Slaa: Please fuatilieni hili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa: Please fuatilieni hili.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Mar 24, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Diwani Mbeya afichua ufisadi michango ya shule

  [​IMG]
  Felix Mwakyembe, Mbeya​
  Machi 23, 2011[​IMG]
  [​IMG]Wafanikiwa kujenga madarasa kwa michango ya 3,000/=

  [​IMG]DC atumia vitisho, kisa diwani ni CHADEMA


  [​IMG]Wananchi washitukia ufisadi kwenye michango  WANANCHI wa Kata ya Mwakibete jijini Mbeya wamekuja na ufumbuzi wa michango kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari, lakini Mkuu wa Wilaya hiyo, Evans Balama, anawaona ni wapinga maendeleo, kisa wanachangishana 3,000/= badala ya 10,000/= anazozitaka yeye.
  Kamati ya Maendeleo ya Kata (KAMAKA) hiyo ya Mwakibete ikiwa chini ya uongozi wa Diwani Lucas Mwampiki kutoka Chama cha Demokrasia na
  Maendeleo (CHADEMA) iliamua kiwango cha mchango kiwe 3,000/= kufanikisha ujenzi wa vyumba saba vya madarasa katika shule yao ya sekondari badala ya kiwango kilichozoeleka cha 10,000/=. Msingi wa hoja ya KAMAKA inajengwa na ukweli kwamba kiwango cha 10,000/= kilikuwa kikilalamikiwa sana na wananchi kwamba hakina ufanisi, kwa maana thamani ya fedha kutonekana kwenye kazi, kwamba hakikukusanywa kwa ufanisi na hata makusanyo yake halisi hayakufahamika.

  Wananchi wanaiona michango hiyo kama sehemu ya mradi wa viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi wilayani, kujikusanyia mapato kwa kisingizo cha ujenzi wa shule.
  Hesabu ya Kamati hiyo ya Maendeleo Kata ya Mwakibete ni rahisi sana, wamechukua idadi ya wakazi wenye uwezo wa kuchangia wakazidisha na shilingi elfu tatu wakapata shilingi milioni 22.5 ambazo wanasema zinawatosha kujenga vyumba saba vya madarasa, kila chumba kikigharimu shilingi milioni tatu ambayo ndiyo inayoelekezwa na serikali.
  Pamoja na hesabu kuonyesha kuwa fedha hizo zinatosha, bado Kamati hiyo iliweka angalizo na kukubaliana na wananchi wake kwamba iwapo patakuwapo na mapungufu basi watakaa tena na wananchi kupanga kiasi gani wachangie kulingana na mahitaji yatakayojitokeza. “Tukianza na shilingi elfu tatu tunaangalia impact yake. Tunalinganisha na gharama halisi, iwapo hazitoshi tunakaa tena na wananchi kuangalia kiasi kinachopungua tunachangia tena. Wananchi walikata tamaa, kupunguza ni kuwa motivate waone kile kidogo walichochangia kimefanya kazi. Itawahamasisha zaidi,” anasema Diwani Mwampiki.

  Anaongeza Mwampiki: “Wananchi wanapenda kuchangia maendeleo. Wanakatishwa tamaa na sisi viongozi kwa kutokuwa wawazi kwenye masuala yanayohusu michango yao.”
  Mwalimu wa shule moja ya sekondari jijini Mbeya ameiambia Raia Mwema kwamba wananchi hao wa Kata ya Mwakibete wamekabiliana na tatizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa uhalisia zaidi kuliko msukumo wa kisiasa ambao hutoa mwanya kwa wajanja wachache kujinufaisha na michango hiyo. “Jambo la msingi hapa ni vyumba kujengwa. Hawa wananchi wametumia busara zaidi, wamepiga hesabu wakaona shilingi elfu tatu inatosha kukamilisha vyumba wanavyovihitaji, na impact yake inaonekana, hata ikifeli ni wazi watakuwa na moyo wa kuchanga zaidi kwani kazi inaonekana,” anasema mwalimu huyo na anaongeza:

  “Watu wamehamasika. Kazi inaponekana wanahamasika zaidi. Ile michango ya 10,000/= wananchi hawakuona kazi yake na wala kupewa mrejesho. Naona diwani amehamasisha vema. Watu walishajenga mtazamo hasi na hii michango.”
  Utaratibu wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kama unavyoelekezwa na Mpango wa Maendeleo ya Shule za Sekondari nchini ni kwamba wananchi wanajenga maboma hadi kiwango cha lenta au ring beam na serikali inamalizia.
  Hadi Machi 05, mwaka huu wananchi wa Kata hiyo ya Mwakibete, kwa michango yao hiyo hiyo ya 3,000/ walikuwa wamekamilisha ujenzi wa vyumba vitatu na sita vikiwa katika hatua mbalimbali. Miongoni mwa vyumba hivyo tisa, vyumba saba vinajengwa kwa nguvu za wananchi huku viwili vikijengwa kwa michango ya wazazi wenye watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo.
  “Watu wameitikia sana. Nina mitaa saba katika Kata yangu. Kila mtaa unajenga chumba kimoja. Kuna mitaa wamefikia kwenye lenta wanasubiri mchango wa Serikali,” anasema Diwani Mwampiki.
  Wananchi wanahoji, iwapo Kamati ya Maendeleo ya Kata ndiyo yenye kusimamia ujenzi na iliyo karibu zaidi na wananchi, iweje Mkuu wa Wilaya ang’ang’anie 10,000/=, analenga kumnufaisha nani, na wanahoji zaidi uharaka wake kwamba kwa nini asisubiri matokeo ya kiwango walichokubaliana cha 3,000/= iwapo kina ufanisi au la?
  Mkuu wa Wilaya hiyo alifika kuonana na Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo na kuishutumu kwa hatua yake hiyo huku akidaiwa kumtishia Diwani Mwampiki kwamba anao uwezo wa kumfanya lolote kwa kuwatumia Usalama wa Taifa na kutamba kuhusu ukada wake kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).
  Diwani Mwampiki anaweka wazi vitisho hivyo katika barua yake ya malalamiko aliyomwandikia Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, akimnukuu Mkuu wa Wilaya akisema:
  “Nina uwezo wa kukufanyia kitu chochote na jambo lolote kwa kuwatumia Usalama wa Taifa ili kukuondoa katika nafasi hiyo ya udiwani, japokuwa kufanya hivyo ni dhambi mbele za Mungu lakini nitamuomba Mungu anisamehe,” kisha katika barua hiyo Mwampiki anaendelea kumnukuu DC Balama akisema:
  “Mimi nimezaliwa ndani ya CCM, nimekulia ndani ya CCM, nimesomea ndani ya CCM, ninafanya kazi ndani ya CCM, hivyo sitakuwa tayari kuona vyama
  uchwara na sera zake uchwara ndani ya mamlaka yangu.”
  Diwani Mwampiki hakuishia kumwandikia Meya wake tu bali amewapelekea nakala ya barua yake hiyo, ya Desemba 30, 2010 (nakala tunayo), viongozi kadhaa mkoani Mbeya wakiwemo, Mkuu wa Mkoa, Afisa Usalama Mkoa, Kamanda Polisi Mkoa, Katibu Mkuu CHADEMA Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini, Katibu CHADEMA (W) na Mkuu wa Wilaya mwenyewe.
  “Nawasilisha kwako ili Ofisi yako ilione hili pia ipate ufafanuzi wa kauli hatarishi na za kiimla kama hizi. Katika zama hizi za utawala bora ambao naamini Serikali anayoitumikia yeye ni muumini wa dhana hii ya utawala bora, je, hayo ndiyo matumizi ya Uslama wa Taifa,?” anahoji Diwani Mwampiki kwenye barua yake hiyo kwa Meya Jiji la Mbeya.
  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya hakanushi madai hayo ya kumtishia diwani huyo, zaidi anasisitiza kwa kuwaelezea wapinzani wa michango ya 10,000/= kuwa ni wahuni, wapinga maendeleo na wavunja sheria za nchi, kwake thamani ya kazi si jambo la msingi.
  “Hao ni wahuni, wapinga maendeleo, michango imepitishwa kisheria, ipo kwa mujibu wa sheria za Jiji, walipitisha 10,000/= . Huyo anayesema ufanisi wa 3,000/= nani huyo. Kama unataka kubadilisha sheria unafuata taratibu za kisheria zilizopo. Kwanza mimi nimesamehe tu, ningeweza kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria,” anasema Mkuu huyo wa Wilaya katika mahojiano na Raia Mwema yaliyofanyika kwa njia ya simu na anaendelea kuweka msimamo wake:
  “Yeyote anayepinga sheria nitamshughulikia. Huwezi kumuondoa mtu katika nafasi yake ya uongozi hivi hivi. Zipo taratibu za kisheria kumuondoa. Nilisema hivi, anayekwamisha shughuli zetu za maendeleo nitamshughulikia. Nitamuondoa katika nafasi yake kwa mujibu wa sheria.”
  Wakati Mkuu huyo wa Wilaya akiendeleza msimamo wake huo, baadhi ya maafisa waandamizi ndani ya Usalama wa Taifa mkoani humo wanamuona kuwa ni kiongozi mkorofi na asiye na uwezo wa kusoma alama za nyakati, wanabainisha wazi kukerwa kwao na kauli yake kutumia idara hiyo kuwatisha viongozi wa kutoka vyama vya upinzani.
  “Hata mimi nilimuona yule diwani ana akili zaidi kuliko sisi. Tatizo hawa ma DC wengi wamepata nafasi hizo kutokana na ukada wao kwa chama. Wako nyuma ya wakati. Bado hawaamini mambo yamebailika. Wanadhani upinzani ni uhaini,” anasema afisa mmoja mwandamizi wa idara hiyo nyeti.
  Wakati Mkuu huyo wa Wilaya aking’ang’ania kiwango cha 10,000/= kumekuwapo na shaka miongoni mwa wakazi wa Jiji hilo juu ya ufisadi kwenye michango hiyo ya ujenzi wa shule za sekondari.
  Shaka hiyo inajengwa na aina za stakabadhi zinazotolewa zinazodaiwa kutengeneza mwanya wa wizi pamoja na baadhi ya wachangishaji kutumia kopi za stakabadhi zenye namba aina moja.
  [​IMG]


  MY TAKE: CHADEMA INABIDI KUMBEBEA BANGO DC HUYU KWA MAANA AMEVUNJA SHERIA ZA NCHI KWA KUTUMIA VIBAYA NAFASI YAKE KWANI
  YEYE HAJACHAGULIWA NA WANANCHI NA HIVYO AWAJIBIKI KWA WATU
  KAMA ALIVYO MHESHIMIWA DIWANI.  [​IMG] Mwanzo[​IMG] Toleo Lilopita[​IMG] Hifadhi[​IMG] Matangazo[​IMG] Tuwasiliane
   
 2. W

  WFM Senior Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 45
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 4. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
   
 5. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
   
 7. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,970
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG] JF Senior Expert Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Join Date : 14th November 2010
  Posts : 2,105
  Thanks 100 Thanked 400 Times in 246 Posts

  Rep Power : 25


  [​IMG] Re: SERIKALI: Katiba mpya 2014

  CHADEMA TUPENI MELEZO HARAKA JUU YA SWALA ZIMA KATIBA MPYA NA
  TUME HURU YA UCHAGUZI

  Tafadhali Mhe Dr Slaa, Mhe Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika na Uongozi wetu Mzima wa BAVICHA pamoja na Matawi yetu kote nchini na Vyuo Vikuu, tupeni majibu sisi wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba haya ya Oliver Mhaki yatoka wapi na kwa ruksa ya nani tena???

  Chonde tuokoeni na hizi hasira na kinyaa cha ofisi za Waziri Mkuu na Wizara ya sheria: Uongozi wa juu CHADEMA, kama jambo la dharura kitaifa, tunaomba ufafanuzi wenu juu ya hizi KERO ZA KUPIGISHA DANADANA SWALA ZIMA LA KATIBA MPYA NCHINI na vile vile mtufahamishe kwamba mpaka hivi sasa nyinyi wenyewe mnafahamu nini na mmeshirikiswa kiasi gani juu ya SWALA MASWALA NYETI ya:

  1. Tarehe ya muswada kupelekwa bungeni???
  2. Muswada wenyewe huo ni wa aina gani na je unasema kama wananchi tunavyotaka wenyewe???
  3. Haki ya serikali ya CCM kujipangia ratiba ya zoezi hili muhimu sana kwa maisha yetu kitaifa wamepata wapi??
  4. Je, inamaana CHADEMA hamtaki kutii amri yetu wananchi kupeleka mswada wetu kule bungeni kupitia kwa dogo Mnyika???

  NB: CHADEMA tupeni majibu ya uhakika na kwa haraka sana juu ya hili swala ambalo kumbe huko serikalini wameligeuza mdoli. Mungu wangu kumbe hawa CCM wapuuzi hivi?? Ngoja!!!!!
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,174
  Trophy Points: 280
   
Loading...