sokoine akumbukwa, awa kaka wa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sokoine akumbukwa, awa kaka wa taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Apr 14, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [h=1]Waziri Mkuu Mizengo Pinda Audhuria Ibada ya Kumkumbuka Aliyekuwa Waziri Mkuu,Hayati Edward Moringe Sokoine[/h]

  Written by haki | // 0 comments

  [​IMG]
  Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhasham Telsphor Mkude akibariki sanamu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine kwenye viwanja vya Kikagango cha Kanisa hilo katika kijiji cha Wami Sokoine , Morogoro baada ya kuongoza Ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo Aprili 12,2012.
  [​IMG]
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude baada ya Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye kanisa katoliki, Kigango cha Wami Sokoine Aprili 12, 2012. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watatu kulia ni Binti wa Marehemu Soine, Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum
  [​IMG]
  Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude akiteta na Namelok Sokoine, Binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum katika ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine,Morogoro Aprili 12,2012.
  [​IMG]
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, wa zamani , Edward Lowassa katika Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12,2012. Watatu Kushoto ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
  [​IMG]
  Baadhi ya washiriki wa Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine wakishiriki katika Ibada hiyo kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
   
Loading...