TAKUKURU hii Rushwa Kubwa na ya aibu katika Soka la Tanzania kwa sasa hamuioni au mnaifurahia ije Kutugharimu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,363
108,403
Leo nasema (naandika) hapa wazi wazi kabisa kuwa Ligi Kuu ya Tanzania NBC Premier League imeshaharibiwa kwa Rushwa zilizovuka Viwango ambavyo GENTAMYCINE siogopi na sioni Aibu kusema kuwa zimechochewa na Utajiri wa hawa Matajiri Watatu Gharib na GSM yake, Yusuf na Azam yake na Mo na Mohammed Enterprises yake.

TAKUKURU ni kwamba Yanga, Simba na Azam Wanashinda Kuhonga kwa sasa ila kuna Timu Mbili zinafaidika na Kuhonga Kwao huko kwani pamoja na Kuhonga ila wana Timu Imara ila ipo Moja hata kkihonga bado kwa Wachezaji wake wa Kubahatisha na wa Bei Nafuu Matokeo yao huwa ni Kufungwa, Kutoka Sare na Kushinda kama leo.

Sijawataja Wizara chini ya Waziri Mchengerwa (mwana Yanga SC) na Shirikisho la Soka nchini Tanzania kupitia Rais Karia (mwana Simba SC) nikiamini kuwa hawa Wawili hawana Ubavu wa Kukemea kwani nao huwa ni sehemu za Mikakati ya Ushinci kwa hizi Timu zao Kubwa Mbili za Kariakoo.

NBC Premier League imeharibika. Kuna Timu ilipewa Penati ya Uwongo Mwanza, kuna Timu juzi ilizawadiwa Goli la Offside na kuna Timu leo Refa kwa Kuona Matokeo ni 2 kwa 2 na tayari ameshahongwa Pesa akaamua Kuchezesha Mechi kwa dakika 103 badala ya halali 93 (90 za Mchezo na 3 za Nyongeza) mpaka Mhongaji apate Goli lake la Tatu (3) na la Ushinci.

Nimeshawaambia Kazi Kwenu sasa!

Cc: Mwishokambi
 
Mkuu popoma niseme tu kuwa mm sikutazama mpira huo leo ila nilipita hapahapa jf nikamuona mwana mmoja akilalamika Kama wewe hivi. Ila baada ya kupotia comment za wadau wa soka nilijiridhisha kuwa refa alikuwa sahih aslimi zote.

Kumbe timu yako hyo ya coastal ilijipanga kuhakikisha kuwa kak Yao Simba sc anabaki nafasi ya pili kwanamna yoyote ile hvyo iliwapelekea kulalalal ovyo nakupoteza Muda ili refa amalize mpira na kuifanya Simba sc yako irejee rasm nafsi ya pili.

Sas Kama anataka Simba sc kukah kilelelni Ni vyema amaruhusu Simba imfunge na kumpatia phiri hat trick ili ampite mayele idadi ya magoli ikiwezekana apigwe nane bila Kama kawaida Yao.

Shenzi sna coastal Union shenzi sna pumbavu snaaa.
 
Mkuu popoma niseme tu kuwa mm sikutazama mpira huo leo ila nilipita hapahapa jf nikamuona mwana mmoja akilalamika Kama wee HV...

Wewe jamaa unaonyesha tabia za watanzania mlivyo ndio ile mtu umehangaika umepata ukwasi wako mmaanza ooo jamaa freemason,oo jamaa kawatoa wazazi kafara,oo jamaa mwizi.

Tanzania ukiwa maskini hakuna mwenye shida na wewe tajirika kidogo sasa utasikia kila aina ya unafiki kipindi #YANGA wanapitisha bakuli hizi kauli za kipuuzi hazikuwepo leo Yanga analia kivulini mmeanza kelele zenu.

Wewe kama unaushahidi pasipo na shaka njoo inbox kwangu nipe ushaidi kesho niamke nao na kama hakuna ushahidi i wish tuanze na wewe.

Nakuomba uje inbox utoe ushahidi wako pasipo na shaka tuanze kudili na mmoja mmoja.

La sivyo kama huna ushahidi nakuweka kwenye kundi la wambeya tu wa vijiweni

Karibu inbox
 
Hakuna cha rushwa wala hongo. Angalia coastal union walivyokuwa wanapoteza muda.

Tena ilibidi refa aongeze ata 15mins, kitu kilichofanya nibakie kuwa mshangiliaji wa vpl mpaka hivi sasa NBC pl ni kitendo cha timu ndogo kupata goal mapema na kuanza kujidondosha.

Jamani mashabiki ndiyo mpira, na lengo la mshabiki yeyote ni kuona timu yake inacheza uwanjani na kupata matokeo.

Sasa timu inatangulia kupata goli wachezaji wanajiangusha, wanachomoa goal kipa anajidondosha, substitution wachezaji wanagoma kutoka uwanjani.

Sasa huo ni mpira kweli?

Hebu tubadilike, kongole referee na mareferee wengine wote wakuige.

Ref: 2022 World cup Qatar
 
Acha tuendelee na ligi ya namna hii.. ila wakigusa klabu bingwa aibu
 
Back
Top Bottom