Siyo CCM au UKAWA ufisadi upo - SERA NA KATIBA Itajenga Tanzania Mpya

dkn

Senior Member
Oct 7, 2010
139
42
Katika tathmini yangu binafsi ninaona watanzania tunaendeshwa kwa siasa za ujanja ujanja na maneno yasiyo na msingi katika kampeni za uchaguzi.

Siasa zimekuwa ni ufisadi na kuchafuana kati ya wanasiasa hata kuingiliana kwa mambo binafsi. Tukianzia na ufisadi siyo CCM wala upinzani rushwa na ufisadi umekidhiri na hili jambo siyo la mtu mmoja;

Mfano hai kwa mgombea wa CCM: Amehusishwa na kununua nyumba za NHC kwa bei ya chini; huu ni ufisadi.
Suala la kuingiza taifa kulipa fidia kwa maamuzi mabaya sioni kama ni ufisadi (kulipia meli iliyokamatwa na samaki pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha, kukatiza mikataba ya makandarasi na baadaye kulipa fidia baada ya kushindwa kesi)..haya yote ni makosa ya taasisi na wizara husika na zaidi waziri anayetoa maamuzi kwenye media bila kuwa na ushahidi wa kutosha; hapa ni kosa la waziri na wizara yake na ndani kuna wengi wahusika moja kwa moja. Walipa kodi ndiyo tunaumia kulipia gharama za waziri kukaa hotelini kwa miaka kwasababu nyumba za serikali zimeuzwa.

Raisi Mkapa alinunua Kiwira kupitia njia za ujanja ujanja leo hii anakaa na kuita watanzania malofa. Sikatai yeye kununua Kiwira ila kama kweli si ufisadi ni kwanini kununua mali kwa bei ya chini na kutokuwa na ushidani wakati wa manunuzi.

Kesi ya Tanesco tumeshindwa na tutalipia fidia hayo ndiyo mambo ya msingi ambayo KATIBA ya “Warioba” imeanisha kuwe na chombo cha maamuzi na Raisi apunguziwe mamlaka…hapa ni kusema, Raisi hakupaswa kufanya maamuzi au kutoa mapendekezo kwa simu nini kifanyike…yeye siyo mtaalamu anatakiwa kushauriwa nini cha kufanya siyo kutoa maelekezo nini kifanyike bila kukaa chini na wataalamu na wanasheria.

Upinzani: Ufisadi upo, Sumaye kuuziwa ranchi siyo kosa lakini ni mchakato gani ulipita yeye kununua? Kama kitu kimewekwa bayana na maamuzi mabaya ya serikali kuuza ranchi au nyumba za NHC, angenunua mtu baki ambaye hayuko kwenye serikali tusingesema kitu ila kwa kuwa yeye ni kiongozi na ana haki kama mtanzania yoyote kununua; jambo la kwanza sisi wananchi tunaona ni ufisadi kwani maamuzi ya kuuza yanaweza kuwa yamewekwa ili viongozi wapate fursa ya kununua kwa bei ya chini na jambo la pili je kulikuwa na ushidani wakati wa manunuzi?
Mifano mingine ya upinzani ni pamoja na mwenyekiti wa Chadema kuhushishwa na ufisadi wa kuuzia chama chake magari kwa bei iliyo zaidi. Haya yote kuna maswali ya kuuliza je mchakato wa manunuzi ulifanyika?
Zitto kapigana vilivyo katuambia kuna hela za viongozi akaunti za nje, leo hii imeishia kuwa historia..hayo majina yako wapi na kiasi gani cha fedha wanacho? Kuwa na akaunti nje si dhambi lakini kwa upande mwingine badala ya kuweka fedha halali nchini kwako kujenga nchi yako kwa uwekezaji n.k. unaweka hela nje ya nchi lakini kikubwa zaidi hizo hela zimepatikana vipi? Leo wanasiasa wa upinzani akiwemo Zitto kimya, tunaweza kusema ni ufisadi kwa yeye kupewa rushwa kukaa kimya kama hatakuja mbele na ushahidi au kukanusha.

Unaona wanasiasa wanatudanganya eti wanakula mihogo na supu ya maharage? Vyote hivyo ni vyakula na kusema hivyo kujionyesha ni mtu wa maisha ya chini ameshindwa labda kupata chakula ambacho yeye anaona ni kwa ajili ya tabaka fulani huu ni uongo. Kwa hadhi ya mwanasiasa kama huyo toka kipindi akimtumikia Mungu hajawahi kukosa chakula anachoona ni bora kwa watanzania wote kwa kutumia sadaka za kanisa, michango mbali mbali sasa hivi kama mwanasiasa unatembelea gari la chama au gari lako binafsi kwa familia yako lita moja ya mafuta shilingi 2000; unalipwa mshahara unasema unaishi kwa kula mihogo na supu ya maharage huu ni upuuzi kuwaonyesha watanzania wewe ni mtu wa hali ya chini kabisa na haiingi akilini.
Wanasiasa kuanza kupanda daladala kuonyesha kuwa na wao pia wanatumia usafiri wa kero kama wananchi wengine, kwenda masokoni na kamera na waandishi kuonyesha na wao pia wanakula kama wananchi wa kawaida huu ni upuuzi kabisa. Angalia gharama za safari za Raisi au matibabu ya viongozi wa serikali, gharama zote zinabebwa na wananchi kupitia kodi na kungekuwa na busara sana hela hizi zingetumika kujenga mahospitali hapa nchini. Viongozi watumie akili na maarifa, nakubali Raisi kutibiwa nje ya nchi lakini kwa miaka 50 tumeshindwa kuwa na hospitali ya kutibu watu wetu basi Raisi awekewe budget ya bima ya matibabu kuliko kupanda ndege kila kukicha nje ya nchi na bado anaongozana na watu kadhaa na gharama za matibabu.

Mwisho uchaguzi wa sasa hivi ni sera na muhimu zaidi KATIBA (kama ni hiyo ya “Warioba”) itaweka bayana uwajibikaji. Unaona jambo la ukweli upinzani unakataa bungeni lakini chama tawala kinakubali kwa sababu tu ya wingi lakini kimsingi hata walio serikalini wako tayari kukataa lakini kwa kuwa kura ni wazi tunategemea nini. UKAWA wanataka katiba ya Warioba, CCM hawataki je ni nini hiki ambacho CCM wanaogopa na UKAWA hawaogopi…na ikitokea kuwa upinzani umeshinda CCM watabaki na msimamo wao au watabadilika kwakuwa itakuwa haiwapi nafasi wao.

SERA na KATIBA ya “Warioba” itawezesha Tanzania kuwa imara bila kujali ni chama gani kitashika dola tarehe 25 Oktoba 2015.
 
Back
Top Bottom