Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla ni kituko linapokuja suala la umri. Wachezaji wengi wamekuwa wakiongopea sana kuhusu umri wao halisi.
Wapo wachejazi wakubwa na wanaoheshimika ambao walishakumbwa na skendo ya udanganyifu wa umri.
Lengo la uzi huu sio kuwazungumzia hao bali huyu mchezaji wa Kagera Sugar ambaye namjua nje ndani.
Anajulikana kama Erick Kyaruzi, ni mchezaji mzuri ndio ila kadanganya umri mpaka inakera. Kwa tunaomjua hili halitupi tabu sana, lakini kwanini huu udanganyifu? Kwa manufaa ya nini hasa?, Ili iweje labda?
Huyu nimekuwa nae mtaani, nimesoma nae shule moja ya msingi nikiwa namtangulia darasa moja. Nimemaliza darasa la saba 2002, yeye 2003. Kutoka 2003 - 2017 ni miaka 14.
Nina miaka 29 kwa sasa, ina maana huyo labda ilitakiwa awe na miaka kuanzia 26-29, ajabu kadanganya ana 19. Karudisha nyuma miaka kuanzia 7-9. Sio jambo zuri kwa ustawi wa soka letu.
Tujirekebishe, Jamal Malinzi hapa una la kuongea.