SNP outlines plans for referendum:Tanganyika na Zanzibar zinahitaji fursa kama hii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SNP outlines plans for referendum:Tanganyika na Zanzibar zinahitaji fursa kama hii.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babylon, Sep 3, 2009.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Scottish First Minister Alex Salmond has announced an independence referendum bill as the centrepiece of the SNP's plans for the coming year. The Scottish Government wants to stage the independence referendum in 2010.
  However, the minority administration's plan faces being rejected because of a lack of parliamentary support.
  Mr Salmond revealed details of a total of 13 bills, including minimum alcohol pricing, marking the start of the SNP's third legislative session.
  The first minister told MSPs there was a "consensus for change" on Scotland's constitutional status.
  He said: "I want Scotland to have the same responsibilities and opportunities as similar nations.
  "Until we can use all the economic and financial levers available to every other government in the world, Scotland will always be at a competitive disadvantage."
  Mr Salmond said he had been "very proud" to lead the Scottish Government but warned a "glass ceiling" threatened to stall the country's progress.
  "This government was elected with a popular mandate to put the question of Scotland's future to the vote in a referendum," he said.
  "It is time for the people of Scotland to have their say. Not everyone will agree with our vision for the future, we know that.
  "But the people of Scotland must be heard. This parliament should not stand in their way - let the people speak."
  The Scottish Government has said it could be a multi-option referendum - and this could include the tax changes proposed by the Calman Commission on devolution.
  Scottish Labour leader Iain Gray said the SNP's priorities should be the economy and crime.
  Mr Gray said: "This year's flagship, the referendum bill, was preannounced last year. It starts with even less support than the late unlamented council tax bill of last year.
  "With its rigged question to suit the SNP, its rigged timetable to suit the SNP and its misplaced prioritisation to suit the SNP, it is a flagship begging to be scuttled."
  Scottish Tory leader Annabel Goldie said Mr Salmond had chosen "posturing" over confronting the challenges facing Scotland.
  She said he was a "lone voice representing a minority view".
  Alcohol problem
  Scottish Liberal Democrat leader Tavish Scott said he would support the government when it concentrated on people's jobs and on the recession.
  He said: "We will not support the government when the SNP's internal party politics are more important than the country.
  "The referendum is about the SNP. The recession and jobs is about Scotland. We will put Scotland before the SNP."
  Other bills put before the parliament include a minimum pricing strategy aimed at stopping high-strength alcohol being sold for "pocket money prices", without affecting premium products like Scotch whisky.
  That plan has run into opposition, but ministers said tough action must be taken to cut the cost of Scotland's alcohol problem, which they estimate costs the country £2.25bn per year.
  There will also be a bill for a replacement of the Forth crossing, building a new bridge to the west of the current road crossing.
  A housing bill would end the right-to-buy for all new-supply social housing and there will be a bill to give patients greater rights on waiting times in the NHS
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Fursa hiyo haipo mbali sana ,maana kila kukicha kuna mambo hayaeleweki na unapoyaulizia unaambiwa ni mhaini,ela yana mwisho.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Watabania wataacha tu, ona hapa Jaji Warioba alivyokuwa anabana.

  Jaji Warioba: Kura za Maoni Zanzibar ni hadaa

  Mwandishi Wetu Mei 7, 2008


  SWALI: Wewe ni kati ya waliopinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kutaka suala la Muafaka wa Zanzibar lipigiwe kura ya maoni. Baada ya CCM wenyewe kujieleza kwa kina, na pamoja na kwamba Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitakwenda tena mezani, bado unaona kuwa si sahihi kuwa na kura ya maoni?

  JAJI WARIOBA: Hili si swali ambalo unaweza kulijibu kwa kifupi. Naamini linahitaji maelezo marefu kidogo. Tumekuwa na historia ya kuwa na Muafaka tangu turudishe taratibu za siasa za vyama vingi.

  Mwaka 1999 tulikuwa na Muafaka ambao ulishindikana kutekelezwa, na baada ya uchaguzi wa mwaka 2000, baada ya matatizo kujitokeza, vyama hivi viwili CCM na CUF, vilikutana na mwaka 2001 tukawa na Muafaka wa pili.

  Sehemu kubwa ya Muafaka huo ilitekelezwa ingawa yalibaki mambo kadhaa ambayo yameshughulikiwa katika Muafaka huu wa sasa. Wakati Kamati inafanya kazi, wananchi kwa ujumla, ukiacha wanachama wa CCM na CUF, walikuwa na matumaini makubwa sana, na wakakaa kwa utulivu wakitumaini kwamba safari hii Kamati hii itakuja na mapendekezo ambayo yatatuwezesha kuepuka vurugu ambazo zilitokea huko nyuma.

  Kwa hiyo ilipoanza kujitokeza ama kusikika kwamba wamefikia makubaliano matumaini ya wananchi yaliongezeka. Kwamba sasa kabla ya uchaguzi ujao tutakuwa tumepata utaratibu ambao utatuepusha na vurugu ambazo zilitokea huko nyuma.

  Nimeusoma Muafaka kwenye magazeti. Naamini hayo ndiyo makubaliano waliyofikia. Nadhani makubaliano yale ni mazuri, na kama yakitekelezwa, ingawa kuna sehemu ambazo zinatia wasiwasi, kwa ujumla yakitekelezwa tunaweza kuwa na matumanini ya kumaliza suala la mpasuko Zanzibar.

  Muafaka ule una sehemu nne kuu. Ya kwanza ni makubaliano waliyofikia, kwamba yale ambayo hayakutekelezwa, yaliyokuwa katika Muafaka wa pili, yatekelezwe. Sehemu ya pili ambayo mimi naiona kuwa muhimu sana ni inayozungumzia kuimarisha mazingira ya uchaguzi.

  Kati ya mambo makubwa yanayozungumziwa katika sehemu hiyo ni kuimarisha mazingira ya uchaguzi. Hayo ni kuimarisha Tume ya Uchaguzi, kwa maana ya kuipa uhuru wa kifedha. Kwamba wawe na uhakika wametengewa fedha, wawe na uhakika nazo ili wasiwe kila mara wanaomba fedha kutoka Hazina, na pia kuimarisha Tume kwa maana ya utendaji na mambo mengine.

  Ni sehemu hiyo pia ambayo inashughulikia daftari la wapiga kura. Kwamba liimarishwe, lisafishwe ili kuepuka matatizo wakati wa kupiga kura hasa kuhusiana na nani ana haki ya kupiga kura na nani hana. Kwa ujumla sehemu hiyo ambayo ni muhimu sana, kama ikitekelezwa itasaidia sana kwa sababu matatizo ya Zanzibar yametokana na uchaguzi.

  Matatizo hayo yalianza kabla ya Zanzibar kupata Uhuru. Kabla ya Mapinduzi kulikuwa na matatizo yanatokea kila uchaguzi ulipokuwa ukifanyika, hata wakati wa serikali ya kikoloni. Na baada ya kurudisha mfumo wa vyama vingi, uchaguzi wa mwaka 1995 ulikuwa na matatizo, wa 2000 ulikuwa na matatizo hata tukapoteza maisha ya Watanzania wenzetu na wengine wakakimbilia nje. Ingawa hali ilionekana nzuri kidogo kuliko huko nyuma baada ya uchaguzi wa mwaka 2005, matatizo hayo ndiyo yaliyotufikisha hapa.

  Matatizo haya ya kisiasa yameigawa sana Zanzibar. Kuna wakati nilisema Zanzibar kuna ukabila. Kwamba siasa imeleta kitu aina ya ukabila Zanzibar. Pamoja na sera za vyama, tofauti kubwa Zanzibar ni kati ya Pemba na Unguja. Inawezekana ukakuta watu wa vyama vingi Pemba, lakini ukifika kwenye uchaguzi, hasa uchaguzi wa rais, wanaona rais wanayeweza kumkubali awe anatoka Pemba.

  Watu wa Unguja nao wanaona rais wanayeweza kumkubali lazima awe anatoka Unguja. Kumekuwa na mapambano hayo, tofauti kati ya Pemba na Unguja ni kubwa kuliko kati ya CCM na CUF. Sasa limekuwa ni suala la kijamii, si la kisiasa tu. Kuna watu wanaamini kwamba utawala uwe Unguja na kuna watu Pemba wanaamini kwamba wanaonewa, kwamba kiongozi hawezi kutoka Pemba. Hili ndilo linaloleta tofauti kubwa katika mpasuko huu.

  Lakini haya yote yanatokana na jinsi uchaguzi ulivyokuwa ukienda, kwa hiyo tukiimarisha tafsiri za uchaguzi, ikawa wazi kabisa kwamba uchaguzi ukifanywa unakuwa huru na haki, inaweza kupunguza mpasuko huu kwani watu wataona uchaguzi umefanywa vizuri, aliyeshinda ana haki ya kuongoza.

  Sehemu ya tatu ya Muafaka ndiyo hiyo inayozungumzia mfumo wa serikali; kwamba iwe na rais na makamu wawili na kwamba chama chochote kitakachopata asilimia tano kiwe na haki ya kuingia katika serikali.

  Sasa hapa mimi nina wasiwasi. Kuwa na rais na makamu wawili inawezekana ikawa na matatizo. Mtu akiwa na cheo cha juu anataka awe na madaraka ya kutosha ya kuweza kutenda kazi zake.

  Akiwa na cheo tu kama kazi hazitoshi ataanza kuingia katika majungu na umbeya na kuingilia utendaji na hiyo itafanya uendeshaji wa serikali kuwa mgumu. Atakosa kazi ya kufanya. Ingewezekana kabisa kuwa na mfumo huu uliopo, ukawa na rais na ukawa na kiongozi wa shughuli za serikali. Inatosha hiyo kuliko kuwa na makamu wawili.

  Zaidi ya hapo pia utaona katika mfumo ule huyu makamu wa kwanza ndiye hasa ambaye hatakuwa na madaraka. Kwa sababu makamu wa pili ukisoma ni kama ni waziri kiongozi. Kwa hiyo hapa una mtu katikati hapa, baada ya rais yupo, lakini hana madaraka ya kutosha, hiyo inaweza kuleta matatizo katika utendaji.

  Jingine ni hili kwamba kila chama ambacho kinapata zaidi ya asilimia tano kiwe kwenye serikali. Ningeelewa kama tungekuwa na kura hii ya uwiano kama tungekuwa tunazungumzia uwakilishi. Lakini kuzungumzia serikali ya uwiano bila kuwa na uchaguzi wa uwiano kuhusu baraza la wawakilishi inaweza kuleta matatizo.

  Kwa sababu inawezekana kabisa ukachagua baraza la wawakilishi, ukapata wawakilishi kufuatana na kura zilizopigwa. Kisha ukijumlisha kura za kila chama ukakuta kuna vyama ambavyo vimepata asilimia tano lakini havikupata hata mwakilishi mmoja.

  Sasa unampataje huyu anayeingia serikalini kama hakuingia katika baraza la wawakilishi? Hii mimi inaniletea matatizo kidogo, nilifikiri kama tunataka uwakilishi wa uwiano tungeanza na baraza la wawakilishi. Sioni umuhimu sana wa kuwa na serikali inayotokana na uwiano.

  Serikali hiyo ingekuwa inatokana na baraza la wawakilishi. Mnachagua baraza la wawakilishi, kisha kwa hali ilivyo, mnasema kwa wakati huu, kwa matatizo tuliyonayo, ngoja tuunde serikali ya pamoja.

  Mnaunda, na nia hasa kwa Zanzibar, ni kuunganisha nchi, uunganishe Pemba na Unguja. Kwa sababu hivi tulivyo kuna mgawanyiko, kwa mfano, Serikali ya Zanzibar, ama tuseme katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Pemba inawakilishwa na chama kimoja na Unguja nayo inawakilishwa na chama kimoja. Kwa hiyo una serikali, lakini waliomo, hasa waliochaguliwa, wanatoka kisiwa kimoja. Rais hawezi kupata mwakilishi wa CCM kutoka Pemba akamwingiza katika Serikali.

  Ukiwa na serikali ambayo inaonekana inatoka sehemu moja, wasiwasi wa sehemu ile ambayo haiko katika serikali ndio unaochochea mpasuko kuendelea. Katika hali hiyo ndiyo mnaweza kuona kwamba muunde serikali ya pamoja. Mnakuwa wote pamoja bila ya tofauti ya vyama, na wananchi kwa ujumla wataona ni serikali yao.

  Kwa hiyo unaweza kuwa na mawaziri kutoka CCM na mawaziri kutoka CUF, Waunguja watajiona wako katika serikali na Wapemba watajiona kuwa wako katika serikali. Sasa ni ngumu sana kwa watu wa kawaida, kwa mfano Pemba, kuona kwamba wanayo serikali.

  SWALI: Kwa hiyo kwa sasa Pemba wanajiona kuwa hawana mwakilishi serikalini?

  JAJI WARIOBA: Pemba kwa sasa hawana mwakilishi serikalini. Nilifikiri hili lingekuwa muhimu kabisa kwa sasa. Linawezekana kwa wakati huu, ikija kufika mahali wanafanya uchaguzi na unakuta vyama vyote hivyo vikubwa vinashinda pande zote mbili. Ukifika wakati huo mnaamua kwamba kwa matokeo haya hakuna haja ya kuwa na serikali ya pamoja.

  Kwamba labda CCM imeshinda, ina wawakilishi kutoka Unguja na Pemba, inaunda serikali ya nchi nzima, kunakuwa hakuna wasiwasi. Ama CUF imeshinda na wawakilishi Unguja na Pemba kunakuwa hakuna wasiwasi.

  Nadhani haja ya sasa ni kuwa na serikali ambayo inawakilisha Zanzibar nzima. Tunaweza kufika hapo kwa kutumia Baraza la Wawakilishi. Na hata huko baadaye ikawa hivyohivyo, hakuna haja ya kuunda serikali ya uwiano. Unailazimisha sasa, lakini unaweza kufika mahali ukaona haina haja ya kuwa nayo.

  Kama chama kimepata asilimia tano, yaani umekusanya kura zote zilizopigwa Pemba na Unguja kimepata asilimia tano, hiyo maana yake hakuna mahali ambako chama hicho kina nguvu. Hakina mwakilishi, kisha unataka kiwe katika serikali. Huyo mwakilishi atakuwa na msingi gani unaomfanya aonekane kuwa ametokana na ridhaa ya wananchi? Muundo huo ndio unaonipa wasiwasi.

  SWALI: Sasa tuzungumzie kura hii ya maoni kuhusu Muafaka.

  JAJI WARIOBA: Kura hii ya maoni ni kitu kingine kinachonipa wasiwasi. Inanipa wasiwasi sana. Ni kweli, ingekuwa vizuri kwa mambo mazito kupata kura ya maoni ili kupata ridhaa ya wananchi. Hilo ki msingi hakuna ayeweza kupinga. Lakini kwa hali halisi ya matatizo ya Zanzibar, je, kura ya maoni inaweza kutatua tatizo hili?

  Kama nilivyopata kusema, matatizo ya Zanzibar yanatokana na uchaguzi. Wakati wote, wakati wa ukoloni, baada ya ukoloni, baada ya kurudisha mfumo wa vyama vingi, matatizo ya Zanzibar yametokana na uchaguzi.

  Kila tukifanya uchaguzi matokeo yaleyale yanatokea. Kura ya maoni ni uchaguzi, ukipiga kura ya maoni, matatizo ambayo tumekuwa tunapata yatajitokeza. Kwa hiyo, utakuta wale ambao wanaunga mkono CCM wataendelea kuunga mkono CCM na wanaounga mkono CUF watafanya hivyohivyo. Kutakuwa na mgawanyiko uleule. Lakini zaidi, madhambi hayahaya ambayo yanatuletea matatizo sasa hivi yatakuwapo.

  Kutakuwa na udanganyifu katika kupiga kura ambao umekuwa ukitokea. Maana tumeshuhudia kila tunapofika wakati wa kupiga kura vyama hivi vinatafuta wapiga kura kutoka nje ya Zanzibar. CUF wanatafuta, zaidi kutoka Pemba, waandikishwe Unguja kupiga kura na CCM wanapeleka Pemba waende wapige kura, na hiyo haitalamalizwa na kusema tu kwamba hii ni kura ya maoni.

  Lakini pia viongozi, wapo na wanatofautiana. Wapo wanaotaka ushirikiano na ambao hawautaki. Hali hiyo itaendelea hata wakati wa kura ya maoni, utakuta kuna viongozi ambao wanakwenda kushawishi wananchi wakatae. Na kwa hali tuliyonayo uwezekano wa kukataliwa Muafaka huu ukienda kwenye kura ya maoni ni mkubwa sana.

  Wananchi wakiukataa Muafaka, tatizo la Zanzibar litakuwa kubwa zaidi kwa sababu hapatakuwa na njia tena ya kupata Muafaka. Mimi sioni, kwa hali halisi tuliyonayo, kwamba kwenda kwa wananchi ndiyo kutatua tatizo hili.

  Kinadharia, watu wanaweza kusema kwamba ni muhimu kupata mawazo ya wananchi, sawa. Lakini kwa suala la serikali mbona tumepitsha mambo mazito kabisa ambayo yanahusu wananchi. Tumebadili Katiba kwa mambo yanayohusu wananchi na hatukusema twende tupate maoni ya wananchi.

  Hapa ni suala la uongozi tu, kuna mgawanyiko katika uongozi. Wale ambao hawataki Muafaka wanaona njia ni kusema tupate maoni ya wananchi wakitarajia kwamba wananchi watakataa. Hiyo haitatusaidia, si Zanzibar wala Tanzania.

  SWALI: Kule Butiama kwenye mkutano wa NEC wapo wajumbe kutoka Zanzibar, ambao kwa chuki yao ya Muafaka nadhani, walisema ikibidi watarejea kwenye Afro Shirazi Party (ASP) kuliko kuingia katika Muafaka na CUF. Unalizungumziaje hilo?

  JAJI WARIOBA: Nimelisikia hilo. Sina hakika kama ni kweli au la. Lakini kama ni kweli, nadhani hawa ni watu wanaotishia tu. Ningekuwa kwenye nafasi ya kuamua, ningewaruhusu warudi ASP.

  Kwa sababu sasa ni miaka 30 tangu ASP na TANU viunde CCM. ASP na TANU vilikwisha. Tukaunda CCM. Sasa kama kuna mtu bado anaamini anaridhika zaidi akiwa ASP, arudi. Kama wanataka kuunda ASP waunde. Mimi nisingewakatalia. Kuna watu ambao wanaomba wangekuwa na TANU. Bara wanataka TANU. Kama wanataka kuanzisha TANU waende wakaanzishe.

  Hivi vilikuwa ni vyama vya wananchi. Vilifanya kazi kubwa, lakini sasa vyama hivi ni historia. Tuitumie historia hiyo na tumejifunza kutoka kwenye historia hiyo.

  Mimi nilikuwa kijana wa TANU, nimekaa katika TANU. Niliingia katika Halmashauri Kuu ya TANU miaka 31 iliyopita. Wakati CCM inaundwa kijana wangu wa kwanza alikuwa na miaka minane. Huyu kama ni siasa anachofahamu ni CCM, kwake TANU ni historia. Ukichukua watu wa umri huo, watu wa miaka 40 na 45, maisha yao ya siasa yamekuwa ni CCM. Kwao ASP na CCM ni historia.

  Ni historia nzuri. Inawafunza tulikotoka na kazi nzuri iliyofanywa na ASP na TANU. Lakini maisha yao ya kisiasa ni CCM. Kama mtu anataka kurudi, akafufua ASP mimi sina hakika kama hawa atawapata. Waone CCM haiwafai, waende ASP? Lakini kama kuna watu wanataka, muwaruhusu waunde ASP kisha uje uchaguzi wagombee kama ASP, tuone kwa Zanzibar ya sasa, na kama Wazanzibar wa sasa wataiunga mkono hiyo ASP.

  Mimi nadhani hii ni kauli ya kutishia tu. Kama kweli ni ya dhati wawaache warudi. Wakirudi ASP si kwamba wataua CCM Zanzibar. CCM itabaki. Acha ASP ije ipambane na CCM na CUF. Hapa kinachofanyika ni kuendekeza watu ambao wanatishia kwa kutumia historia.

  Sijui kwa nini watu wanababaika wakisikia mtu anasema anataka kurudi ASP. Tungekuwa makini hili tungelikataa kabisa. Tungesema tuna matatizo, ni ya wakati huu, tuyashughulikie kwa hali ya sasa hivi tusiende kwenye historia.

  Zaidi wanaosema warudi ASP ni watu wa Zanzibar, lakini nadhani pia kuna udhaifu katika viongozi Bara. Wakiisha kusikia madai hayo ya ASP, wanasema jamani waachieni mambo yao! Lakini haya si mambo yao, ni mambo ya nchi. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, likitokea tatizo Zanzibar ni tatizo la Tanzania. Hawa wanaosema waachieni haya ni mambo yao ni viongozi dhaifu.

  Ni lazima hili tulione kuwa ni tatizo la nchi, tulishughulikie. Asije akatokea mtu akasema hili ni la kwetu Zanzibar, tuachieni. Tukiendelea hivyo, atakuja mtu kutoka Bara atasema hili ni la Bara tuachieni. Na tunazungumza kuimarisha Muungano, hatuwezi kuuimarisha kwa kauli hizi za tuachieni ni mambo yetu.

  Hili ni suala la pande zote mbili. Zanzibar wasianze kutishia kwamba wanarudi huko nyuma, na wa Bara wajue kuwa hili ni suala la Tanzania wachukue msimamo.

  Kuna mambo tumepata kufanya pamoja. Mwaka 1984 tulishughulikia suala la uongozi wa Zanzibar kwa pamoja. Hata tulipowashughulikia kina Seif ( Seif Sharrif Hamad) mwaka uliofuata, tulikuwa pamoja. Sasa ni kwa nini yawepo mambo ya Zanzibar yanayoshughulikiwa kitaifa na kisha yapo mengine ambayo wanasema yashughulikiwe na Zanzibar? Wakati umefika kwa pande zote mbili kulitazama hili kwa sura ya kitaifa.

  Mtu mmoja alitania aliposikia kuwa Serikali inashughulikia kero za Muungano. Yeye akasema moja ya kero za Muungano ni Zanzibar. Huko nje wanapozungumzia na kukosoa Tanzania, wanazungumzia Zanzibar. Kwamba katika Muungano, Zanzibar imekuwa ni kero. Kwa hiyo hili ni suala la kitaifa, tunapaswa kulishughulikia kwanza.

  SWALI: Ukisoma lugha ya CUF ni kwamba hawatakaa tena na CCM. Tena, wengine wanakwenda mbali zaidi wakisema kwamba lugha ya kura ya maoni haimo katika Katiba.

  JAJI WARIOBA: Ni kweli hakuna sheria ya kura ya maoni. Kwa hiyo kama unataka kura ya maoni lazima utengeneze utaratibu wa kupiga kura hiyo ya maoni. Na tumebakiza miaka miwili tu kabla hatujafika kwenye uchaguzi. Na hatuwezi kuendelea na hilo bila kulimaliza mpaka uchaguzi ujao. Tungependa uchaguzi wa 2010 usiwe na matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita.

  Lakini lile la kwamba CUF hawataki tena kuzungumza, ningesema tu kwa vyama vyote viwili kwamba hakuna namna, bali ni kuzungumza. Lazima wazungumze kwa sababu hakuna mbadala katika suala hili. Hakuna njia ya katikati. Lazima wazungumze, wanaweza kutofautiana, lakini waende wakae wapate njia ya kuendelea suala hili.

  Kwa CUF wasifikiri maandamano na kushinikiza kutaleta suluhu. Hapana. Hili linataka wote tukubaliane. Kwa hiyo badala ya kusema waendelee kwa maandamano ili CCM ikubali ama waende nje kushinikiza, haitasaidia. Kwanza uzuri ni kwamba suala hili tumekuwa tukilizungumza wenyewe bila ya watu wa nje. Wakiingia wa nje, tutapata matatizo makubwa. Wataleta masharti na inaweza kutuharibia.

  CCM, nao wafahamu, na muhimu zaidi, wasikilize hoja. Ikiwamo hoja kwamba walipofikia CUF, hawawezi kwenda zaidi. Kwamba kama mnakwenda kuzungumza kuwa na kura ya maoni, je, kamati iliyojadili Muafaka huo itaweza kufikia makubaliano juu ya hilo?

  Kama haiwezi kufikia makubaliano juu ya hilo ni lazima utaratibu mwingine wa kuendeleza mazungumzo utafutwe. Malumbano ya pande zote hayasaidii.

  Walipokuwa wakizungumza walileta matumaini, malumbano ya sasa yanazidi kuwagawa wananchi. Hayatasaidia. Ni lazima wake pamoja, watafute njia ya kuendeleza mazungumzo na kukamilisha Muafaka huu.

  Katika Muafaka kuna sehemu ya nne, huko nyuma tatizo moja limekuwa ni utekelezaji. Kwamba tunafikia Muafaka kisha Serikali inapewa jukumu la kutekeleza. Kisha unakuta CUF inalaumu tu kwamba Serikali haitekelezi. Katika Muafaka huu, wakisha kukubaliana, wataunda serikali ya pamoja, hiyo ndiyo itakuwa chombo cha utekelezaji. Maana yake ni kwamba wakiisha kutia saini wanaunda serikali ya pamoja ambayo ndiyo inakuwa chombo cha utekelezaji.

  Nafikiri ni makubaliano mazuri na kwa kweli yanaweka msingi wa kuja kuwa na serikali ya pamoja baada ya uchaguzi unaokuja. Ni jambo la kawaida kuwa na serikali ya pamoja. Mimi sioni matatizo makubwa sana ya hiyo.

  Huko nyuma nilipata kutoa mifano. Afrika Kusini baada ya kuondoa serikali ya kibaguzi mwaka 1994, katika uchaguzi ule ANC ilipata viti vingi, ingeweza kuunda serikali bila kushirikiana na chama chochote.

  Lakini si tu kwamba walikubali kushirikiana na chama kikubwa cha upinzani cha William de Klerk, lakini walichukua hata vyama vidogo vyote. Inkatha waliingizwa, PAC (Pan Africanist Congress) waliingizwa na vyama vidogo vyote viliingizwa katika serikali.

  Inkatha iko katika jimbo moja tu, Kwazulu Natal, chini ya Wazulu, ni kama chama cha kikabila, lakini walikiingiza kwenye serikali. Kingozi wake Chifu Mongusutu Buthelezi akawa namba nne katika orodha ya viongozi wa juu uliokuwa na Rais Nelson Mandela, de Klerk na Thabo Mbeki kisha Buthelezi. Kwamba kama Mandela hayupo, hawa watatu wanaweza kushika nchi, na kuna wakati Buthelezi alishika nchi, akaendesha kama Rais.

  Kwa nini walifanya hivyo? Wenyewe walikuwa wanataka umoja. Walijua wanatoka katika mfumo uliokuwa umewagawanya kabisa. ANC wakaogopa, wakasema ingawa tumepata viti vingi itaonekana kuwa ni serikali ya Waafrika. Tena Waafrika wa makabila kadhaa tu. Wakasema wanataka kuunganisha Afrika Kusini.

  Uchaguzi uliofuata mwaka 1999 wakapata kura kwa wingi mkubwa zaidi. Bado wakaendelea vilevile, mwaka 2004 walipata zaidi ya theluthi mbili lakini bado waliendelea vilevile. Wanataka kujenga umoja wa kitaifa. Hiyo ndiyo hali tuliyonayo Zanzibar. Zanzibar hatuna umoja.

  Tukifanya kazi kwa umoja tutaunganisha Zanzibar. Na hii haina haja ya kwenda kupata kura za maoni. Mbona Kenya tumekwenda kusaidia? Wamekubaliana, wamepeleka kwenye Bunge, wamepitisha.

  SWALI: Lakini ili mfike mahali kama Kenya si lazima pawe na utashi, hasa kwa uongozi wa juu kabisa? Lakini pia pawe na maono, kwamba kwa mwendo huu huko tuendako yataibuka makubwa na yatakuwa mabaya?

  JAJI WARIOBA: Mimi nataka kuamini kwamba viongozi wetu wanataka tatizo hili limalizike. Katika hotuba yake ya kwanza kabisa bungeni, Rais Jakaya Kikwete alilifanya hili kama mojawapo ya masuala muhimu ambayo angeyashughulikia. Naamini hivyo. Ushauri wangu ni kwamba katika mambo haya ya mazungumzo mambo huwa magumu sana.

  Kwa sababu mnaanza hamjaaminiana, kila mmoja anamshuku mwenzake. Mkiendelea mnaanza kuaminiana na mtaendelea hivyo hadi kufikia sehemu kubwa ya muafaka. Mwisho huwa mgumu sana, kama mmehitilafiana sehemu ile ya mwisho huwa ngumu sana. Hapa sasa kuna tofauti, tuwe na kura ya maoni au tusiwe na kura ya maoni.

  Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa.

  Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaimu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana. Manufaa ya Taifa sasa hivi ni kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Lolote linalohitajika kumaliza mpasuko huo ni vizuri viongozi wakachukua uamuzi, utakuwa ni mgumu lakini ni wajibu wao kuchukua uamuzi.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bluray,
  Hawa Wazanzibar wanachekesha sana yaani hata sielewiwanachojaribu kusema hapa.. Kuanzia mwkaa mwaka 2001 nimekuwa nikiwaambia viongozi wa Zanzibar kuhusu referendum, nimeakilisha mawazo haya ktk vijiwe mbali mbali nahata ktk mikutano yao lakini wapi wamechukua miaka mingapi hata kufikiria tu..

  Kisha basi swala la zanzibar kujitenga na Bara sii swala la CUF tu, nina hakika viongozi wengi na wananchi wengi wqa Zanzibar wanataka kujitenga isipokuwa wanashindwa kusimama pamoja kwa sababu hakuna mtu anayethubutu kunasha hoja hiyoi bungeni mwao.. Kila mmoja anaogopa yaliyomkuta Malecela, kila mmoja anaogopa ataanza na lugha gani..

  Kwa hiyo yoote haya yanazungumzwa kichini chini tu wkwa sababu sioni sababu ya hoja hii kukataliwa bungheni ikiwa serikali ya ASP na chama CUF wote wanaunga mkono kuwepo kwa referendum, besides hawajawahi kujaribu kuwakilisha z muswada huo zaidi ya maneno matupu...
   
 5. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wananchi wa scotland hawataki independence, ila viongozi ndio wanachochea kwa ulafi wa madaraka
  hata gordon brown zamani kabla hajawa kwenye rank za juu alikuwa anataka independence na siku hizi amesahau kabisa hicho kitu..
  SNP wanachelewesha referendum kwa ajili wanajua wananchi wa scotland hawataki kuwa independent
   
 6. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Lisemwalo lipo halipo linakuja
   
Loading...