Sitosahau siku mchepuko uliponiachia mtoto kwenye daladala (Story Na Pongwer Mastory)

pongwer

Senior Member
Mar 19, 2015
174
26
((( SITOSAHAU ))))
SIKU MCHEPUKO" ULIPONIACHIA MTOTO KWENYE DALADALA.
soma story hii.

Mke wangu MARY aliamka mapema na kuniomba niende nikamsaidie badhi ya majukumu sokoni, kwani yeye siku hiyo alikuwa akijisikia vibaya, Hakukuwa na wakumtuma kwani tangu Tuoane tuliishi sisi Wawili hatukubahatika kumpata MTOTO KWA MIAKA ZAIDI YA MI TANO YA NDOA YETU".
Nikaenda mpaka kituo cha DALADALA ingawa nilikuwa na mawazo mengi sasa" kutokana na badhi ya mambo yangu kuenda ndivyo sivyo.

Nikiwa kiwa katika DIMBWI LA MAWAZO daladala iko kituo cha mbele mara MAMA MMOJA akiwa na MTOTO MCHANGA akaniita dirishani na kuniomba NIM'BEBEE MTOTO kwani daladala ilijaa naye alihitaji kupanda.
Nilimpokea mtoto na baada ya hapo nikamwona akizinguka upande wa pili apande, nami nikaendelea kuwaza lakini safari hii nikasali kimoyomoyo kuwa MUNGU Anipe nami Baraka ya mke wangu kuzaa.

Mawazo mchanganyiko yaliendelea kwa muda mpaka nilipokuja kugundua kuwa Daladala ndio inaingia kituo cha mwisho.
Nikakaa pale kusubiri watu washuke ili nimkabazi mtoto yule kwa mama yake lakini CHA KUSHANGAZA ni kwamba kila MTU ALISHUKA NA KUJIKUTA NIPO MIMI NA KONDA TWAANGALIANA.
Nikamuuliza mama wa mtoto yuko wapi?
Akadai yeye hajuwi wala hakuona mama mwenye mtoto.....

Nikamhadithia jinsi ilivyo akaniambia MJOMBA HAPO NENDA POLISI TU.
Nikaenda polisi na kutoa maelekezo nikiwa na konda pamoja na mtoto yule. Baada ya maelezo wakanambia sasa wewe baki na mtoto na sisi tunaendelea na UPELELEZI".
Nikaahirisha kufanya yale niliyodhamiria na kurudi nyumbani MKE WANGU ALINISHANGAA!!!! na hata nilipojaribu kuelezea hakunielewa zaidi ya kudai MTOTO YULE LAZIMA AWE NA MAHUSIANO NAMI"
akazidi kusema kuwa lazima NIMEZAA NA MTU NA KANISUSIA BAADA YA KUTOMJALI AU ANATAKA NIOANE NAE AU MAMBO MENGINE AMBAYO YAWEZEKANA KUWA SIRI ZA MIMI NA HUYO MAMA YAKE.
Na mke wangu alikasirika aliondoka na kwenda kwao.
Ikanilazimu niende kituo cha kulelea WATOTO YATIMA nilichoambiwa kiko pale mtaani kwetu, na baada ya kufika pale na kutoa maelezo wakakubali na kumchukuwa mtoto jambo lililofanyika ndani ya siku nne maana ilinibidi niende pia na polisi wathibitishe.

Baada ya hapo nikaanza safari ya kwenda kijijini kwa mke wangu mary, kufika kule BABA NA MAMA wa mke wangu wakadai kuwa kwa UNYAMA NILIOMFANYIA MWANAWAO HAWATANIRUHUSU NIRUDI NAE TENA NA SASA WATAMRUHUSU AOLEWE NA MTU MUNGINE.

Nililia kama mtoto mdogo nikiomba WANISAMEHE NA HAWAKUNIELEWA, Kwani mkasa huu hata mimi wanipa wakati mgumu lakini hawakuelewa.
Nikakumbuka sisi Kwa KABILA LETU tukiwa tunahasira tuna asili moja ya KUJINYONGA".

Jioni ile nikanunua kamba yangu na nilipohakikisha kila mtu kalala, nikapanda juu ya mti kamba yangu shingoni na kisha kujitupa chini ili kama ile ininyonge...
Nilitapatapa pale na taratibu nikahisi haja kubwa ikinitoka kwa shida ikiashiria ndio nilikuwa NAKATA ROHO NIKALIA KILIO CHANGU CHA MWISHO KWA UCHUNGU" kabla kunaswa kibao na DEMU niliyelala naye GUEST BUBU huku akinisema" MWANAUME hauna haya wewe mimi nakuangalia hapa warusha rusha miguu na kujifanya unalia kumbe UNAKUNYA KITANDANI??
Mwanaharamu mkubwa wewee!!!!

Ha ha ha ha ndoto nyingine buana laana tupu.
 
pongwer naona umekuja kwa kasi ya magu kwenye mastori kuwashika wana jf
 
Last edited by a moderator:
pongwer naona umekuja kwa kasi ya magu kwenye mastori kuwashika wana jf

ha ha ha ha unajua nlkuw insta ila now ac yng nailekebxha but hpa nlkuw na ac ya JF ktambo ila nlkuw mviv
 
Last edited by a moderator:
INSHU YA DR MWAKA ILIPANGWA

Hivi karibuni mdada machachari anayejulikana kwa kutukana watu bila uoga akijivunia kutoishi Tanzania hivyo mkono wa dora hauwez kumkamata na ambaye alikuja ili agombee ubunge akaishia polisi Mange Kimambi aliibuka na kuanza kumsakama dr Mwaka kuwa ni daktari feki na amekuwa akiwafanyia vitu vya ajabu akina mama.
Iliniumiza akili kumuwazia Mwaka kwa sababu nina ndugu yangu aliyepata tiba kwa huyu jamaa na akapona tatizo lake na leo ana mtoto na furaha maishani mwake.
Nikajiuliza hivi kama kuna watu walifanyiwa vitendo visivyofaa mbona hawajawah toka hadharani? Basi hata huyo Mange mbona hakuweka ushahidi juu ya hao watu zaidi ya porojo?
Nikajiuliza tena! Hivi kila sehemu ya tiba mfano Muhimbili kila anayeenda kupata tiba anapona? Iweje kwa Mwaka waseme kuna wasiopona? Inamaana walitaka wote walioenda pale wapone? mpaka wale waliotoa mimba na kuharibu vizazi?
Wakageuka na kusema anajifanya daktari wa kisasa wakati ana kibali cha mitishamba! Nikajiuliza kuna mtu alishapewa dawa za hospital kule kwa ? Mwaka? Mbona wote wanaoenda pale wanapewa mitishamba na matunda pekee?
Wakauliza amesomea wapi udaktari hivi kumbe uganga wa mitishamba unasomewa? Chuo gani hapa Tanzania na mimi niende??
Nilipata walakini lakini baada ya mishemishe za kutwa tangu Mwaka aumbuliwe kule Insta kama wanavyodai kuna mtu mpya kaibuliwa na anapewa promo sana anaitwa Fadhageti! Kwa sasa ukienda kila page ya superstar utakuta kampost huyo jamaa tena kwa advetise nyingi kuwa anatibu matatizo ya uzazi na sio tapeli na kumpamba kibao.
Jana usiku Mange naye akampost kwa sekunde chache ila watu walipomshambulia akatoa!
Baada ya kuunganisha hayo yote nikagundua kuwa kuna mchezo unaendelea chini kwa chini tena watu wakiwa wamelipwa pesa ya kutosha(mange) na mheshimiwa mmoja ili tu wamshushe Mwaka na kumpandisha jamaa mwingine baada ya kuona Mwaka anakuwa tishio kwa matabibu wenzake wa tiba za asili!
Naamin hamtaweza kwa sababu waliowahi kupata tiba kutoka kwa Mwaka na kupona ni wengi na wanashuhuda zao!!
Sinema bado inaendelea subirini tuone mwisho wake

Junior
Insta USHAURI_mahusiano
 
mbna unachangany madawa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom