Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 26,634
- 38,245
Mpaka sasa nina hakika ukimuuliza Mwafrika yeyote kama amepata faida gani kwa uwepo wa rais Mwafrika huko Marekani atasema hakuna!
Nakumbuka kipindi Obama anaingia madarakani Waafrika wengi hasa ndugu zetu Wakenya, walifurahi sana, wakiamini kwamba sasa neema tele zitawafikia kutoka kwa Obama kutona na Ukenya/Uafrika wake.
Lakini sasa kiko wapi? Obama karibu anaondoka madarakani lakini hata ziara tu hajafanya huko Kenya. Kwa wenye akili walijua tu kwamba anaeongoza Marekani sio Obama peke yake, bali kuna na watu wengi ambao pia wanamcontrol hata Obama mwenyewe!
Hali hii na ifananisha na hapa kwetu, alipochaguliwa mzee Sitta kuwa mwenyekiti wa bunge la katiba, watu wengi walishangilia sana wakisema sasa bunge maalumu limepata dereva sahihi! Lakini sasa kiko wapi?
Kwa wenye akili walijua tu kwamba Sitta atapaswa kuongoza bunge kutokana na matakwa ya wenye chama!! Na hivyo siyo Sitta tu anaeongoza bunge, bali kuna na wengine pia ambao wana m-contol hata yeye mwenyewe!
Hili lilikuwa bunge la kung'oa, kuharibu, kuvunjavunja na kuchoma mifumo dharimu ya kiutawala, na maadamu Sitta ni miongoni mwao hangeweza katu kujikaanga mwenyewe na chama lake!
Sasa matumaini tena hakuna watanzania tungojee mtu sahihi atakae kuja na nia ya dhati ya kutupatia katiba, CCM wameshindwa!