SMZ yaridhia Taasisi zake kutoa likizo za lazima ili kupunguza misongamano. RC Makonda apiga marufuku wazururaji Dar es Salaam

Kabla Gwaji boy hajaunga juhudi alishawahi kusema "Zero always is Zero" hivyo hatuwezi tarajia lamaana toka kwa mtu huyo tumuombe Mungu amsaidie

"Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu"


Mithali 12:23
Hatarious
 
Ni wazi hakuna leadership kwenye kupambana na Corona wala mkakati kutegemea kauli za viongozi wetu badala ya wataalamu ni kujiweka kwenye hatari mbeleni.

Labda kama una health condition, umri umeenda na wale wengine percentage ndogo sana ya vijana ambao Corona inawasumbua vibaya kwa sababu ambazo azijaeleweka.

Wengi Corona ikiwapata ni homa yakawaida tu (ndio maana kipimo cha awali ni temperature) kubaini kama kuna homa ili uchunguzwe zaidi iwapo ni ya kawaida au la.

Corona ukipata kwa wasio kwenye risk groups ni homa kwa sana kuliko mafua na kifua (na iwapo kuna kifua kikavu ndio ukimbilie hospitali). Kwa homa pekee inadumu kwa wiki mbili mpaka tatu huko mbele ujue hospitali zitajaa na asilimia kubwa ya watu itabidi kujitibu majumbani, kasheshe sasa usiwe na paracetamol au dawa zako za kawaida Corona ikikikuta.

Hizo dawa zitaadimika tu pharmacy kadri siku zinavyoenda, sasa sijui itakuwaje.
 
Makonda wa Juzi alisema wananchi msijifungie ndani, tokeni nje mfanye kazi na biashara la sivyo mtakufa kwa njaa.

Makonda wa leo anasema kuanzia kesho ukionekana nje mtaani bila shughuli maalumu utakamatwa kwa kosa la uzururaji. Maajabu.

Machinga atapata wapi wateja bila kutembea mtaani? Nini tofauti kati ya mzururaji na mteja anayekwenda kununua bidhaa?

Mungu tunaomba hekima.
 
April 5 , 2020
Mpya Hivi punde

Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini Hosteli za Magufuli


Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini Hosteli za Magufuli ... kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli....
Source:
Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini hosteli za Magufuli .

Serikali imetangaza rasmi kwamba wasafiri wote kutoka nchi za nje zilizoathirika na ugonjwa wa Corona watalazimika kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli.

Akizungumza katika hosteli za Magufuli, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema wasafiri hao watafikia katika hosteli za Magufuli ambazo zipo katika eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam.

“Lengo ni kuhakikisha tunadhibiti mienendo ya wasafiri hawa.Tumeona taarifa ambazo zimetoka kule Iringa, kuna baadhi ya wasafiri tuliwaweka hotelini wakatoroka sasa ili kudhibiti mienendo ya wasafiri hawa na kuwalinda Watanzania wengi tumeona kuna ulazima wa kuwaweka sehemu moja ambako kutakuwa na ulinzi wa saa 24 na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam,Bw. Paul Makonda atasimamia kwa karibu chini ya Wizara ya Afya,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi waelewe kwamba wasafiri hao si wagonjwa kwa sababu wanatoka kwenye nchi zenye maambukizi yenye virusi vya Corona (Covid-19) hivyo wasichukuliwe kama ni wagonjwa.

“Tunawachukulia kwamba miongoni mwao kuna mmoja, wawili au watu watatu wakawa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Tutawaweka hapa kwa siku 14 kwa lengo la kuwaangalia afya zao, itakapofika siku 14, wale ambao hawajaonyesha DALILI zozote tutawaruhusu waende majumbani kwao lakini wale watakaoonyesha dalili ndani ya siku tano, sita, Saba, nane hadi siku ya 14 tutachukua sampuli na kuwapima ili kujiridhisha Kama wana virusi vya Covid-19,” amesema Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa kwa mujibu wa taarifa za maambara Hali ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19.“Tuko vizuri, watu waliopata maambukizi ni 20, tumepata kifo kimoja, wagonjwa watatu wamepona na wamesharudi nyumbani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameishukuru Wizara ya Afya kwa namna ambavyo Imekuwa ikipambana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Corona nchini.

WhatsApp-Image-2020-04-05-at-07.43.38-1024x683.jpeg



“ Sisi Kama Mkoa tumejipanga kuhakikisha kwamba watu wote wanaokuja na ambao wapo wanakuwa na afya Njema kwa ajili ya kujenga uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla.

“Maelekezo ambayo ameyatoa mheshimiwa waziri wa Afya ni maelekezo ambayo kila anayeingia kwenye Mkoa huu kutoka nchi yoyote, Magufuli hoteli inamuhusu,” amesema Paul Makonda.

Makonda amewataka Watanzania kufanya kazi na kwamba kuanzia kesho jumatatu atawakamata wazururaji wote wanaozunguka mjini bila kuwa na kazi maalumu watakamatwa kwa kuwa wanasababisha mikusanyiko isiyokuwa na tija.
 
safi sana RC Makonda, naunga mkono hiyo safisha safisha, wazururaji ni wengi hapa mjiini,hawana shughuli maalum wanaleta msongamano wa buree, tuwasake kote, pia wazururaji ndio vibaka wenyewe.

Wenyeviti wa serikali za mitaa msaidieni Mkuu wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bagamoyo,
Nani anagharamia? Yaani CEO wa crdb boss nsekela katoka uswis .kutanoni umpeleke magufuli hostel? Acheni utani
 
Thukilala ndhani thuthakuva njaa.. Acha thukadhurure bhana. Huyu ni Makonda tofauti na yule wa jana au?
Na hiyo ndio shida yangu, kuna uwezekano wa kuwepo kwa Makonda na Bashite. Au cloning imechukua nafasi yake.
 
safi sana RC Makonda, naunga mkono hiyo safisha safisha, wazururaji ni wengi hapa mjiini,hawana shughuli maalum wanaleta msongamano wa buree, tuwasake kote, pia wazururaji ndio vibaka wenyewe,
wenyeviti wa serikali za mitaa msaidieni Mkuu wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wangetaka hivyo, vitambulisho vya nida vingeonyesha kazi ya mtu, hii nchi Nani hajawahi zurura?
 
Katika critical issue kama hii, inaongozwa na slouch person kama Bashite, tutegemee minus zero results, tena with a devastatin impact..
 
Back
Top Bottom