Pamoja na kukubaliana nawe kuwa haikustahili kwa Jaji Mkuu kutumia njia aliyotumia lakini tunavyoelewa kuwa uongozi ni busara na sio jazba na kejeli.
Sawa Spika amemkejeli Jaji Mkuu kwa kutekeleza yale ambayo yeye Sitta na Wenzake wameyatunga na kuyakabidhi kwa Jaji mkuu ayatekeleze nani mkosa hapa. Huyu alieyetekeleza yale aliyoambiwa ayatekeleze au yule aliyoyatunga na kuamrisha yatekelezwe?
Aidha ubabe ndio kigezo cha uongozi? Sitta anakurupika kwa ubabe huku tukijuwa kuwa huyu Bwana ndiye mwenye wajibu wa kututungia sheria zitakazotulinda sisi hana uwezo wa kurekebisha makosa anapokumbushwa,sasa wananchi tukimbilie wapi?
Ninachoona mimi ni kuwa huyu Mzee sasa anaelekea katika udikteta na kujichukulia maamuzi mikonono mwake. Tuangalie mifano kule Zanzibar Wajumbe wa Baraza kutoka upinzani kila wanapofukuzwa Barazani hukimbilia mahakamani na juu ya siasa za kule hawa wajumbe hushinda na Spika hutekeleza maagizo ya mahakama. Sitta hakuwa na haja ya kutumia lugha ya kejeli kwani kwa upande mmoja yeye ana uwezo wa kuzuia au kurekebisha hayo anayoona kuwa ni mapungufu kwa kufuata SHERIA NA KATIBA au anataka tuelewe kwa vile yeye ni kiongozi wa kutunga sheria basi habanwi na sheria? Do we need to read between the lines ili kufahamu nini Jaji Mkuu anakisema?
Ni uozo mtupu, lakini bora bunge - humo kuna baadhi ya watu makini.
Akitoa taarifa hiyo bungeni leo mjini hapa, Sitta alionyesha kulaumu baadhi ya uamuzi ambao umekuwa ukitolewa na mahakama na kusema kwamba unatoa fursa kwa mtu mmoja kuliko jamii nzima, jambo linaloumiza.
Ndugu yangu Ngekewa. Mambo mengi yanayofanyika hapa nchini yanahitaji kujitolea zaidi. Kauli ya kejeli iliyotolewa na Speaker wa BUnge sijaiona. Kama kauli ya "Na hapa watasema naingilia Mahakama, Potelea mbali" ndio kauli ya kejeli, basi nadhani kejeli inabadilika maana. Maana nijuavyo mimi maneno hayo si kejeli bali ni sawa na kusema "Basi acha wachukulie hivyo".
Ndugu yangu, sheria ingekuwa inafuatwa vizuri (inavyotakiwa), malumbano kama haya yasingekuwa na nafasi. Ni kweli kabisa kuwa sheria zinaanza kutozingatia maana ya kuundwa kwake. Inawezekanaje sheria iwe na manufaa kwa mtu mmoja mmoja bila kujali haki sawa kwa wengine (ambao wanaweza kuwa wengi) na mtu atakaelizungumzia hilo aonekane anaingilia mamlaka ya Mahakama? Uingiliaji gani huo wa mamlaka ambao umefanyika baada ya mahakama kuamua? Nadhani uingiliaji ungekuwa wakati/kabla ya mahakama kufanya maamuzi, tungeweza kusema mahakama imeingiliwa na kuwa na haki ya kulaumu uingiliaji huo. Ila kama Mahakama inaelekea kufanya maamuzi yasiyo na mantiki yoyote (yasiyo make any sense) sidhani kama huo ni uingiliaji wa mahakama zaidi ya kulaumu utendaje wake. Mahakama ni zetu kama zilivyo kwa Majaji na Mahakimu wengine. Tunayo haki (na hasa kwa kupitia Bunge letu) kulalamika tunapoona kuwa haki iliyotarajiwa kutolewa na mahakama zetu inatolewa visivyo na hata kusifia endapo tunaona haki inatolewa ipasavyo. Tusizoee kusifiwa tu, tukubali kukosolewa ili tuwe bora zaidi. Majai wanaanza kuelekea kufikiri kuwa Mahakama ni mali yao binafsi. Inawezekanaje kuwa hivyo?
Katika hii mihimili mitatu, "unaoongoza kwa ufisadi na watendaji wake kuona mali za wananchi hazina mwenyewe na kuzifuja kama mchwa" ni Serikali(Executive branch), "unaoongoza kwa Rushwa za kubaka haki za raia" ni Mahakama na "Unaoongoza kwa uzembe na ubendera fuata upepo bora liende sisi tupate posho" ni Bunge
Sasa hapa ni kwamba mihimili yote au system nzima ni uozo yaani mfu hawezi kulala tanga la mfu mwenzake.
Jaji Mkuu alieleza hayo kwa kutoa mifano, ikiwamo ya Bunge kusikiliza shauri la Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima na suala la Sitta kuzungumzia uamuzi wa Mahakama juu ya shauri la vituo vya mafuta mkoani Morogoro.
Kwenye kesi ya Dambo la takataka vingunguti ambalo wananchi waliomba liondolewe sababu wataalamu wa mazingira walisema linalleta magonjwa na uchafu wa kuua afya za watu.
Serikali ilikata rufaa ikapeleka kesi kupinga mahakamani dampo kuondolewa.Mheshimiwa Jaji aliyesoma sheria akazielewa barabara na namna ya kuzitumia kwa maslahi ya wananchi alisema kuwa anashangaa kuona serikali inakata rufaa kuua wananchi wake kwa uchafu wa lile dampo.Akaamuru Dampo lifungwe mara moja na lihame Vingunguti ili wananchi wasife kwa uchafu wa hilo Dampo.
Sasa simwelewi Jaji mkuu anaongea nini? EWURA ambao ni wataalamu waliobobea kwenye mambo ya mafuta walisema vituo vya mafuta vilikuwa vikiuza mafuta machafu yasiyofaa ambayo yanaua uhai wa magari ya watanzania hivyo vifungwe.Baada ya kuamuru vile na kuvifunga wenye vituo wakakimbilia mahakamani kukata rufaa waendelee kuua uhai wa magari ya watanzania kwa kuendelea kuuza mafuta machafu ya vituo vyao vilivyofungwa.
Kesi ilipofika mahakamani mahalkama ikatoa ruksa vituo vifunguliwe waendelee kuuza hayo mafuta yao machafu yauayo magari .Spika kweli kwa hasira akaijia juu mahakama na kuambia inatoa maamuzi ya ajabu ajabu.Jaji mkuu anasema haikutoa maamuzi ya ajabu mhhhhhhhhhhhh!!!!!!!?
Matarajio ya Bunge na wananchi ni kuwa mahakama ingetoa uamuzi kama ule wa Dampo la VINGUNGUTI na si vinginevyo.Lakini sababu mahakama ilitoa uamuzi tofauti na ule wa Dampo la vingunguti na mimi naungana na sita na kutamka wazi kuwa uamuzi ule ulikuwa wa ajabu.Na kama naonekana naingilia mahakama na mimi namcharukia jaji mkuu na kusema POTELEA MBALI.
SPIKA SAMWELI SITTA I SALUTE YOU.Nakuelewa unachoongea kuliko alichoongea jaji mkuu.Ukimwona msalimie mwambie wananchi hatumwelewi alichoongea.Na huyo jaji aliyetoa uamuzi wa vituo vyenye mafuta machafu aliyesema vifunguliwe naomba itakapofikia kupandishwa cheo wananchi tuulizwe kama tunakubali au tunapinga kupandishwa kwake ikiwezekana.
Alichofanya Jaji Mkuu ni sahihi.
...............Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania, Ijumaa iliyopita, Jaji Mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhani alieleza kuingiliwa kwa chombo hicho cha kutoa haki na mihimili mingine miwili, yaani Serikali na Bunge.
Jaji Mkuu alieleza hayo kwa kutoa mifano, ikiwamo ya Bunge kusikiliza shauri la Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima na suala la Sitta kuzungumzia uamuzi wa Mahakama juu ya shauri la vituo vya mafuta mkoani Morogoro.
Jaji Mkuu pia alisema serikali imewahi kuingilia uhuru wa mahakama. Lakini pengine kwa kuwa muungwana, Jaji Mkuu alishauri siku moja mihimili hiyo mitatu ikae pamoja na kuzungumza faragha kwa nia ya kuleta mkabala murua baina yao. Bila shaka, huu ulikuwa ushauri wa busara na wa bure....................
Mwaka 1951, katika mji wa Toeka, Kansas Linda Brown aliongozana na baba yake Oliver L Brown kwenda kujiandikishwa katika shule ya jirani ambako watoto wenzake walikuwa wanasoma. Maombi yake yalikataliwa kwa vile yeye alikuwa mweusi na ile shule ilikuwa ya watu weupe. Baba yake, Oliver, akajiunga na wazazi wenzake weusi 12 ambao nao watoto wao walikataliwa kujiunga na shule za watu weupe, kuifungulia mashtaka Bodi ya Education ya Topeka kupinga kanuni zake za ubaguzi katika masuala ya elimu. Kesi hiyo iliitwa Brown v Board of Education of Topeka na ilisimamiwa na wakili mweusi aliyeitwa Thurgood Marshall. Kesi ilienda mpaka Supreme Court ya Marekani. Uamuzi wa Mahakama Kuu ulikuwa ni dhana ya separate but equal ilipingana na Katiba kwa sababu haiwezekani usawa ukapatikana chini ya dhana hii. Uamuzi huu ndiyo ulioashiria mwisho wa ubaguzi wa rangi katika elimu Marekani kote. Mwaka 1955 Dada Rosa Parks alipokataa kumpisha mtu mweupe akae kwenye kiti chake, uamuzi huu, ulichangia katika kumaliza ubaguzi wa rangi katika mabasi ya umma.
Mwaka 1970, Norma L McCorvey ("Jane Roe") alifungua kesi dhidi ya Henry Wade aliyekuwa Distict Attorney wa Dallas County, Texas. Kesi ilihusu haki ya Norma ku'abort' mtoto wake na ilijulikana kama Roe v Wade. Mwaka 1973, Mahakama Kuu ( Supreme Court) ya Marekani iliamua kuwa sheria nyingi za marekani zinazomzuia mwanamke ku'abort' mimba yake zilipingana na haki yake ya chini ya Katiba ya Marekani. Uamuzi huu ndiyo ulio legalize abortion marekani.
Mifano kama hii iko mingi. Hivi karibuni, ni Mahakama Kuu hiyo hiyo iliyoamua kuwa kumnyonga mtoto ni kinyume na Katiba ya Marekani. Ninachotaka kusema kusema kuwa mara nyingi haki ( justice) kwa mwananchi inapatikana mahakamani na sio kwenye bunge. Bunge lingeachiwa, pengine ubaguzi wa rangi ungeendelea kwa muda mrefu marekani kwa sababu wabunge wengi walikuwa weupe na wengi wao wabaguzi. Wabunge hawa waliwakilisha majimbo ambayo majority ya wapiga kura walikuwa wabaguzi. Hawa kama walitaka kuendelea na ubunge wao bila shaka walitakiwa kutetea fikra na imani ya wapiga kura zao. Mahakama Kuu ni tofauti. Wao hawajibiki kwa yeyote kwa hiyo wanachoangalia ni haki basi. Hawatoi uamuzi kwa vile utawafanya kuwa popular au kulinda maslahi yao. Ndiyo maana hata kwetu, ni vigumu sana kwa hata Rais kumfukuza kazi jaji.
Kitu kingine cha msingi ni kuwa Mahakama Kuu inatoa uamuzi wao kutokana na kesi iliyo mbele yao. Mahakama haiwezi kama ilivyopendekezwa na wengine kumfungulia mashtaka Spika. Lakini ni Mahakama hii iliyotoa uamuzi kupinga fee za juu mno zilizowekwa kwa wale waliotaka kupinga matokeo ya uchaguzi. Mahakama iliamua kuwa fee hizi ziliendana kinyume na haki ya mwananchi chini ya katiba ya nchi yake. Ni Mahakama hii hii ndiyo iliyotoa uamuzi kusema kuwa ni haki ya mwananchi kugombea ubunge bila kuwakilisha chama chochote cha siasa (independent candidate). Uamuzi ambao serikali unautilia mikwala mpaka leo. Maamuzi haya yalitokana na kesi zilizopelekwa na wananchi wenye uchungu. Hivi kuna mtu anayeamini kuwa maamuzi kama haya yangeweza kupatikana katika bunge letu la sasa?
Kabla ya kumtupia lawama ni lazima tujiulize ni wangapi katika sisi ambao tumewapelekea kesi ambazo zilipinga sheria za kigandamizi? Si ni wakina Mtikila peke yao wenye ujasiri huo? Na hata akifanya hivyo, wengi wetu tunamuona chizi.
Tofauti na Spika, Jaji Mkuu hana jukwaa formal la kusemea yale aliyoyasema. Hawezi kuamka katikati ya kesi na kutoa malalamiko yake. Alichofanya ni kututetea sisi na kutukumbusha kuwa kuna njia mbadala ya kudai haki zetu za kikatiba. Sasa kwa kufanya hivi, tunambeza kweli? Kweli hatujipendi.
Amandla........
Ndugu yangu Fundi Mchundo, uliyoyasema hapo juu ni sahihi kabisa. Ila naomba nitofautiane na wewe kidogo, hasa katika maneno yako niliyoyawekea 'Bold" hapo juu.
Ni kweli kwamba Mahakama ilitoa uamuzi kusema kuwa ni haki ya mwananchi kugombea ubunge bila kuwakilisha chama chochote cha siasa (independent candidate). Katika maelezo yako ya awali, umezungumzia Mahakama za Marekani zilivyofuata Katiba ya nchi katika kutoa maamuzi. Vile vile Katiba yetu inatamka wazi kuwa mtu yeyote atakaeomba kuchaguliwa katika nafasi ya Rais na Ubunge, atatoka katika chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria. Je, huoni kuwa mahakama ilitakiwa kufuata Katiba yetu katika kutoa maamuzi?
.
Mheshimiwa Recta huo ni mfano mwingine wa mahakama zetu kutoa maamuzi ya ajabu ajabu.Ndiyo maana hata serikali haitaki kuyatekeleza sababu inayaona ni maamuzi ya ajabu ya kipuuzi ambayo hayaangalii kwa upana katiba.Mtu kaangalia kipengele kimoja tu cha katiba huyo akaibuka na hukumu.Tena hakuwa mmoja lilikuwa jopo la majaji.
Nadhani majaji wapandishwe vyeo kwa kuangalia maamuzi yao katika kesi mbalimbali badala ya kuangalia idadi ya miaka waliyokaa wakiwa wamevaa majoho kwenye viti vya hukumu za ajabu ajabu kama hizo.
Sasa serikali ikimcharukia jaji mkuu ikisema uamuzi huo wa mahakama uliotolewa na huyo jaji wa kuruhusu wagombea binafsi ulikuwa wa ajabu ajabu kwa kuwa ulikiuka katiba inayotaka watu wagombee kupitia vyama itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama?
Nafikiri jaji mkuu na majaji wenzie inabidi waanze kututhibitishia wananchi kuwa kweli wao ni learned brothers and sisters vinginevyo tutaendelea kuwacharukia bila chembe ya huruma wala lugha nyepesi za kidiplomasia ambazo wangependa Spika azitumie anapowasema wakikosea.
Huu si uamuzi wa ajabu ajabu. Katiba zote haziko perfect lakini katika kila Katiba kuna kile kinachoitwa haki ya msingi. Ni wajibu wa Mahakama kuitafsiri wakiangalia haki kwa raia wote wa JMT. Vipengele vinapopingana basi wanatoa tafsiri yao ya kipi ndio kipewe kipaumbele. Kwenye hii ishu Mahakama ilikuwa inaangalia haki ya msingi ya raia wa Tanzania kugombea nafasi yeyote anayotaka. Hiki kipengele kinazuia hiyo. Kwa hali hiyo maamuzi ya Mahakama yalikuwa yanamaanisha kuwa hiki kipengele kinafunikwa na hiyo haki ya msingi. Hiki kipengele kiliwekwa ili kulinda maslahi ya sehemu ya jamii na si jamii yote. Sasa kilichotakiwa ni serikali kukata rufaa na kusema kuwa hiki hakipingani na haki ya msingi ya raia wa JMT. Mbona wanasita kufanya hivyo?
Amandla.....