Sitta na mwakyembe wawe realistic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta na mwakyembe wawe realistic

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KASIGAZI, May 26, 2011.

 1. K

  KASIGAZI Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sitta na Mwakyembe wamejitwalia umaarufu kwa muda mrefu kama makamanda wa kupinga ufisadi ndani ya chama cha majoka. Lakini ufisadi ktk ccm ni namna tu ya kawaida ya kutenda kazi...ni mfumo ambao hakuna jinsi ya kujitenga nao ukiwa ndani. Sasa ni kweli hawa jamaa hawajui kwamba huwezi kusukuma gari ukiwa ndani yake, au wanajificha humo ili kulinda ulaji wao? Kweli mtu mzalendo mwenye uchungu na taifa hili anaweza kuendelea kukaa katika chama hiki? Sitta alisema juzi kwamba inamgharimu kushikilia misingi ya baba wa taifa ndani ya chama chake,lakini hawezi kutoka hadi kieleweke; kwani baba wa taifa aliweka misingi hiyo kwa chama au kwa taifa zima? Kwani kushiikilia misingi hiyo ni lazima uwe ndani ya ccm? Nachelea kwamba hawa wazee wamepoteza hadhi yao ya uadilifu wa dhati.
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mpendazoe alisema ukweli kuwa Sitta na Mwakyembe ni wanafiki wanaofikiria matumbo yao kwanza na si uzalendo wanaotaka watu waamini. Mwalimu mwenyewe alishatamka hadharani kuwa ccm [chama alichokiasisi yeye mwenyewe] hakikuwa MAMA yake na angeweza kukihama wakati wowote kama kingeendelea kukiuka misingi iliyojiwekea!! Sasa ccm ya leo imekiuka misingi ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na kimekuwa chama cha wafanyabiashara mafisadi; kama ni hivyo Sitta na Mwakyembe wanangojea nini kukihama kama sio ubinafsi? Sasa hawa jamaa ndio wameonesha true colours zao kuwa kumbe yale makelele yote yalikuwa kutafuta ulaji tu!!
   
 3. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kwa ujumla watanzania walio katika uongozi wa kisiasa katika Chama Cha Mapinduzi ni watu ambao kufika kwao katika nafasi za uongozi ni kwa bahati na sio kwasababu za kimantiki ya sifa za uongozi. Kuna wale walioibukia kutoka vijijini kwakua ndio walioonekana kwamba wamesoma miongoni wa watu wa eneo husika na kuna wale waliovutwa na viongozi wenzao hasa Mwalimu Mwenyewe. Hii imekua ni sababu ya kuwa na watu ambao ni vigumu hata kuelewa ni kwa sifa zipi wamefikia kupewa mamlaka walizonazo. Kuna ambao hata watu wao wa karibu wanashangaa imekuaje. Siku hizi watu wengi wanaposhindwa kabisa kuona sifa za Uongozi wanaishia kusema "huyu ni Usalama wa taifa". Ingawa viongozi wengi ni miongoni mwa maofisa wa idara hiyo ya serikali lakini imetumika pia kuficha udhaifu dhahiri anaouonyesha kiongozi. Kufupisha yote hayo na kwa masikitiko Tanzania ni moja ya nchi chache ambapo kiongozi anapewa nafasi hiyo bila kuwa na sifa hata moja ya kuongoza na matokeo ni hali tuliyonayo. Viongozi hawawezi kusimama hadharani kutetea wanachoamini na kila wanachosema "wamedesa". Ni vigumu kuelewa Sita na Mwakyembe kama wanasukumwa na wanachoamini au ubinafsi kama ilivyo kwa viongozi wengi.
   
 4. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Time will tell..... wanafiki njia yao siku zote huwa fupi, wataumbuka tu. Vita ya madaraka imetuonyesha who is who!
   
Loading...