Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,640
- 729,667
Nimesikia mikwara ya Kamanda Sirro na Makonda kwenye vyombo vya habari kuwa wale madalali wa soko la vipuri vya magari Kariakoo watafute kazi nyingine maana siku zao zinahesabika
Lile sio soko ni chaka la wezi wanaoiba na kuuza vifaa vya wizi vya magari.Naamini wengi wetu hapa wana ushuhuda wa kuibiwa chochote na kukipata pale na mtandao wao una mpaka watumishi wa umma ndani yake
Ule mtandao wao unahusisha kada kama nne hivi;
1. Wezi wanaokwenda kuiba
2. Madalali wanaofadhili au kununua vifaa vilivyoibiwa
3. Watu wa kati ya dalali mkuu na mteja aliyeibiwa au anayehitaji kitu fulani
4. Watumishi wa serikali wakiwemo jeshi la police kwa ajili ya kutoa ulinzi na kufanikisha wizi kwenye taasisi zao
Ukifika pale unanyenyekea utafikiri nchi haina mamlaka ya kumlinda mwananchi na mali zake.Ni mahali pa hovyo na wale watu wana jeuri na nyodo, ukileta ujuaji utakosa kitu chako na hata ukienda police hutasaidika
Ni soko chimbo kongwe la wezi lina miaka na miaka.
Sirro akifanikiwa kulitokomeza hili itakuwa faraja kubwa kwa wamiliki wengi wa vyombo vya moto...!
Lakini no vema iwepo mipango kabambe ili tatizo lisije kuhamishiwa pengine