Social Networks: A Useful Place to Gather Intelligence Information | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Social Networks: A Useful Place to Gather Intelligence Information

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Sooth, May 1, 2011.

 1. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  NOTE: This post is intended for novice users. Experts are welcome to contribute.

  Social Networks kama facebook ,tweeter, JF, n.k zimejenga uhuru mkubwa wa kujieleza. Bahati mbaya kuna wengine wanautumia vibaya uhuru huo kwa uhalifu na kutusi watumiaji wengine. Serikali nyingi duniani zimegundua kwamba ktk media kama hizi kuna wahalifu wengi sana na nyingi zinatumia kwa ajili ya kukusanya taarifa za kiintelijensia. Tumia uhuru huu kwa makini, usijione kama umejificha sana kiasi cha kutokamatwa. Unaweza kupatikana kama ifuatavyo:


  1.Unaweza kutambulika kwa kutumia email address. Mfano upo JF na unatumia username fulani ambayo haihusiani na jina lako, lakini email address inatoa hint ya jina lako na hata ukiwasiliana na mtu jina kamili linajitokeza. Wanapata wapi email address yako, jina lako na anwani zako? Kampuni zinazoendesha huduma kama hizi hutumia leseni ambayo moja ya masharti ni kutoa (kwa serikali) taarifa za mtu/watu ambao wametenda uhalifu kupitia mtandao huo.


  Hata ktk nchi ambazo hakuna haja ya leseni, bado dola inaweza ikashurutisha zitoe tarifa za wahusika. Wakati wa maandamano huko Misri, ISPs waliamuriwa ku-disconnet network ili kuzuia watu wasiji-mobilize kupitia facebook. Umeshaiona hii: “JAMIIFORUMS reserves the right to reveal any information we have about you in the event of a complaint and legal action arising from any message that you may post. Please also note that all IP addresses are recorded when items are posted.”?

  Pia Social networks zina uhusiano wa karibu na intelligence services-mfano facebook waliwahi kupata fedha kutoka In-Q-Tel, ambao wana uhusiano na CIA (CIA’s venture capital firm): Source http://righttruth.typepad.com na Exclusive: U.S. Spies Buy Stake in Firm That Monitors Blogs, Tweets | Danger Room | Wired.com.


  Kuna security breaches pia na zimetokea mara kadhaa facebook ambapo personal info zinaonyeshwa wazi kwa kila mtu (hata wale ambao hawako facebook) bila kutarajiwa kwa sababu ya bug. Usijeshangaa siku moja JF inatoa full info unapotoa comments zako. Pia kuna undercover agents ambao ni watumiaji wa kawaida wa social networks.  2. Kama ulichakachua kuanzia email address (hata secondary email address), mpaka majina na address zingine, wanaweza kuku-track kwakutumia IP address ya kompyuta yako maana unavyopost, kuna mawasiliano kati ya kompyuta yako na server za JF, facebook au tweeter. Inakuwa rahisi kupatikana kama unatumia modem ya moja ya kampuni zetu za simu (e.g. voda,tgo etc), watahusianisha muda uliopost na ip address iliyotumika na baadaye namba ya modem (simcard line) yako (so watajua jina kamili, tarehe ya kuzaliwa,n.k, kama umesajili line).


  Kumbuka simcard yako inatumia mnara ulio karibu na ulipo, na hizo taarifa zinahifadhiwa kwenye database. Kama hujasajili line unayotumia kwenye modem, bado wanaweza wakakupata kama utajisahau na kutumia line hiyo hiyo kuwasiliana na watu wengine, hasa waliosajili na wanaokufahamu.


  Kama unapost kutoka internet cafe, inakuwa ngumu kidogo. Lakini kama unaenda sehemu ile ile, mida ile ile na kufungua websites zilezile, bado unaweza ukapatikana, hasa kama wakishirikiana na mhudumu wa Cafe na ISP. Kuna hacker aliyewahi kukamatwa internet cafe baada ya ku-hack systems za FBI (mayb he was an amateur).


  3. Kama umechakachua identity yako vizuri, wakiku-profile vizuri, bado wanaweza kukupata kupitia rafiki zako mtandaoni, mfano facebook unakuwa na friends ambao wanakufahamu kiuhalisia hata kama umechakachua jina. Kuna dogo wa Moshi alikamatwa miezi kadhaa iliyopita kwa kukashfu mheshimiwa kupitia facebook, pamoja na kuwa na aliases (majina tofauti) 7 tofauti za facebook. Kulingana na namna unavyotumia intaneti, uchunguzi mpaka wakupate unaweza kuchukua days, miezi hata miaka.


  Kiujumla sio rahisi hasa kwa case ya 2 na 3 kwakuwa social networks zina maelfu ya watu wanaozitumia kwa siku, hivyo uchambuzi wa data nyingi kiasi hicho unahitaji muda mrefu sana ambao intelligence services nyingi hawawezi kumudu. Kama unatumia net ya kwenye simu, inakuwa rahisi maana hata kama hujasajili line, kuna watu unaowasiliana nao ambao wamesajili na wanakufahamu. Kumbuka ukishakamatwa na kompyuta yako, wanaweza kuona webpage ulizotembelea na comments zako maana zinahifadhiwa kwa muda ktk HDD.


  Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya jamii e.g. JF na tweeter (you don’t abuse, you just want to enjoy your constitutional right-freedom of expression) unaweza ukatumia njia zifuatazo kwa tahadhari:

  1. Change your identity completely- email addresses, names, addresses. Be anonymous even to your friends. Choose ur words carefully-usitumie maneno ambayo itakuwa rahisi kwa mtu kufikiria huyu atakuwa fulani...

  2. Kama unatumia internet cafe, usiende ile ile kila siku, muda ule ule, wala kompyuta ile ile kila siku. Mhudumu wa net asijue websites unazotembelea. Clear the bookmarks, when necessary.

  3. Kama unatumia net ya ofisini au modem za private cell companies, tumia proxy servers (Public Proxy Servers). Yaani badala ya kuwasiliana na Social Media servers directly, do it through another server. Unaweza hata uka-nest hizo proxy servers. This way,inakuwa ngumu (but possible-kuna software za kutrack IP address) kwao ku-trace source. Pia kuna IP address spoofing kwa wataalam zaidi.  proxy.jpg


  Kiujumla, tuwe responsible,tutumie identity zetu halisi, tusifanye vitu kwakuwa tu tumejificha nyuma ya screen. Karibuni kwa maboresho ya mawazo haya.....
   
 2. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ]
  Umesahau ni kuandika kuwa unataiwa kuwa mkweli katika coments au thread zako na itu unachoweza kuthibitisha. Ili ikitoea siku ya siku ukahitajika kuthibitisha ........Sio kupika pika mambo kuwafurahisha waislam au wakristu au CHADEMA au CCM au CUF
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  i have got nothing to hide coz i dont violate...just commenting what i feel but not abusing!
   
Loading...