Habari zenu
Nina mchumba wangu, tumekua na mahusiano muda mrefu sana, sasa imefikia muda nimeona bora nimsogeze niishi nae kabisa, sasa tatizo mimi ni mpagani(sina dini) na huyu mwenzangu kwao wamesema wanataka ndoa ya kidini, yeye yuko tayari tuishi nae ninavyotaka mimi, ila ndugu zake ndio mbogo, hawataki kusikia suala la bomani.
Tafadhali, nashindwa nifanyaje, coz mwanzoni nimewaza niuze kila kitu na biashara zangu nifunge, nitoroke nae mikoani, ila naona hataki hicho kitu. Naombeni mbinu tafadhali.