JF iko poa, na since ni ya home inakuwa bab'kubwa zaidi. Shida ni moja kubwa, huna control ya kuchagua una-interact na watu wa aina ipi kama ilivyo kwenye hiyo mitandao mingine uliyoitaja. Kwingine una uhuru wa kuchagua nani aone unachosema, na ni nani uone anachosema. Humu unaweza sema ABC, kuna great thinker ataelewa XYZ, halafu since wengi hawajui kutengeneza hoja, wanakujengea chuki na kuku-attack.
Binafsi nitakuwa Twitter, IG, n.k. miaka yote. Siwezi kusema nitaendelea kuwa JF mwakani muda kama huu. Kadiri umri unavyosogea, energy pia ya kukomaa na vibes za hii mitaa inapungua. Unless, kutakuwa na mabadiliko.