Siumii kukosa ajira ila napata 'stress' kutoka kwa wanaosubiri niajiriwe

momara

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
463
491
Napigiwa simu naulizwa Kwanini sijaajiriwa.

Mbona Mwenzako hapa amepata we hujapata.

Ndugu zangu wananiona mzembe kwa kukosa ajira. Wanaamini kuna sehemu nakosea, wanaamini mimi mjuaji kila wakiniuliza kuhusu ajira natoa maelezo mengi wakati wenzangu wanaajiriwa.

Wananiambia nimeganda mjini kwenye wasomi wengi na ndomana sijaajiriwa wakati mwenzangu aliepata kaomba ajira akiwa kijijini.

Sichukii mwenzangu kuajiriwa ila amefanya niulizwa maswali ambayo binafsi yananifanya nijiskie vibaya.

Nimepata mawazo sana wakati jambo hili binafsi nlishalimaliza tangu zamani na nimesimama mwenyewe na tayari najitegemea.

Imefika muda siumii kukosa ajira ila napata stress kutoka kwa wanaosubiri niajiriwe.

Mtu ambaye hajaenda hata shule ya upili anakufundisha kuhusu ajira na usipofuata au kutekeleza yeye anaona ndo sababu ya wewe kukosa ajira.

Nashindwa hata kuandika. Kwaherini
 
Da Umesema kwel. Unajua Sis wenyew tuliokaa darasan tunajua hali ilivyo Kwa sasa na tumekubaliana nayo tunasonga mbele asa asa mwngn anakupa stress zisizo na maana na shule hana
Yani aliyefeli hata form four anananga msomi na hajui lengo la elimu ni kutoa ujinga na hayo mengine yanafuata, haelewi mazingira ya uchumi na Hali iliolvo ya uwekezaji yeye ni kuponda wasomi eti walipoteza muda utafikiri yeye ambaye hakusoma ni bilionea. Imagine watu ka ma engineer, ma Dr wasingeenda shule, in short jamii iache kuwapa stress graduate, badala yao wawa support na waache unyanyapaa.
 
Da Umesema kwel. Unajua Sis wenyew tuliokaa darasan tunajua hali ilivyo Kwa sasa na tumekubaliana nayo tunasonga mbele asa asa mwngn anakupa stress zisizo na maana na shule hana
Pole sana ndugu, ndio familia zetu zilivyo ila vumilia tu hayo yote yatapita itabaki historia tu.
 
Back
Top Bottom