Siri za Mtikila hadharani

Siri za Mtikila hadharani

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Baada ya mikakati mingi kuonekana kushindwa kumng'oa Lowassa, wana mkakati hao wameamua kumtumia mchungaji Christofer Mtikila atishie kuwafungulia mashitaka Makada wa CCM wanodaiwa kuanza kampeni mapema na kutumia fedha.

Habari za siri kutoka ndani ya Vikao vilivyopanga umafia huo zinasema kuwa baada ya Mtikila kuongea na waandishi wa habari Kamati ya maadili na usalama ya CCM iandae mapendekezo kuwa Makada wanaodaiwa kuanza kampeni mapema na kutumia fedha waenguliwe kwa hoja kwamba wakipitishwa wanaweza kufuguliwa mashitaka mlengwa mkuu akiwa Lowassa.

Mnyetishaji wa siri hii mwenye jina la RK ambaye ni mtu wa karibu sana wa mgombea mmoja mwenye jina kubwa ametamba kummaliza Lowassa kwa mkakati huo, amesema kuwa hoja hiyo itakuwa ni moja ya hoja muhimu ambazo zitatumiwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa kufanya maamuzi ya kuwakata makada hao akiwemo Edward Lowassa kuingia tano Bora.

Juhudi za Kumkwamisha Lowassa zilianza siku nyingi. Siri hiyo ambayo ilianza kuzurula kwenye hisia za watu wengi tangu February Mwaka 2014 hivi karibuni ukweli wake umewekwa bayana na mmoja wa wagombea ambaye ni mwasiasa mkongwe kutoka kanda ya Ziwa.

Mgombea huyo akiongea na wazee amesema yeye si mgombea halisi bali yupo kwa ajili ya kazi maalumu ambayo ni kumkwamisha Edward Lowassa. Akieleza zaidi anasema hata kifungo walichofungwa makada sita CCM Edward Lowassa, Frederick Sumaye, Bernard Membe, Steven Wasira January Makamba na William Ngeleja, yeye na wenzake walikuwa wasindikizaji lakini mlengwa alikuwa ni Lowassa katika kujenga mazingira ya kuja kumkwamisha.

Akitoa siri hiyo Mgombea huyo wa kanda ya ziwa bwana Wasira alisema Mpango huo ulisukwa mahususi na kuwaingiza wengi ili kuhalalisha mpango wa siri utekelezeke bila watu kubaini. Lengo la Mpango huo ni kukata Majina yote ya Makada hao Sita ili kupunguza mazingira ya Lowassa kuona anaonewa lakini pia kupunguza Hasira za wana CCM kuona Kada wanayempenda zaidi amekatwa.

Siri hiyo aliitoa hivi Karibuni alipoitwa na wazee hao ili kumuomba ajitoe kuruhusu Kada mwingine mwenye ushawishi mkubwa awe na nafasi nzuri zaidi kupitishwa ili kanda hiyo ipate rais kwa mara nyingine.

Hata wadadisi na wachunguzi wa mambo pamoja na tafiti rasmi na zisizo rasmi zinaonesha hali ya kumhitaji Lowassa ambayo asilimia kubwa ya wana CCM na wananchi walio wengi wanayo.

Uamuzi wa kumkata Lowassa kwa sababu ya namna yoyote ile kwa sasa utakiletea Chama Cha Mapinduzi hatari ya kuondolewa madarakani au kutumia nguvu kubwa kupata kiti cha rais lakini wabunge wengi watakuwa ni upinzani. Labda wawaachie wanachama kuamua nani wanamtaka na nai hawamtaki.
 
chezeni na lowassaa weeee mkimtoa kura inaenda Ukawaaa,nataka kuchagua rais,sitaki kupewa rais ni mchaguwe...tusipo mpata tunaemtaka ndani ya ccm tuta mtafuta nje ya ccm...dr slaa kaa mkao wa kula...
 
Sijui hayo uliyosema yana ukweli kwa kiwango gani, lakini ungekuwa muungwana kama ungejibu hoja za Mtikila kumhusu EL na wenzake!
 
hivi huyu mamvi ana nguvu kiasi hiki magambani!!!!!
 
chezeni na lowassaa weeee mkimtoa kura inaenda Ukawaaa,nataka kuchagua rais,sitaki kupewa rais ni mchaguwe...tusipo mpata tunaemtaka ndani ya ccm tuta mtafuta nje ya ccm...dr slaa kaa mkao wa kula...

Mbona ukawa hutumtaki na wewe pia hatukutaki.
 
Kwani ni uongo? Yeye kwelu kafanya hayo mambo so lazima avune alichpanda. Afu hata kama bila hayo ya mtikila lazima tu aenguliwe. Fisadi tu huyo
 
Back
Top Bottom