Sitaisahau siku ya Jana

enjai ya kyasha

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2017
Posts
3,109
Reaction score
3,677
*SITAISAHAU SIKU YA JANA*

Wahenga walisema kuishi kwingi kuona mengi, basi nami nimeona na kufanya mengi ila Jana ilikuwa kiboko. Asubuhi mida ya SAA 3 niliamshwa na meseji za WhatsApp nikaanza kuzipitia moja baada ya nyingine mara ghafla nikakutana na SMS murua na pendwa sana (kuhusu boom kutoka kufikia mchana).

Basi nikaamka nikapiga mswaki huku nikiwaza niende wapi kupata moja moto moja baridi huku nausubiria mpunga wangu. Ndipo akili ikanituma niende glossary moja matata manake hapo kuna mrembo mkali nikiwa nashusha huwa naenjoy sana pale nishushapo funda la bia huku macho yakimwangalia aisee huwa napata raha sana.

Basi nikatembea inkafika kwa mbwembwe nikaagiza supu ya samaki kwanza (ili kuweka protection layer tumboni) baada ya supu nikaangalia saa yangu nikaona yamebaki masaa mawili mchana ufike, ndipo nikamuita waitress kwa mbwembwe zote nikaagiza castle nikaanza kushusha huku napiga stories na mrembo huyo ikawa ni mwendo wa kuzifungua tu bia huku nkitupia jicho kwenye saa yangu iliyoomesha zimebaki dakika 5 mda ufike, basi nkaona isiwe tabu nkaagiza ugali mkubwa na nyama nkala.

Hofu ilianza kutanda moyoni Mara baada ya kuona meseji kwamba mkwanja umeota mbawa mpaka Jtatu, hapo nkajua nimekamatika sina ujanja hadi nikaanza kuhisi tumbo la kuhara. Hali ilikuwa tete mhudumu aliposema nimlipe maana anataka kukabidhi hesabu maana amemaliza zamu.

Nilikosa la kumjibu nikaamua kumwambia nitamlipa meneja lakini aligoma kata kata ndipo ukazuka ubishi mkubwa ambao ulipelekea Meneja wa bar aje mahali hapo. Baada ya kuja na kuambiwa mkasa mzima ndipo nikaamuliwa nilipe la sivyo nitakiona cha moto.

Huku nikiendelea kutoa utetezi usioeleweka nilishitukia buti zito lilioambatana na mtama mkali kutoka kwa mlinzi wa pale bar, nilianguka "pwuuuui" ka furushi la viazi, nikaulizwa tena unalipa ama hulipi?...kabla sijajibu nikatiwa makofi mawili ya uso nikaanza kuona nyota nyota, baada ya kipigo kizito kutoka kwa mlinzi huyo aliyetukuka kwa sifa nikaamuliwa nideki vyoo vyote vya pale bar.

Wakuu nilianza kazi mara moja huku naugulia maumivu makali na maneno ya masimango kutoka kwa mhudumu mrembo. Baada ya kukamilisha adhabu nikaamuliwa nipotee pande hizo huku nikisindikizwa na buti la mgongoni. Niliondoka kwa fedheha huku nikiugulia maumivu makali mno. Mpaka naandika ujumbe huu nasikia joint zinauma, ana kweli Jana ilikuwa siku mbaya kwangu.


Senti furomu mai tekino wereva yuzingi jamii foramu mobaili apu
 
😀😀 Kumbuka hilo bumu utalilipia 15% kipato chako kama kweli utabaadika kupata hata kipato.

Litumie boom ka akili kubwa usije fedheheka mbeleni.

Japo kuonja siku moja moja siyo mbaya lakini wewe inaoneka ni mlevi sugu. mpka unamtaka huyo mhudumu japo domo zege.

Siku nyingine fahamu mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Sasa kamba bado haijarefushwa ushaanza kula vinavyokuzidi kimo.
 
Koma sana!

Utaamkiaje kwenye pombe?

Wangekumalizia tu maana huna faida katika Tanzania hii ya Vi-wonder.
 
Daaah Mkuu umenichekesha sana Mkuu nadhani haukutumia misemo ya wahenga mkuu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Haaaa Haaa!
Nimekatika Maini Yote
Mkuu Kukurupuka Ni Kubaya
Sio Kwako Tu Inatokea Kwa
Watu Wote Sema Njia Tofauti
Nakumbuka Kuna Mdau Alihonga
Bar Kwa Matanuzi Ya Da Gama
Akisubiri Hela Iingie Mbona Aliishia
Kuosha Vyombo Vya Bar Na Makwenzi Ya Haja,,
 
[emoji23] [emoji23] ukome....nyie wanafunzi wenye bumu kazi starehe tu
Mkuu sio starehe na hii hutokea mara mbili kwa mwaka.

Senti furomu mai tekino wereva yuzingi jamii foramu mobaili apu
 
Mkuu natumia kwa hesabu sema hii huwa naifanya pale nimalizapo mitihani ya chuo.

Senti furomu mai tekino wereva yuzingi jamii foramu mobaili apu
 
We nawe kilaza... Bora walivyokutia mangumi
 
Dah...

Mkuu umenikumbusha nilishuka pale Dom siku moja stand kwa jeuri ya fedha kuwa M pesa....nikanywa bia kadhaa

Kilichonipata..hahaha...

Haya maeneo hata kama una uhakika wa kupata hela toka mbinguni. Ni vizuri uwe na balance.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…