Soko la HIMARS lazidi kupaa

Japan:-unajua moja ya sababu ya Mwalimu kuaingia vita na Amini ni kwasababu kuna Mwehu mmoja ndani ya jeshi la Amini aliingia ndani ya Ardhi ya Tanzania akanywa Gongo then akaanza fyatua risasi hovyo ndani ya Ardhi ya Tanzania na tukio hilo likachukukiwa kama uchokozi mkubwa.yaan kufyatua risasi tu ikawa ni moja ya sababu ya Tanzania kuingia vitani.
Sasa 7 Dec 1941 unprovoked Japan ikaingiza jeshi lake ndani ya Marekani na kufanya uharibifu mkubwa na watu 2,403 wakafa... Sasa kufyatua risasi tu kuliingiza Tanzania vitani, mfyataji hakuua wala kujeruhi mtu ila vita ikatokea ila kwa US unaashilia kusema haikupaswa kujibu chochote dhidi ya Japan ilhali watu 2,403 wamekufa?.
Sikubalini na jibu zito la US, ila naunga mkono kujibu kwake.
tunaishi katika dunia ambayo hupaswi kumuacha Mungu kila kitu.

AFGHANISTAN:- Baada ya Osama kuwazidi Ujanja US akakimbilia Afghanistan, Bush akawaomba Taleban kwa amani wamkabidhi Osama kama alivyo.. Taleban hawakukataa kuwa Osama hayupo ndani ya Ardhi yao bali walikataa kwa dharau tu kumkabidhi Osama kwa Bush.
Unajua Sep 11 Osama aliondoa Roho za watu wa ngapi? Unajua ni hasara kiasi gani Osama aliyoitia US?.
watu 2,753 walikufa na majeruhi ni karibia namba ya wafu.. Yaan Mtu aje kwako aue watoto wake na akimbilie ndani ya nyumba ya jirani yako then umuombe huyo jirani yako kwamba:, Khamis kaja nyumbani kwangu, kaua watoto wangu na kuvunja madirisha ya nyumba yangu then akakimbilia ndani mwako.
Then jiran yako akujibu:, ni kweli khamis yupo ndani kwangu lakini siwezi nikamkabidhi mikononi mwako.. what would you do?.

Cuba:- uko sahihi, marekani aliiwekea vikwazo tu ila hakujaribu hata kidogo kufanya kama inachofanya Urusi I wish Putin nae angalifanya kama alichofanya US dhidi ya Cuba.

Nyuklia:- US wanaweza wasiwe sahihi katika ila fikiria dunia ambayo nyuklia inapatikana kama Ugoro Sokoni.. leo Boko haramu wana miliki nyuklia.
Alshababu wanamiliki nyuklia..
ISIS na wana nyukilia...ikiwa wanamiliki Ak47 tu moto wao haushikiki ni vipi wawe na nyuklia?.
Kuwa na nyuklia si tatizo, tatizo ni, unaaminika kuwa na hayo madude?.
Unajua hatari ya hayo madude yakiingia kwenye mikono hisiyo sahihi?.
 
Hawa wajamaa kipindi kile cha ujima walipiga nagasaki na Hiroshima kwa kitu kizito kichwani je nyakati hizi zenye kuongezeka maarifa sijui itakuwaje.
Ndo anasubiriwa mrusi adondoshe nuclear kisha wenzie wamnyooshe
 
Nchi yoyote ya kiarabu au inayofungamana na vikundi vya kigaidi au vya itikadi kali, kumiliki nuclear HAIFAI KABISA.
 
Una akili sana na una uelewa mzuri tu wa mambo sema unajitoa akili kisa tu unataka kuonyesha kila afanyalo us yupo sahihi!

Japani alienda tu ghafla au ilkua vita kati yao? Jibu unalo
Ila jua tu ilikua vita ya dunia wengine wooote walikua vitani lakini hawakutumia hilo bomu yeye ni nani hadi akalitumia?
HAPA NGUVU IMESHINDA SIO HAKI

Vita ya idi amini umenipiga na kitu kizito[emoji1787]

Hivi ushawahi jiuliza kama Quba angeendelea na mpango wake us angemvamia au angetulia tu? Na kwanini aingilie uhuru wa nchi nyingine kufanya watakalo na wakati hilohilo nae hufanya? HAPA NGUVU IMESHINDA SIO HAKI

Kwanini hakushtaki UN wakadili na Afghanistan badala yake akadili nae yeye?
HAPA NGUVU IMESHINDA SIO HAKI.

Mpaka sasa hivi nchi nyingi tu zina nyuklia lkn hazijawahi kuitumia zaidi ya us maanake hata hao boko haramu wana akili kuliko yeye maana kutumia lile bomu ni ufedhuli na ugaidi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa duniani hadi sasa
HAPA NGUVU INATUMIKA SIO HAKI.


Sasa ujue haki haiwezi kuishinda nguvu hata siku moja, hata mafanikio anayoyapata ukraini anapata nguvu toka kwa us.
 
Sio kwamba nina defend Us bali nina jadili mambo yaliyo. . Hiko hivi, baada ya Russo War Urusi kupoteza vibaya dhidi ya Japan, nguvu ya Japan ikaimalika mara dufu huko Bahari ya Pacific. Japan ikajitanua zaidi,US nae akawa very concerned na kujitanua huko kila mmoja akaanza mvia mwenzie. Then baadae Japan ikaivamia China... US akapata Gap la kumdhibiti Japan, US akamkingia kifua China, akaiwekea vikwazo Japan.
Hivyo vikwazo ndivyo vilivyo muumiza Japan ikapelekea kushindwa vibaya na China.
So, hiyo ni moja ya sababu ya Japan kuivamia US.
 
Kumbe mchokozi ni us? [emoji23][emoji23][emoji23]
Kichapo kilipomzidia akatumia nyuklia.
Kumbe kutegemea kushinda vita kwa nguvu ya vikwazo sio ya kivita kaanza kitambo eeh!!

Aya futa kauli yako kua haki ina nguvu kuliko nguvu yenyewe.
 
Kumbe mchokozi ni us? [emoji23][emoji23][emoji23]
Kichapo kilipomzidia akatumia nyuklia.
Kumbe kutegemea kushinda vita kwa nguvu ya vikwazo sio ya kivita kaanza kitambo eeh!!

Aya futa kauli yako kua haki ina nguvu kuliko nguvu yenyewe.
US hakumchokoza bali aliamua kuzuia vitu vyake visiende Japan moja ya hivyo vitu ni silaha ambazo Japan alizitegemea kumpigia mchina.baada ya sanctions Japan nguvu ikakata, vita akapoteza,akabaki na kisasi.
Wakati huo US na Urusi mambo shwali.
 
Mkuu unaakili sana. Huyo jamaa asipokuelewa basi tena.
 
US hakumchokoza bali aliamua kuzuia vitu vyake visiende Japan moja ya hivyo vitu ni silaha ambazo Japan alizitegemea kumpigia mchina.baada ya sanctions Japan nguvu ikakata, vita akapoteza,akabaki na kisasi.
Wakati huo US na Urusi mambo shwali.
Hivi us hawezi shinda vita bila kuwekeana vikwazo, yaani us anapigana na mtu aliefungwa mikono afu anajiona mshindi,
Na kwanini hakumuacha mchina na mjapani wakaumana?
 
Acha utani mkuu
Polish defence minister Mariusz Blaszczak announced on May 26 that he had requested 500 HIMARS launchers plus ammunition – an enormous number which he said would involve extensive co-production.

Estonia would buy six launchers and ammunition worth $500m, the US Department of State said on July 15. Latvia made public its request for $300m in launchers and rockets a week later. And Lithuania is expected to follow suit.

https://www.google.com/amp/s/www.al...ve-nothing-equivalent-how-himars-help-ukraine
 
Hahaa poland anataka kuzifanyia nini zote hizo kama ni kupambana na mrusi 20 tu zinatosha hafurukuti[emoji23]

Nadhani washauriwe vizuri mkuu labda kama wanataka kupambana na dunia nzima.[emoji23]
Hahahaha....wameshasema wako radhi waingie kwenye madeni lakini wawe na jeshi na zana bora za kupambana na Urusi siku akijichanganya kuwavamia
 
Mkuu naomba elimu kidogo jinsi hili dude linavyofanya kazi
Kiufupi
HIMARS ni mfumo mzima wa kurusha maroketi pia Makombora.

Ina Rocket za M31 ambazo ndo Ukraine imepewa,zina range 80km.
Pia inaweza kurusha Makombora makubwa kama Army Tactical Missile (ATACMS) ambalo hili linakwenda umbali Hadi 300km likiwa na mlipuko mkubwa zaidi,hili tunaweza fananisha na kombora la Urusi linaitwa Iskander.
Na sasa wanatengeza kombora jipya "Precision Strike Missile" nalo litarushwa kupitia HIMARS,zitaanza kutumika kuanzia mwakani Range yake ni 500km.

Himars sio mfumo mpya Marekani imeutumia Sana kwenye vita ilizopigana Kama kule Iraq, Afghanistan,nk. Kinachofanya iwe deadly ni uwezo wake wa kurusha Makombora na kukimbia,wenyewe wanaita Shoot and Scoot (Unaweza Rusha Maroketi yote sita ndani ya sekunde 20 na kukimbia). Hivyo ni vigumu Kwa adui kujua mfumo upo wapi pia si rahisi kwa adui kuziharibu,ndio maana ikaitwa High Mobility Artillery Rocket launchers System (HIMARS).

Maroketi yake Yana speed Sana yanakimbia Kwa Kasi ya mara mbili zaidi ya sauti (Mach 2) hayafuati ballistic trajectory pia yana Radar cross section ndogo hivyo inakua ngumu kwa mifumo ya adui kuyatungua ndio maana unaona kule Ukraine maghala ya silaha ya Urusi na command posts zinalipuliwa na HIMARS na air defense system zinapata taabu kuyadaka haya maroketi.

Maroketi yake yanatumia GPS kufikia target. Na Kama ikatokea GPS imekua jammed pia yana uwezo wa kupiga target kupitia INS.
 

Attachments

  • IMG_20220916_102644.jpg
    301.9 KB · Views: 9
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…