Soka la bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soka la bongo

Discussion in 'Sports' started by assa von micky, Mar 28, 2011.

 1. assa von micky

  assa von micky Senior Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wana JF naomba nitoe changamoto zangu katika mustakabali mzima wa soka la Tanzania.Soka la Tanzania ni la maneno na siasa nyingi ,hakuna mipango thabiti ya kutukwamua hapa tulipo ,nikionacho mimi ni viongozi wa soka ambao wanatafuta umaarufu kataka kuelekea kwenye safari ya siasa, Siasa ya nchi hii inalipa siasa katika nchi hii ni kikwazo cha maendeleo, sasa siasa imeingia katika soka leo hii kiongozi asiyejua chochote kuhusu soka ndiye kiongozi wa soka ,wanadinga wengi wa zamani Ukiondoa akina Tenga wamechoka kiuchumi,hawana uwezo wa kupigana vikumbo na wenye pesa katika kuongoza soka.
  Benchi la ufundi la timu zetu nyingi kuanzia timu ya Taifa limejaa ubabaishaji tu ,benchi la ufundi linamafundi wasiokuwa na taaluma ya mchezo husika, nyuma ya mafanikio ya kocha yoyote duniani kuna mlolongo wa watu ambao wanataaluma mbalimbali za mchezo wa soka.Tukubali wanachokifanya Azam leo hawa ni wawekezaji halisi wa soka wamejenga viwanja,wanatengeneza timu za vijana, uwekezaji katika soka sio kuinunua moro united au kuinunua African lyon ili upate sifa kisha baadae unaitelekeza,uwekezaji mzuri ni kujenga miundo mbinu mizuri kama viwanja bora ,timu za chini ya umri wa miaka 14,17,20,23.Tukifika hapo tutakuwa na akina Essien wetu wengi ambao wataleta sifa kwa taifa.
   
Loading...