SoC01 Siri ya mafanikio katika maisha ya Binadamu

Stories of Change - 2021 Competition

Nester Reuben

New Member
Sep 14, 2021
3
6
SIRI YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YA BINADAMU

NA: NESTER REUBEN
'Unazo nguvu za kujidhuru au kutojidhuru mwenyewe kama utachagua kutokuwa na furaha hakuna mtu anayeweza kukufanya ufurahi''

Angalia maisha yako. Je, kuna maeneo katika maisha yako hayakufurahishi?
Maisha yako ni wajibu wako; uchaguzi ulioufanya jana au leo una mahusiano ya moja kwa moja na kesho yako. Kwa hiyo, kipekee kama hupendi ubora wa maisha yako ya leo, hivyo jiandae kufanya mabadiliko na kusonga mbele.

Hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kuwa na ukamilifu wa asilimia mia moja anaposhughulikia mambo ya kifamilia, ndugu, rafiki na jamii. Siku zote kutakuwa na nyakati ambazo tutajisikia kuchanganyikiwa au kuridhika. hata kama hatutakamilika, tunazo nguvu na uwezo wa kufanya mabadiliko yenye uhalisia katika maisha yetu. Tunaweza kufanya ongezeko, wakati mwingine kwa mabadiliko bora katika maisha yetu, kama tutabadili mitazamo yetu hasi na kuwa mitazamo chanya. Mawazo hasi siku zote ni gharama' kwa sababu yanauwezo wa kutuvuta chini kifikira na kimwili. Kuanzia sasa na kuendelea mawazo hasi ni anasa ambayo huwezi kuimiliki.

Uko na nguvu kuliko unavyo fikiri. Kadiri unavyojitambua na kujifunza kutumia urithi wa nguvu zako, hakikisha unazitumia tu kwa kujijenga na kujiimarisha mwenyewe, na zaidi sana wengine.
Furaha yetu na mafanikio hutegemea sana tabia tulizo rithishwa, tabia kuelekea sisi wenyewe na tabia kuwaelekea wengine; tabia zetu kuelekea uwekaji malengo na kufanya kazi kwa bidii; tabia zetu kuelekea kushindwa, kukatishwa tamaa, kuvunjwa moyo, msongo, maumivu na mzunguko mzima wa maisha.

Watu wanaokubali mabadiliko huwa tofauti na watu wanaopinga mabadiliko.
Dunia inabadilika kwa kasi na kwa namna mbalimbali, imefikia kipindi mabadiliko yamekuwa ni kitu kisichoepukika, mtu aweza kubadilika na kuwa mzuri zaidi au mbaya zaidi ya alivyokuwa mwanzo
Tunapozungumzia mabadiliko tunamaanisha kukua, kuongezeka, kuendelea kutoka hali moja kwenda nyingine, kiwango kimoja kwenda kingine, kuacha kufanya kitu kimoja na kuanza kufanya vitu vingi na vya tofauti, kuendelea kufanya kitu kile kile lakini kwa ubora zaidi. Inaweza kumaanisha pia kuondoa kitu kimoja mahali fulani na kuleta kitu kingine mfano kuacha tabia fulani isiyo na manufaa na kujenga tabia nyingine yenye manufaa. Neno lenye nguvu zaidi ni mageuzi, mtu unageuzwa na kuwa mtu mwingine kiroho na kitabia, kifamilia, kiuchumi na katika mambo mengine yote yahusuyo maisha kwa ujumla.

Neno la Mungu limezungumzia sana kuhusu mabadiliko na lengo hasa la Mungu ni kubadilisha maisha ya watu. Nami kama mshirika au mdau mkuu wa ufalme wa Mungu sina budi kushiriki kikamilifu katika mpango wa Mungu wa kubadilisha maisha yangu na ya watu wengine pia kwa njia ya neno la Mungu.

Biblia inaeleza habari za Yesu Kristo tangu kuzaliwa na kukua kwake kama sehemu ya mabadiliko ya kawaida. Na hata wakati anaanza huduma alipitia vipindi mbalimbali vya mabadiliko mfano katika kitabu cha Luka 2:40, 52; Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Ukitaka vitu ambavyo hujawahi kuwa navyo, lazima ufanye mambo ambayo hujawahi kuyafanya. Ni wale tu wenye hekima kupita kiasi huthubutu hayo. Ni ombi langu uwe miongoni mwao. Pia kuna wajinga kupita kiasi hubaki vile vile wakipinga mabadiliko ya kila namna yanayowajia, naomba usiwe miongoni mwao.

Kuvua tabia zisizofaa na kuvaa tabia zinazofaa
Yesu mwenyewe baada ya kubatizwa na hatimaye kupandishwa nyikani akiongozwa na Roho Mtakatifu, ili atahiniwe, kwanza aliwekwa kwenye mtihani ambao aliushinda kwa majibu sahihi. Kama tunavyosoma katika kitabu cha

Mathayo 4:1-10; 4:4; Naye akajibu akasema. Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.(mtihani katika NAFSI yenye uhai ibebayo uzima na neno ndiyo chakula)

Hatuna budi kuwa tayari kupokea mabadiliko, kufanywa upya mitazamo, fikra na mawazo yetu vinginevyo tutakufa kiroho na Kimwili baada ya muda mfupi hatutafaa tena katika jamii inayotuzunguka ambayo kila inapoitwa leo inabadilika.

Ni muhimu pia kufahamu na kuamini kwamba tuna uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha yetu na ya wengine. Hata kama tutashindwa kubadilisha hali zinazotuzunguka na watu wanaotuzunguka lakini bado sisi wenyewe tunaweza kubadilika.

Mabadiliko yanaweza kuchukua sura nyingi kutegemea na malengo yanayotaka kutekelezwa na mtu binafsi au kikundi fulani. Kwa mfano kuna wakati ambapo mtu una maono, ndoto au mipango fulani na ili uitimize unahitaji kuwa na utayari wa kubadilika kwa kiwango fulani ili itimie au kuongeza ujuzi fulani unohitajika kutimiza malengo hayo. Yote haya ni mabadiliko na ili yatokee utayari wa kufanya hivyo unahitajika sana. Lakini watu wengi huwa hawapendi kupokea mabadiliko na watu hawa kwa kadri muda unavyopita inafika mahali mitazamo yao, fikra na mawazo yao yanakuwa hayafai tena kuleta manufaa katika jamii husika au maisha yao binafsi.

Ni muhimu kufahamu kwamba siyo kila mabadiliko ni kitu chema na cha kupokelewa, msisitizo wetu uko kwenye mabadiliko mema yaletayo maendeleo. Kumbuka hatuna sababu yoyote ya kutufanya tupokee mabadiliko mabaya yanayoturudisha nyuma, yanayoharibu misingi yetu ya kiutu kwa sababu tu ya kuwapa watu uhuru wa kufanya mambo wanayotaka bila kuingiliwa au kuulizwa na mtu. Siyo mabadiliko hayo tunayoyazungumzia, kwani mabadiliko ya namna hiyo hayapaswi kukubaliwa wala kupokelewa na watu ambao wanamjua Mungu na mapenzi yake.

Warumi 8:28-31; Nasi twajua kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazipamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, walioitwa kwa kusudi lake.

Mungu siku zote huwa anatafuta watu ambao wako tayari kufanya kazi pamoja naye ili kuleta mabadiliko katika jamii fulani na ili mabadiliko hayo yatokee wale wale watakaotumika kuleta mabadiliko lazima kwanza wao wawe wamebadilika na mabadiliko hayo yaonekane katika maisha yao yaani tabia zao, usemi wao, mwenedo wao. Yaonekane wazi kwa watu kiasi cha 1kuleta mvuto wa mabadiliko hayo, wanaowaona na kuwasikia watamani kubadilika na kuwa kama wao na hata kuwazidi kwa kutafuta mabadiliko zaidi.

Kwanini watu hawabadiliki
Hawako tayari kuacha mambo waliyoyazoea na namna walivyozoea kufanya mambo, ambayo wameridhika nayo na wanajiona wako salama kuendelea kufanya au kuendelea kuwa vile walivyo. Wanaogopa maisha yatakuwaje watakapoamua kubadilika, wana hofu ya mabadiliko, wana hofu ya kesho.

Kwa maneno mengine dhambi nikigezo kikubwa cha kutufanya tusibadlike kwa wepesi. Jiulize mwenyewe maswali haya: Ni nini nikifanya mwenyewe kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi kwa mwaka ambacho ni chanya? Chukua muda na ulifikirie swali hili. Ni nini ungependa kipite au kikupishe kile kitu kikuzuiacho? Ni nini ungependa kubadilika katika maisha yako na ufanye nini kufanya kibadilke? Haya ni baadhi ya maswali yakujiuliza na kujitahimini.

Mara tu utakapotaka kubadilika kwenye mambo hasi kwenda chanya, utashangaa sana jinsi mazingira (ulimwengu) yanavyofanyika msaada kwako. Wakati mwingine hali inaweza kuwa mbaya kabla ikawa nzuri, na hii ni sawa kwa sababu ndiyo mwanzo wa mabadiliko, mfano kama hivi karibuni umepoteza kazi, ni wazi kwamba utakuwa umekatishwa tamaa. Lakini usivunjike moyo, badala yake angalia namna nyingine. Hili linaweza kuwa gumu kufanyika; lakini usikatishwe nalo jipe matumaini ya kufanikiwa kwa kuanza upya.

Kupoteza kazi hakumaanishi kwamba ndiyo umeshindwa maisha. Kazi mpya huleta mabadiliko mapya na msisimko mpya katika maisha yako. Kwa vyovyote vile utaishia kupata fursa nzuri kutokana na mabadiliko hayo.

Jiulize mwenyewe hivi: Ni kweli nahitaji kubadilika au nataka tu kuendelea kulalamika na kile nisicho nacho katika maisha; nataka kuboresha maisha yangu kwa kiwango cha juu kuliko nilivyo sasa?
Kama unataka kufanya kazi itakayohusika na mabadiliko, hivyo huna budi kubadilika kiubora zaidi. Hakuna mtu atakaye fanya kwa ajili yako. Ni wewe tu mwenye nguvu kwa hiyo unahitaji kuendelea kujikumbusha mwenyewe juu ya hilo.

Usiwe mkusanya takataka
Nani anaamua kama maisha yako yatakuwa ya furaha au yenye huzuni? Jibu ni wewe!
Tunadhibiti furaha zetu. Lakini ili kuwa na furaha yatupasa kuyafanya yale yanayo sababisha tuwe na furaha.

Hebu fikiria juu ya hili! Ni mara ngapi umepuuzia majumuisho yaliyogharamiwa juu yako na bado umeingiza maneno yasiyofaa kwa wiki? Wengi wetu tunakumbuka matimizo kwa muda na tunakumbuka maudhi kwa miaka mingi. Tunakuwa wakusanya taka-tukitembea nazo taka za miaka mingi iliyopita. Kama unaruhusu mambo mabaya katika ufahamu wako ni wazi utapata madhara makubwa maishani.
Kumbuka unaudhibiti ufahamu wako mwenyewe. Kwa hiyo lazima ujitengenezee furaha ya kweli mwenyewe iwe ni tabia ya kudumu. Furaha siku zote vipo ndani ya uwezo wako. Mwanadamu ameumbwa kwa kufurahi. Unachotakiwa kufanya daima hakikisha mwisho wako unaishia kwenye furaha. Halafu jenga maisha yako katika sehemu hii ya furaha, kufurahia na upendo.

Wafilipi 4:4-7; Furahini katika BWANA siku zote, tena nasema furahini. Upole wenu...
Warumi 15:13; Basi na Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini.......
 
Back
Top Bottom