Kutokana na maendeleo ya sayansi ya teknologia Tanzania,Dini zimeanza kutumia internet sawia na mashirika ya kibiashara kujitangaza. Hivi viashiria vimepelea watu kusema kwamba " dini zimekuwa biashara". Hii ndio sababu imenipelea kuchunguza hili swala kama ilivyo hapo chini.
Soko la dini, linafanana kama masoko mengine ya bidhaa. Kama ilivyo kwenye masoko mengine, kunasehemu mahalumu ambayo mnunuzi na mhuzaji wanakutana ili kubadilishana bidhaa au taarifa kwakutumia pesa au bila pesa. Kwenye soko la dini, mhuzaji ni Mchungaji na mununuzi ni Mshirika. Kuna viashiria vingi kwamba soko la dini na soko la bidhaa kufanana. Kati ya hivyo vitu ni kama ifuatavyo:-
- Ushindani,kama ilivyo kwenye masoko ya bidhaa, wahuzaji wamekuwa wakishindana kwa nguvu. Mfano wamekuwa wakitumia matangazo kupitia Television,Redio,na magazeti. Kawaida gharama za matangazo huwa ni kubwa sana kwa wauzaji wadogo. Mara nyingi wahuzaji wadogo, au wenye kipato kidogo wamekuwa wakifunikwa na kupotezwa kabisa kwenye soko na mahuzaji wakubwa. Hivyo hivyo kwenye soko la dini, Dini zenye pesa au uwezo mkubwa wa matangazo zimekuwa zikifunika dini dogo nakuzipoteza. Hapa tunaweza kuona kwenye matangazo ya mikutano ya injili, makanisa ambayo yanaweza kutumia television,redio,magazeti na internet kujitangaza, yamekuwa yakipata idadi kubwa ya washiriki kulinganisha na makanisa ambayo hayana uwezo wa kujitangaza.
- Bidhaa, kama ilivyo kwenye masoko ya kawaida, mhuzaji huwa anabadilishana bidhaa na mnunuzi kwa makubaliano Fulani. Mara nyingi kwenye masoko ya bidhaa, ili kuweza kupata faida,mhuzaji anatakiwa kuuza bidhaa ambayo inapedwa na wanunuzi. Kufanya kinyume na hapo, mhuzaji hupata hasara. Hivyo hivyo kwenye masoko ya dini, Dini zimekuwa makini sana kuchaguwa “ujumbe” wakuuza au kuhubiri kwa wateja wake(Washirika). Dini zinazo weza kuhubiri vitu watu wanapenda, zimeendelea kukuwa kwa haraka sana wakati dini nyingine zimeendelea kudumaa au kufutika kabisa. Hapa tunaweza kuangalia bidhaa ya "Miujiza" amabayo kwa sasa imekuwa ikinunuliwa kwa wingi. Makanisa ambayo yameweza au yanayo tangaza kufanya "miujiza" yamekuwa yakifurika watu,wakati wakanisa ambayo hakuna "miujiza" yamekuwa yakifa au kupotea.
Baada ya kuangalia hayo mambo mawili hapo juu,bila shaka hakuna tofauti kati ya masoko ya Dini na masoko ya biashara. Kufanikiwa kwa Dini yeyote kutatengemea na namna abavyo itazingatia kanuni za biashara. Kwa mfano,Makanisa yanatakiwa kutambuwa washindani wao na kutafuta namna au nyezo zakuweza kuwafunika. Hii ni kwasababu hali ya sasa ya makanisa ni hali ya "USHINDANI".
Nakaribisha majadiliano. Asante