Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    565
Wewe uliyefuatilia hebu nipe mwanga wa hili, jamaa amesema dunia ni tambarare na maji yamezuiliwa kwa mabone makubwa ya barafu. Swali, mwishi wa hayo mabonge ya barafu ni wapi na baada ya hayo mabonge kuna nini!
nimeishia njiani mkuu niliona nachanganyikiwa theory zao nyingi zina mashiko sana. nitaludi kusoma tena haya mambo nikitulia
 
Unajaribu kuongea uongo kwa kufanya comparison na vitu ambavyo vingine haviwakilishi uhalisia,mf.kusema kuhusu bendera ya U.N... kilichofanyika hapo ni kuwa ni kama wame-strech tu kwamba mabara yote yaonekane kwenye bendera. Hivi wangeonesha bara la Ulaya na Asia tu si ungekuja hapa useme huu umoja wa mataifa ni kudanganyana,mbona kuna mabara ya Weupe tu.

Nimesoma 60% ya andiko lako refu naona hakuna sababu yoyote ya Kisayansi ulioitoa.
 
Ndio maana leo hii ni watu wengi sana hawaamini kama Mungu yupo, kwamba hakuna pia mwisho wa dunia.

WATU wanaosoma biblia huchanganya na nadharia za kisayansi kuhusu umbo la dunia. UKISOMA sana biblia, imeandikwa kuwa dunia ni flat, pia imetulia, ukitegemea sayansi za wapagani ndio hizo ambazo zinajitahidi kushawishi watu kuwa hakuna uumbaji uliofanyika bali uibukaji wa vitu, binadamu hakuumbwa bali alitokana na vimelea, na hakuna Mungu wala mwisho wa dunia.

Hii imeleta ndani ya mind za watu kuwa waovu kadiri iwezekanavyo kwa sababu hakuna kuwa na chochote after death.

Na hao mleta uzi unaosema ni ma elites umeshindwa kuwataja ni Vatican na agents zao kama Jesuits, illuminatti, freemason na wengineo wengi. HAWA ndio wameshika miradi yote ya science za kilimo kama mambo ya GMO, spaceprogram zote zipo chini yao Including NASA na karibu everthing iwe ni siasa au uchumi nk.

Na mambo haya wanahakikisha hakuna anayejua na kusambaza. HATA HUU UZI HAUTAFIKA MBALI LAZIMA UFUTWE .
 
Kuna vitu ukiangalia ulivyoandika kuna ukweli fulani hivi ila bado nakuwa na mashaka na baadhi ya theory zako je vipi kuhusu usiku na mchana kama kweli dunia ni flat na vipi kuhusu utofauti wa muda hivi kuhusu jua kua ndio linazunguka dunia kwa hiyo jua ni dogo na dunia kubwa na vipi kuhusu kupatwa inakuaj hapo??
 
sinajinasasa,
Tatizo lenu mnaotetea hii hoja mnaishi kwenye dunia ya kufikirika na pia kukaa kwenye wasiwasi ambao hata nyie wenyewe hamjui kiini chake. Unapozungumzia Jesuits, illuminatti, freemason nk. na kusema wao ndio wameshika mambo yote ya science za kilimo, Je, una udhibitisho wa hilo?

Ulimwengu wa zamani za mwanzo wa hizi dini zetu, walikuwa na maarifa yao ya wakati huo ambayo pia yaliwasaidia sana kwa kipindi chao. Tatizo lenu mnataka tuishi katika ulimwengu wa sasa kwa taaluma/maarifa ya ulimwengu wa zamani zile. Hilo ni gumu kutekelezeka!

Mfano, enzi hizo(biblia) waliamini Ukoma ni ugonjwa uliompata mtu kutokana na laana au adhabu toka kwa Mungu. Ili watu wengine wasiupate, mgonjwa sharti atengwe ili wengine waepuke adhabu(kuugua). Hilo liliwasaidia sana kwa wakati ule. Je tuendelee kufuata na kuamini UGUNDUZI huo wa kale kwenye dunia hii ya sasa?

Tuelewe wazi kwamba ulimwengu tunaoishi kwa sasa ni wa FACTS. Hii ni kutokana na nyenzo,utaalam pamoja na maarifa yaliyopo na ambayo yako bayana na yanayotoa nafasi ya kujua mambo kwa uhakika bila shaka yoyote. Kwamba dunia ni tambarare au duara inabidi unayetetea hoja ujitosheleze.

Tuliofundishwa kwamba ni duara tukaamini hivyo tuna vigezo vya kuamini.
 
Cc Kiranga
 
Ngorunde,
Ushahidi au evidence ninayo! wewe nina uhakika huna uhakika na unachong'ang'ana nacho...umefundishwa na kukaririshwa kama mtoto asiyejitambua.

Ushahidi kuwa dunia ni flat upo dhahiri na wazi

1. Maji naturally ni flat haiwezekani bahari na maziwa yakae kwenye round ball. Wewe kwa ujinga utasema yanakaa kwa nguvu za uvutano wa dunia, sio kweli.

2. Maji pia hufuata mkondo, yaani yanatoka kwenye miiniko kwenda bondeni mfano maji ya Victoria kuelekea Mediteranian, dunia isingekuwa flat yasingefika huko.

3. Ungekuwa rubani wa ndege ungetambua kuwa unapokuwa hewani akiisha kaa kwenye degree zone fulani hakuna muda unabadilisha angle kufuatia bending.

Unataka kuendelea kuamini ujinga wa kukaririshwa kuwa dunia ni sphere kwa sababu tu ya upatikanaji wa usiku na mchana?

Mungu mwenyewe namna alivyoitengeneza mifumo ya jua na mwezi hakuna binadamu anayejua. Hao NASA na CERN wanatumabia kutoka Big bang theory kuwa the Universe is Expanding, na hizo nyota tunazoziona juu ni makundi ya nyota yaani galaxies, na umbali wake ni milions of light years, hii yote ni uongo kama ilivyo uongo kwenye kipimo cha carbon14, Hizi zote theory knowledge ni global agenda na imefanikiwa sana. Wapagani sasa ndo wameshika hatamu.

Na siwasingizii Vatican kuwa wapo behind yote haya, nadhani kwa kuwa huielewi historia ya hizi dini na historia ya ulimwengu na empire zake. Na kwa sababu huelewi hayo hujui sasa hivi tupo wapi katika historia na hivyo basi hujui tunapopelekwa na hii historia. Wakati wewe kazi yako ni kula, kunywa na kulala wapo wanaume duniani wanaishi wakifikiria wakufanyie nini ili uwe mtumwa wao. Tafakari, naamini muda sio mrefu moderators wataambiwa wauondoe uzi huu.
 
Uzuri ni kwamba, si NASA peke yake iliyofanikiwa kwenda nje ya dunia. Mataifa ya Uchina, Urusi, India nk hakuna aliyesema dunia ni tambarale.

Ukweli utabaki pale pale, ukianza safari kutoka point A kuelekea mashariki au magharibi kwa kipindi fulani utajikuta umerudi pale pale ulipoanzia safari. mfano mtu akianza safari ya kuelekea China kutoka Africa, akifika China anaweza kuvuka bahari ya Pacific hadi USA. kisha kutoka USA akavuka bahari ya Atlantic kurudi Afrika...

sidhani kama dunia ni tambarale hili linawezekana?

Kwa wanaofatilia makala za kisayansi wamepata kuona hata wanafunzi wakiwa field katika bara la Antarctica.
binafsi iko duara.
 
Duh! Hahahhaha, huyu jamaa kama sikosei ni msabato. Tena umbumbumbu wake unajipambanua kwa jinsi asivoweza kuandika kiswahili kwa ufasaha. Ni heri ya mjinga atafutaye elimu kuliko mbumbumbu ajifanyaye anajua, ni janga! Haiingii akilini katika karne hii ya sayansi na teknolojia, mpaka live feed kutoka ISS zipo kwa watu wanaotaka kushuhudia na kujifunza! Ni aibu sana.

Ndugu moudytunechi naomba nikuulize maswali moja tu kabla hatujaendelea kujadiliana!
  • Unaweza ukatuonesha ramani ya dunia bapa, na magema ya ukingo wa dunia?
 
moudytunechi,
Hii elimu siasa nyingine. Napenda kutambua uwepo wa Chama duniani Flat earth society wanaoeneza elimu hii.
Kabla sijazama ndani zaidi na kufuatilia hii mada naomba mwandishi nikukumbushe yafuatayo.

1: Galileo hajawahi kuwa mgiriki Bali ni muitaliano.
2: Kusema Dunia ni flat sio elimu mpya Bali imekuwepo miaka mingi na Dunia inamshukuru Galileo kwa kutambua Hilo na kuwaangusha Wagiriki walioamini uzushi wa Aristotle na hizo dini uliyotaja zilizokuwa zinafundisha Dunia ni tambarare iliyobebwa na tembo kobe Mara nyoka.

3: Moja ya utetezi wa watu hawa yaani flat earth society ni uwepo wa Ile bendera ya UN. Hivi kama mimi ni naanzisha taasisi ya kidunia na Nataka mabara yote yaonekane in 2D nitafanyaje Bila kuweka kama inavyoonekana UN.

Nitapita baadae ila research ndani zaidi ili utendee haki wasomaji wako. Hilo Labda ukiamini kama dini ila sio science maana Kuna laws lukuki za physics inabidi zivunjwe ili hili wazo uliolileta like halisi.

Badaebdae kdg
 

Sijawahi kuona uzushi mkuu kama huu. Na aibu kubwa runners wa haya mawazo ya kizamani mwenyekiti wa taasisi ni Evolutionist kwa sababu anajua fika bibilia inakubaliana na wkin Galileo na NASA. Nilitegemea kwenye pics zake anionyeshe spaces photo au satellite photo to support his arguments. Analeta picha zilizopigwa ambazo sio reliable maana zinarepresent tiny particle ya Dunia.

Pili aeleze ni kwa vipi Russia ipakane na ulaya wakati huohuo inapakana na us kwa umbali uliochini ya km4 huko Alaska. Na kama Russia wasingewauzia marekani eneo lote la Alaska hoja hii ingeeleweka mapema zaidi.

Kazi kweli kweli
 
Thibitisha nadharia yako. Unapoambiwa dunia ni tambarare unaweza kutoka sehemu 1 ukazunguka dunia bado ukarudi pale pale ukajichorea duara lako.
labda nijaribu kutoa mfano: ukitoka Afrika ukafika Amerika (mfano Alaska); ukapata safari ya kwenda China, je! ni lazima urudi Afrika? Je! huwezi kuvuka bahari ya pacific kwenda china? kama utafika china kwa njia hiyo, kufika Afrika utarudi kwa utaratibu wa kawaida kupitia nchi za arabuni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…