Soka la tanzania limeingiliwa na mafisadi papa

HPAUL

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
410
567
Watanzania wengi, Wakiwamo wapenzi wa Simba wote wanajua ya kwamba Yusuf Manji ni fisadi namba moja nchini kwa sasa hivi. Kila mzalendo wa nchi hii anajua jinsi Yusuf Manji anavyohusika katika masuala EPA, mikataba ya kifisadi na NSSF nk. Itakumbukwa Manji alivyopata na mshtuko wakati alipokaribia kushtakiwa kwa kosa la ufisadi – KAGODA – EPA hata ikabidi akambizwekatika hospitali ya nje ya kutibiwa. Ilibidi Kikwete mwenyeweamuokoe Manji asishtakiwe. Sio siri ni Manji aliyerejesha sehemu kubwa ya fedha zilizoibwa benki kuu kupitia Kagoda huku akishirikina kwa karibu na fisadi mwenzake Rostam aziz.
Kitendo cha Manji ambaye aliletwa Yanga na Kikwete kwa kushirikiana na Ridhiwani kuuhujumu mchezo wa kandanda na hususani klabu ya Simba si cha kimichezo hata kidogo. Wakati samba imekamilisha usajili wa Twite (APR) na Ngassa (Azam) wao kwa kutumia pesa haramu wanazozipata kwa kuwaibia Watanzania wakiwamo wapenzi wa Simba wamewashawishi tena wachezaji na kujaribu kuwasajili kinyume cha utaratibu. Wamefanikiwa kwa Twite lakini wamekwama kwa Ngassa kwani viongozi wa Azam wanamsimamo.
Watanzania wanaelewa fika kuwa pesa hiyo chafu vilevile imepenyezwa TFF ili zoezi la usajili lisogezwe mbele kuwapa mwanya mafisadi kuhujumu soka la Tanzania na hasa klabu ya Simba. Hakunasiri kwa viongozi wakuu wa TFF ni Yanga damu (Tenga, Angetile na Kawemba), Ni ukweli usiopingika kuwa sio rahisi kupata viongozi wa kandanda ambao sio Simba au Yanga, lakini ubaya ni pale viongozi wa soka wanapotumia wanapotumia unazi wao wa Yanga kwa kutumiwa na mafisadi papa kuihujumu Simba. Tutaendelea kusikia maamuzi ya ajabu ajabu katika kipindi cha wiki mbili zijazo kutoka kwa viongozi hao wa TFF wanaotumiwa na mafisadi papa.
Wanachama na wapenzi wa Simba hawatakaa kimya na kuona pesa haramu za mafisadi zinatumika kuihujumu klabu yao, ni lazima watachukua hatua kali siku chache zijazo.
 
Mafisadi Papa tushawazoea tunawataka mafisadi Nyangumi..

Na Mbona Huu ufisadi upo siku nyingi sana hata yanga enzi za kina Mpondela walikuwa wanamaliza account ya klabu bila hata noti Timu utasikia Imezuiliwa Hotelini dah ilikuwa ni aibu tupu...

Rage huyu huyu ameshafungwa kwa Kuiba na kufoji Risiti FAT Ndolanga akaponea tundu la sindano

Kati ya Pondamali au Mambosasa mmoja alishawahi Iba Godolo la Klabu alipokuwa Mlinzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom