SOKA: Maamuzi ya refa kusaidiwa na teknolojia ya video

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Teknolojia ya video ilitumiaka usiku wa jumanne katika pambano kati ya Spain na France. Huku goli lililofungwa na Antoine Griezmann likikataliwa kwa kuwa alikuwa ameotea, na goli la Gerard Deulofeu kukubaliwa huku wachezaji hawa wawili walionekana kana wapo katika mazingira sawa.

Deulofeu alipofunga goli lake lilikataliwa na refa msaidizi aliesema Deulofeu alikuwa ameotea, lakini baada ya refa kuwasiliana na maofisa walio kwenye television waliosema Deulofeu hakuwa ameotea goli hilo lilikubaliwa.

1.jpg

marudio ya video yakionyesha Gerard Deulofeu kuwa alikuwa hajaotea.

2.jpg

marudio ya video yakionyesha Layvin Kurzawa alikuwa amekwisha otea kabla ya kupokea mpira na kumpasia Griezmann na kufunga goli.

Watu kadhaa maarufu wa soka walitoa maoni yao, kuhusu teknolojia hii ya video. Jamie Carragher beki wa zamani wa timu ya taifa ya England na club ya Liverpool alionekana kuisifia teknolojia hiyo, kwa kuandika haya kwenye mtandao wa twitter;

3.jpg


Je, wewe mwanasoka maoni yako nini juu ya teknolojia hii ya video itaongeza au utapunguza ladha utamu wa soka?
 
Teknolojia inakua, tunapoelekea kila kitu kitakuwa kinaamliwa kwa teknolojia, hakutakuwa na haja ya marefa tena
 
Back
Top Bottom