Soko la madini kufunguliwa kahama

Soko la madini kufunguliwa kahama

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
1060098


NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amemwagiza Osa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Andrea Fabian, kuhakikisha anafungua soko la madini ya dhahabu haraka ili kuwapunguzia adha wachimbaji kusari hadi Geita kuuza dhahabu zao.

Nyongo alibainisha hayo juzi wakati wa ziara yake aliyoifanya wilayani humo kwa lengo la kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini hayo, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini. Baada ya kusikiliza kero za wachimbaji hao ikiwemo ya kukosekana kwa soko la madini wilayani Kahama, ndipo Naibu Waziri akamtaka osa madini huyo kutumia sehemu ya osi yake kama soko la madini ya dhahabu ili wauzaji na wanunuzi waweze kufanya biashara na serikali ipate mapato yake.

Uamuzi huo wa Naibu Waziri Nyongo ulipokewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa madini ya dhahabu kwa kuwa utasaidia kudhibiti utoroshaji wa madini hayo. Nyongo pia aliutaka uongozi wa osi ya osa madini huyo wa Kahama kushirikiana na mamlaka zingine za serikali ikiwemo osi ya mkuu wa wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama na mabenki wakati wa kuanzisha soko hilo.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri aliambatana na Kamishna Msaidizi-Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali, wataalamu kutoka Tume ya Madini pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama
 
Back
Top Bottom