Sitaisahau kauli hi ya Benard Membe "Hamjui kama mi ni Waziri? Nitaita askari sasahivi" pale Dodoma

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Kuna binadamu wengine huwa wanadharau na kiburi sana. Mwaka 2013 nikiwa Dodoma CRDB kwenye foleni ,akaja Mh Benard Membe (ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na ghafla bila hata salamu, akasogea mbele kabisa ili achukue hela haraka.

Sisi wa mbele kabisa,hatukuweza kunotice kuwa yeye ni nani maana alikuwa kavaa kofia aina ya 'pama' na pia hakuwa na ulinzi wowote. Na pia kama nilivyosema,hata salamu hamna.Kavukavu tu.

Mzee wa mbele yangu alihoji "We nani tena hufuati utaratibu,hautuoni sisi tuliopanga mstari?". Watu wengine nao wakadakia "Utaratibu gani huo?"

"Hamjui kwamba mm n Waziri?Nitaita askari sasahivi hapa". Alifoka Membe.

Kwakuwa pale benki palikuwa na askari, ubabe ukatumika tu akachukua hela na kuwahi huko alikokuwa anakwenda.

Mawaziri kuweni wavumilivu na tuheshimiane tu maana you never know. Leo hii Membe yuko wapi?

Siyo kila raia ana interest ya kukariri political figures

Alfajiri njema
 
Kumtaka kiongozi wa kitafa kukaa ktk foleni hii siyo sawa
basi asiende kwenye huduma za kijamii zinazohitaji foleni, yaani atengenezewe mazingira yake kupata hizo huduma, ikishindikana aambatane na mtu mwenye busara ambaye anaweza kuwaomba walioko kwenye foleni hadi wakaelewa, tena si sawa yeye kujiombea hata kama ana busara, sembuse kutumia nguvu na ubabe na dharau!!!!!!
 
Back
Top Bottom