Slaa: CCM wanafiki

Slaa: CCM wanafiki

Isaac JK

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
563
Reaction score
92
KATIBU Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amesema viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni wanafiki ndiyo maana amani na utulivu vinaanza kupotea. Alisema serikali ya chama hicho ni mtuhumiwa mkubwa wa uvunjifu wa haki mbalimbali za wananchi lakini imekuwa kinara wa kuzungumzia amani ambayo ni tunda la haki.

Kauli hiyo aliitoa juzi mkoani Manyara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kukijenga chama ambapo alisema viongozi wa CCM wamekuwa wakihubiri amani bila kuzungumzia haki ambayo ni msingi wa amani na utulivu imara. "Kama watawala wangekuwa na dhamira ya dhati na amani ya nchi hii, wangetenda haki, amani haihubiriwi majukwaani ni tunda la haki na matumaini ya wananchi kwa viongozi wao," alisema.

Alisisitiza kuwa ni vigumu kwa viongozi kueleweka kuwa wana nia ya dhati kuona nchi ikitawalika kwa amani na utulivu, wakati wananchi wengi wanaendelea kutaabika kwa kunyimwa haki zao na kunyanyaswa ndani ya maeneo yao. "Nani hajui uvunjifu wa haki za wananchi unaofanyika katika ardhi, elimu, ajira na usalama wa raia?...haya yanafanywa chini ya serikali ya CCM ambayo inahubiri amani inaacha haki, hawa ni wanafiki ndiyo maana nchi inawashinda," alisema.

Dk. Slaa pia alisema CHADEMA inajisikia fahari kuona serikali ya sasa inatekeleza sera za chama hicho kikuu cha upinzani nchini chenye utajiri wa mawazo mbadala mbalimbali namna ya kuwatumikia Watanzania. Alisema wamefurahi kusikia serikali ina mpango wa kuongeza miaka ya wanafunzi kusoma elimu ya msingi kutoka miaka saba ya sasa hadi 10, ambayo ilikuwa sera ya CHADEMA siku nyingi na waliinadi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akadai kuwa kutokana na mawazo mgando ya chama kilichoko madarakani na viongozi serikalini, walimbeza.

"Tunashukuru wameanza kutekeleza sera zetu. Sisi hatuna kinyongo kama wanatumia sera zetu kuongoza nchi hii, kwa sababu hatimaye anayenufaika ni mwananchi na hiyo ndiyo furaha yetu. Lengo letu ni Watanzania hawa kunufaika na nchi yao," alisema.
Alibainisha kuwa mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu waliposema kuwa wakiichukua nchi wangetoa elimu bure walijua wangefanya nini lakini CCM kwa mawazo mgando walibeza kwa madai haiwezekani.

Aliongeza kuwa CHADEMA ilisema ikichukua nchi itaangalia na kurekebisha mfumo wa kodi na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ikiwemo mfuko wa saruji uwe sh 5,000.

Alisema chama chake kilitoa kauli hizo kwa kuwa kinaamini bati, nondo na vinginevyo kadhalika, vingeshuka bei. Alisisitiza kuwa ni suala la formula na mfumo wa ulipaji kodi na uzalishaji viwandani, hilo nalo walibeza na wakasema haiwezekani lakini sasa wanatekeleza.

Tanzania Daima
 
Dr. Yuko sahihi, ccm chini ya serikali yao wameshindwa kuliongoza taifa letu kwa msingi wa haki na utawala bora, tumeshuhudia wabunge wa upinzani hususani wa chadema wakikamatwa hovyo kama si viongozi waliochaguliwa na wananchi tena watanzania, wakati wabunge wa ccm wamekuwa lulu hata kwa uvunjifu wa sheria., wao ndio waheshimiwa, tumeshuhudia polis wakitumika kubambikizia wananchi wasio na hatia kesi! Usalama wa taifa hautumiki kwa maslahi ya taifa letu kwa kulinda raslimali na usalama kiujumla, unatumika kulinda mafisadi na kunyanyasa wapinzani, vyombo vya usalama vingi hunyanyasa raia na kung'oa kucha na meno waandishi wa habari! Viongozi wa ccm hutumia muda mwingi kuwatisha wananchi wasijiunge na vyama wavipendavyo hasa maeneo ya vijijini mfano Halisi ni Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, huyu ukimuangalia kwa haraka hana tofauti na majasusi au mafia, lakini ndani ya ccm amekuwa lulu! Ccm wakiendelea kuongoza taifa letu watalisambaratisha dalili zimeanza kuönekana!
 
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Chadema kusema wataakikisha nchi haitotawalika tena sio unafiki huo.
 
Dr. Slaa ndiye mnafiki kwasababu anatuambia anaweza kuliongoza taifa letu lenye watu zaidi ya milioni arobaini wakati ameshindwa kuiongoza familia yake isiyozidi watu kumi.
 
Wewe ni mmoja wa wanafamilia wake au ni kipele tu kinakuwasha?
 
KATIBU Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amesema viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni wanafiki ndiyo maana amani na utulivu vinaanza kupotea. Alisema serikali ya chama hicho ni mtuhumiwa mkubwa wa uvunjifu wa haki mbalimbali za wananchi lakini imekuwa kinara wa kuzungumzia amani ambayo ni tunda la haki.

Kauli hiyo aliitoa juzi mkoani Manyara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kukijenga chama ambapo alisema viongozi wa CCM wamekuwa wakihubiri amani bila kuzungumzia haki ambayo ni msingi wa amani na utulivu imara. "Kama watawala wangekuwa na dhamira ya dhati na amani ya nchi hii, wangetenda haki, amani haihubiriwi majukwaani ni tunda la haki na matumaini ya wananchi kwa viongozi wao," alisema.

Alisisitiza kuwa ni vigumu kwa viongozi kueleweka kuwa wana nia ya dhati kuona nchi ikitawalika kwa amani na utulivu, wakati wananchi wengi wanaendelea kutaabika kwa kunyimwa haki zao na kunyanyaswa ndani ya maeneo yao. "Nani hajui uvunjifu wa haki za wananchi unaofanyika katika ardhi, elimu, ajira na usalama wa raia?...haya yanafanywa chini ya serikali ya CCM ambayo inahubiri amani inaacha haki, hawa ni wanafiki ndiyo maana nchi inawashinda," alisema.

Dk. Slaa pia alisema CHADEMA inajisikia fahari kuona serikali ya sasa inatekeleza sera za chama hicho kikuu cha upinzani nchini chenye utajiri wa mawazo mbadala mbalimbali namna ya kuwatumikia Watanzania. Alisema wamefurahi kusikia serikali ina mpango wa kuongeza miaka ya wanafunzi kusoma elimu ya msingi kutoka miaka saba ya sasa hadi 10, ambayo ilikuwa sera ya CHADEMA siku nyingi na waliinadi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akadai kuwa kutokana na mawazo mgando ya chama kilichoko madarakani na viongozi serikalini, walimbeza.

"Tunashukuru wameanza kutekeleza sera zetu. Sisi hatuna kinyongo kama wanatumia sera zetu kuongoza nchi hii, kwa sababu hatimaye anayenufaika ni mwananchi na hiyo ndiyo furaha yetu. Lengo letu ni Watanzania hawa kunufaika na nchi yao," alisema.
Alibainisha kuwa mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu waliposema kuwa wakiichukua nchi wangetoa elimu bure walijua wangefanya nini lakini CCM kwa mawazo mgando walibeza kwa madai haiwezekani.

Aliongeza kuwa CHADEMA ilisema ikichukua nchi itaangalia na kurekebisha mfumo wa kodi na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ikiwemo mfuko wa saruji uwe sh 5,000.

Alisema chama chake kilitoa kauli hizo kwa kuwa kinaamini bati, nondo na vinginevyo kadhalika, vingeshuka bei. Alisisitiza kuwa ni suala la formula na mfumo wa ulipaji kodi na uzalishaji viwandani, hilo nalo walibeza na wakasema haiwezekani lakini sasa wanatekeleza.

Tanzania Daima

Kweli kabisa wala hajadanganya na kila mtanzania anajuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom