Mkuu, inaonekana unaandika kwa uchungu sana kuwashangaa na kuwaonea huruma wanachadema. Lakini unachokikataa wewe, wenzako ndio wameamua kuwenda nacho mbele, sasa ukiwa na uchungu sana na kitu kisichokuhusu, maana yake ni kwamba kitadumu hivyo hivyo huku wewe ukiwa hauna uwezo wa kukibadilisha, kwani sio miongoni mwa wanachama wa Chadema. Na kwa kuwa hakuna uwezekano kwako, utaishia kuumia roho mwishowe utakufa kwa mawazo. Ili usife au usiumie, fanya moja ya mambo mawili haya; Jiunge CHADEMA ili uwe na uhalali wa kuhoji AU kaa kimya uwaachie wanachadema walioridhika. Kuhamishia hasira zako za hawa wanachadema wasiohoji kwa chama chako cha CUF kunaweza kukusaidia pia kupunguza mawazo. Pole sana kwa kuandika kwa uchungu mkubwa, lakini tatizo ni kwamba jambo hili linawahusu wanachadema tu, labda wewe anza kumuandama Prof kuhusu muda wa uenyekiti wakeChadema mbona hawaundi tume huru kuchunguza hela ya Chama ?....
Chadema mwisho wao ndiyo huu hakuna kipindi kingine tena cha kuwazika wao wamefanya chadema kuwa ni sacos yao wanaendesha maisha yao kwa kuiba pesa za chama huku viongozi wa mikoa na wilaya hawalipwi kitu wanaambiwa wajitolee.
Hawa jamaa kwa kweli wameiua Chadema na kuirudisha nyuma sana ,kumbe tatizo ni hela walizochota kwenye chama na hawana wala hawaonyeshi nia ya kuzilipa ,sasa hizi ziara ambazo nazifananisha na za yule ndege Kinana ni kutaka kuziba ufa na kulifuta deni kwa kujazia mahesabu huko kwenye ziara ,ikiwa bado mwaka tu na ushei kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu ziara hizi hazikuwa na maana zaidi ya ufisadi tu wa kuzila hela za Chama na kuwalaghai wananchi.
Madai ya Zito na wenzake kutaka hesabu za Chama yana ukweli kuwa sio bure kuna watu wanakula hela ndani ya Chama chao na hakuna wa kuwahoji ,badala yake wakubwa hao wanadai Chama ni Cha watanzania wote wapenda demokrasia hivi ,hapa pana demokrasia hapa ? Au ni wizi tu na kujirundikia mali kupitia hela za Chama.
Chadema mbona hawaundi tume huru kuchunguza hela ya Chama ? Kuna siri gani kwani tuhuma za kula hela sio ndogo na wahusika wawajibishwe ikionekana kweli.
Nawaonea huruma sana wanachadema ambao hawana mdomo wa kuwahoji viongozi wao na wale wanaowatumainia wakiinua sauti wanafukuzwa na hili genge la watu wachache waliokidhibiti chama.