Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano litajulikana hatima yake baada ya miezi minne.
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, alisema jana kuwa suala hilo tayari limezungumzwa katika vikao vya pamoja vya kujadili kero za Muungano na kukabidhiwa Makamu wa Rais wa Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bilal, ili
kulifanyia kazi kabla ya ufumbuzi wake kutolewa ndani ya miezi minne.
Azimio la kuondolewa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano lilipitishwa na Baraza la
mapinduzi Zanzibar na kuungwa mkono na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwaka 2009.
Hata hivyo suala hilo limechelewa kuodolewa katika orodha ya mambo ya Muungano kutokana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuchelewa kutoa msimamo juu ya mamuzi ya Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE