SMZ imeitaka polisi kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa wanaochochea fujo Zanzibar

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,578
2,000
smz25(1).jpgSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria kwa wanasiasa ambao wanahubiri vurugu na fujo na kuwahamasisha wananchi uvunjaji wa amani kisiwani Zanzibar.

Kauli hiyo nzito ya serikali imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mhe Mohmaed Aboud wakati akizungumza na askari wa jeshi la polisi akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa cheo cha Ukoplo na Sajenti yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Messi hapa Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu wa jeshi hilo na wananchi ambapo amesema Zanzibar imepania kuwa kisiwa cha amani lakini wako wanasiasa wanataka kuharibu amani hiyo hivyo amelitaka jeshi hilo kutoacha kuchukua hatua za kisheria kupinga kwa nguvo zote vitendo hivyo.

Naye kamishna wa polisi Zanzibar CP Hamdan Omar Makame amewataka wahitimu hao kuingia uraiani kwa kutekeleza mafunzo waliyoyapata na kuweka heshima kubwa ya jeshi hilo katika kuwatumikia wananchi kwa hoja za kisheria na kuepukana na vitendo vya rushwa na ubaguzi, kwa upande wake mkuu wa chuo hicho ACP Deus Dedit Msimeki amesema umefika wakati wa mafunzo hayo kufundishwa kitaalamu zaidi hivyo ameishauri serikali kuimarisha eneo lao la mafunzo ili liweze kukidhi mahitaji ya elimu hiyo nchini.

Katika hafla hiyo Mhe Mohamed Aboud alikagua gwaride rasmi liloandaliwa na jeshi hilo ambapo baada ye jeshi hilo lilipita mbele ya Mhe waziri kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa na baadaye kupita kwa mwendo wa kasi ambapo liliwachangamsha wananchi waliofurika katika uwanja huo.

Katika mafunzo hayo ya miezi Mhe Mohmaed Aboud aliwatunuku vyeti na kuwavisha askari waliomaliza kozi hiyo ya Ukoplo na Sajenti huku katika mafunzo hayo jumla ya askari walioshiriki mafunzo hayo na walomaliza.

Chanzo: ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom