Sitofahamu yaibuka! kijana adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana tangu Mei 19 mwaka huu Kibaha

Sitofahamu yaibuka! kijana adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana tangu Mei 19 mwaka huu Kibaha

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kijana Hussein Abdallah Mkwame (26) mkazi wa eneo la Ungindoni -Kongowe, wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani kwa takribani miezi miwili (2) sasa hajulikani alipo baada ya watu wasiojulikana kumkamata na kuondokanae tangu Mei 19 mwaka huu

Mzee Abdallah Omary Mkwame mkazi wa Buza, Dar es Salaam ambaye ni Baba mzazi wa kijana huyo ameieleza Jambo TV kuwa familia, ndugu, jamaa na marafiki baada ya kupata taarifa hiyo wamechukua juhudi za makusudi kumtafuta kijana wao kwenye vituo mbalimbali vya Polisi, Hospitali (Wodini na Mochwari) za Kibaha lakini hadi sasa hawajamuona, na hakuna taarifa zozote kumuhusu

Amesema baada ya kupata taarifa hiyo, mwanzo kabisa alifika eneo la tukio na kwamba baadhi ya mashuhuda aliowakuta wakati huo walidai kuwa kijana huyo amekamatwa na askari Mgambo waliokuwa wameambatana na maafisa wa Polisi kutoka Kituo kidogo cha Polisi Kongowe wakiongozwa na Mkuu wa Kituo hicho, ambapo katika ufuatiliaji wake Polisi wamekanusha kuhusika na suala hilo,

 
Back
Top Bottom