Soka la bongo: Wapi tumejikwaa?

Soka la bongo: Wapi tumejikwaa?

yutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
1,779
Reaction score
1,227
Wachezaji wetu wanajituma na kujitahidi sana toka enzi nonda, lunya,machepe, machupa, kali ongala ,kaniki, nsajigwa n.k. lakini wameshindwa kupenya kwenye level ya kimataifa xana xana wameishia kucheza araqbuni ambako ni kama dampo la walioshindwa hata wakienda ulaya na kwingineko basi uishia ligi drj la 4. asa"fari samata yuko jirani lakini mafanikio yake yanaonekana kwa club kubwa na kongwe balani africa. tatizo nini hasa? hakuna vipaji, kuridhika kuchezea simba na yanga, miundombinu, (academy sports) wazawa wamekosa uzalendo, kubaniana(ndumba), uongozi wa kifisad, tff na weak policies, au...emh funguka swahiba 2014 tujue wapi tunakosea, tujirekebishe vip .....
 

Attachments

  • as.jpg
    as.jpg
    7 KB · Views: 62
  • swa.jpg
    swa.jpg
    12.8 KB · Views: 56
Kwanza Lunyamila ameisha pona maana nilisikia na kuona kwamba anaumwa na alikuwa amelazwa Mwananyamala Hospitali....badae nitajikita kwenye mada
 
Kwanza Lunyamila ameisha pona maana nilisikia na kuona kwamba anaumwa na alikuwa amelazwa Mwananyamala Hospitali....badae nitajikita kwenye mada

Najua unapita ila karibu
 
Kwanza wachezaji wetu wajitambue na wajue hii ni ajila kama ilivyo kazi nyingine pili waachane na michezo ya mtaani maarufu kama NDONDO Unakuta mchezaji yuko ligi kuu anaenda kucheza kombe la Diwani au Mbunge tena kinachoshidaniwa hapo ni Mbuzi au kuku Jogoo.
 
sababu wachezaji hawajitumi kabisa, wakisha pata ustar ndio usiseme wanatembea barabarani utafikiri wana majipu.mchezaji akisha chezea yanga au simba ndio anaona mwisho wa soka. afikiri kama kuna mafanikio mengine.
 
Kwanza Lunyamila ameisha pona maana nilisikia na kuona kwamba anaumwa na alikuwa amelazwa Mwananyamala Hospitali....badae nitajikita kwenye mada
Nilikutana naye kama wiki mbili zilizopita alisema anajisikia vizuri baada ya hapo sijaonana naye tena.
 
Kwanza wachezaji wetu wajitambue na wajue hii ni ajila kama ilivyo kazi nyingine pili waachane na michezo ya mtaani maarufu kama NDONDO Unakuta mchezaji yuko ligi kuu anaenda kucheza kombe la Diwani au Mbunge tena kinachoshidaniwa hapo ni Mbuzi au kuku Jogoo.
kwenda kucheza kwenye ndondo si kama wanapenda wakati mwingine ni njia ya kutafuta na kujiongezea kipato NAPITA
 
Last edited by a moderator:
sababu wachezaji hawajitumi kabisa, wakisha pata ustar ndio usiseme wanatembea barabarani utafikiri wana majipu.mchezaji akisha chezea yanga au simba ndio anaona mwisho wa soka. afikiri kama kuna mafanikio mengine.
YAP naamini ilo nalo linachangia kwa kiasi fulani kwani anaona akichezea yanga au simba basi amemaliza
 
Michezo haionekani kama ni ajira,matokeo yake wengi wanaofanikiwa katika michezo wanakuwa hawana Elimu,kwahiyo ni ngumu mbumbumbu kupambanua nafasi yake,
Nina mfano wa mchezaji mmoja mkubwa alikwenda majaribio Ujerumani kilichomwangusha alikosa nguvu za kucheza mpira wa kijerumani,lakini agent akamtafutia timu Venezuela ili apate uzoefu wakati anajenga mwili.Mimi wakati huo nilikuwa nafanya kazi na kiongozi mmoja wa YANGA,mchezaji akarudi ili kusubiri msimu wa Venezuela uanze ,kukawa na mechi ya SIMBA v YANGA akalaghaiwa abaki acheze hiyo mechi ndio arudi,mapaka mechi imechezwa na agent amekata tamaa ya mchezaji....Hapo ndio utaona UJINGA unavyogharimu wachezaji wetu.
 
Nimekuwa nikiwasikiliza wadau wengi wakiwalaumu wachezaji wetu kwa kishindwa kucheza Ulaya. Wanaoongoza kwa lawama hizi ni waandishi wa habari. Lakini wachezaji ni kundi dogo sana (ingawa lililo muhimu sana) la wadau wote wa mpira duniani. Ili nchi ifanikiwe, ni lazima viungo vyote vya mnyororo huu viwe madhubuti na vilivyolainika: viongozi, waamuzi, waandishi, wapenzi, washabiki, madaktari, waalimu, wadhamini mawakala, n.k. Kabla hatujajiuliza ni wachezaji wangapi wameshaenda kucheza soka ya kulipwa kwenye Ligi zilizokomaa, tunapaswa kujiuliza ni wangapi kati ya wadau waliobakia nao wameshapata ajira kwenye mataifa hayo? Talib Hilal aliyeko Oman? Huko nako wachezaji kadhaa walikwishacheza. Jamhuri Kihwelu alipokwenda Yemen? Abdi Kassim yuko mbele zaidi ya hapo. Mawakala wanaosemekana wako ughaibuni? Kwa rekodi zao, ni madaraja ya akina Henry Joseph aliyeamua kurejea nyumbani baada ya kubangaoza hukohuko. Charles Hilary, Mwamoyo Hamza na wengineo? Wako huko wakiwa watangazaji wa jumla, mahsusi kwa idhaa za Kiswahili, sio wachambuzi wa kimataifa wa soka. TBL na udhamini aw Barcelona? Labda. Na ndio angalau wanaoisukuma hiyo Taifa Stars yetu. Sasa kama visima vyenyewe vimekauka, utategemeyaje maji mtungini?
 
nchi kama nchi hatuna mfumo endelevu wa kukuza na kuiniu vipaji katika nyanja mbalimbali za kimichezo,hii tumerithi toka kwa mwalim akiwa kiongozi mkuu wa nchi si katika soka tuu au michezo mingine wewe tazama hili swala zaidi katika hii wizara tunayoita ya utamaduni na michezo,kila muhusikia katika hii wizara hajanufaika ipasavyo leo hii tunazungumzia wachezaji kushindwa kushine kwenye majukwaa ya kimataifa kama wakina Maliga,oriech,Nonda n.k lakini hata ukija kwenye muziki wetu hakuna jipya unaloweza kulipeleka mbele ya jukwaa la kimataifa likaonyesha utofauti

Swala hapa nikutokuwa na sera endelevu toka serikalini katika nyanja nzima ya utamaduni na michezo ikiiacha hii sector kama ziada katika maisha ya watanzania wakati ndio eneo linalo onekana kama ajira ya vijana wengi waliokosa nafasi katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.Ikiwa tutapata sera madhubuti na yenye usimamizi kuanzia ngazi ya kata mpaka taifa naamini leo hii tungecheza World cup kwa mara ya kwanza kama hamasa aliyo kuja nayo Jakaya ingekwenda sambamba na sera madhubuti na usimamizi wa vyama na hizi taasisi zote za michezo..kukiwa na sera ya taifa ya michezo yenye usimamizi hivi vyama vyote vitakuwa vikifata na kufanya kazi kulingana na misingi iliopo si kama leo mambo tunavyo jiendeshea hovyo,watu wanaingia kwenye madaraka kuiba na kutafuta popularity kesho wawe wanasiasa

swala si wachezaji kujitambua swala ni kutokuwa sera muafaka ya michezo na utamaduni,kutokuwa na viongozi wawajibikaji na wenyenia ya kuinua michezo katika vyama na taasisi za michezo
 
Back
Top Bottom