Siri ya polisi kujiua Dar yafichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya polisi kujiua Dar yafichuka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bramo, Jul 9, 2010.

 1. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  SIKU chache baada ya kutokea matukio mawili ya askari polisi, WP Susana na aliyekuwa mkufunzi wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, Konstebo Noel Jenga (33), kujiua kwa kujipiga risasi, imebainika kwamba siku chache zilizopita marehemu Noel alitajwa kuhusika katika tukio la uhalifu.

  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya jeshi hilo, zinaeleza kwamba wakati wa uhai wake marehemu alikuwa akifanya vitendo vya uhalifu kwa kushirikiana na raia.

  Habari zaidi zinapasha kwamba siku chache zilizopita kulitokea tukio la uhalifu jijini Dar es Salaam na watuhumiwa kukamatwa na baada ya kubanwa walimtaja marehemu kushiriki katika tukio hilo.

  “...Marehemu alikuwa miongoni mwa watu wanaolisumbua Jeshi la Polisi kutokana na kushiriki katika matukio ya uhalifu mara kadhaa na siku chache zilizopita alitajwa kuhusika kwenye tukio moja.

  “…Baada ya kutajwa, alishikiliwa na wakuu wake kwa mahojiano zaidi na wakati uchunguzi ukiendelea ndipo tulisikia mwenzetu kaamua kujiua,” kilisema chanzo kingine cha habari.

  Inadaiwa hata alipokuwa mkoani Iringa, alikuwa akijihusisha na matukio hayo, ndipo ilipoamuliwa ahamishiwe katika Chuo cha Mafunzo cha (CCP) mkoani Kilimanjaro ,” alisema mmoja wa maofisa wa jeshi hilo, ambaye hakuwa tayari kuandikwa gazetini.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu juzi, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Robert Manumba, kuhusu tukio hilo, alisema mtu pekee wa kulizungumzia ni mkuu wa chuo alichokuwa akifundisha marehemu huyo.

  “...Zungumza na mkuu wa chuo, yeye ndiye anayeweza kujua tabia za askari wake,” alisema DCI Manumba kwa kifupi kisha kukata simu.

  Naye Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam,(Tanzania Police Academy), SACP, Alice Mapunda, alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia tukio hilo, alisema hana taarifa kama hizo.

  Alisema kabla ya tukio hilo, chuoni hapo hapakuwahi kuwa na taarifa zozote kuhusu suala hilo.

  Alipoulizwa iwapo anafahamu tabia za askari wake, alikiri kuzifahamu na kusema kwa kuwa upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea kufanyika na jamii inapaswa kuvuta subira.

  Konstebo Noel, alijiua kwa kujipiga risasi moja kichwani, akiwa kwenye chumba cha kutunzia silaha katika chuo hicho cha polisi cha jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

  SACP Mapunda, alisema mara baada ya kupokea zamu ya ulinzi askari huyo, aliwaruhusu wenzake waliokesha kwa ulinzi katika kituo hicho kisha kuandika taarifa ya kusudio lake la kujiua kwenye kitabu maalum cha shughuli za zamu maarufu kama OB.

  Katika taarifa hiyo, iliyoandikwa saa 12.45 asubuhi, inaeleza kuwa Konstebo Noel alijiua mwenyewe kwa hiyari yake bila ya kulazimishwa na mtu yeyote na ameomba asisumbuliwe mtu yeyote kutokana na tukio hilo.

  Katika hatua nyingine, msemaji wa jeshi hilo nchini, Abdallah Msika, amestaafu kazi. Habari kutoka ndani ya jeshi hilo, zinasema Msika alistaafu wadhifa huo, tangu Juni 15 mwaka huu na nafasi yake imekaimiwa na afisa aliyetajwa kwa jina la Adivera Senso.

  Source:Tanzania Daima

  My Take:
  Hivi mtu mhalifu ndo apandishwe ngazi kiasi hiko kutoka polisi wa kawaida hadi kuwa mkufunzi????mnapata picha gani na ma askari wetu!!!wanakuwa trained na wahun!!!
   
Loading...