenezea mikosi wenyewe mwanetu"
"Mimi sina cha kupinga kwasababu mama mtu na mwanae wameungana na kukubaliana ila nina ombi moja tu kwenu"
"Ombi gani hilo?"
"Naomba yule shangazi yangu wa ukoo aliyeko Rombo atumiwe nauli na kuja hapa na kisha amsimulie Joan kila kilichompata huko na baada ya hapo Joan akiwa bado na nia ya kuolewa na kabila hilo tusimkatalie tena"
"Hapo sawa mme wangu,aelezwe ukweli kisha apewe nafasi ya kuamua mwenywe"" akajibu mama mtu.
Usingizi ukawachukua na kisha kila mmoja akalala!!
Itaendelea......