Sioni gazeti la kununua kwa sasa

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Nimefuatilia uandishi wa yale magazeti huru mawili yaliyokuwa yamepewa angalizo naona nao wameingia kwenye mkumbo wa kusifu na kuabudu!

Nina hela za kununulia gazeti lakini uandishi wake unaukakasi haulezei uhalisia wa maisha tunayoyaishi, vitisho vimefanikiwa kwa mara nyingine.

Siwalaumu wamiliki,kweli mwenye nguvu mpishe lakini hela yangu ya kununulia gazeti mtaikosa.

Jiandaeni kupunguza wafanyakazi na pia kuchelewa kuwalipa kilichobakia ni kusikiliza sauti ya Mungu na kuitii.
 
Asante kwa kuliona hilo, kuna hatari inanyemelea uchumi wa wamiliki, binafsi hata taarifa ya habari itv siangalii tena na kile kipindi cha magazeti RFA sifuatilii tena, nimebakiza kuangalia BBC dira tv, kusikiliza BBC radio (dira ya dunia na amka na BBC) na kusoma gazeti la Mwanaspoti tu, full stop
 
Asante kwa kuliona hilo, kuna hatari inanyemelea uchumi wa wamiliki, binafsi hata taarifa ya habari itv siangalii tena na kile kipindi cha magazeti RFA sifuatilii tena, nimebakiza kuangalia BBC dira tv, kusikiliza BBC radio (dira ya dunia na amka na BBC) na kusoma gazeti la Mwanaspoti tu, full stop
ITV wametangaza kuchelewesha mishahara ya mwezi huu! wakati Nipashe lilikuwa linafanya vizuri sokoni kabla ya kupiga goti kwa Faru John
 
kuna gazet leo, habar kuu imensikitsha sana. N moja ya yale mawil
hata mimi nimeona mtandaoni nimesikitika sana.nafuu ufanyekazi kwa weledi ufungiwe kuliko kujitoa ufahamu na kusaliti wananchi kwa kuwalisha sumu! moja linaongelea upinzani kukatariwa toka ripoti ya Nyalali huku akishindwa kueleza ukweli namna upinzani unavyofinyangwa na watawala.hata Zanzibar ambapo upinzani ulishanda haliongelei.waandishi wa habari wetu wapuuzi.sana! hata wakipata fursa ya kuongea na hao wagandamizaji wanawachekea.sasa hivi ilibidi wasijipendekeze watetee taaluma zao.
 
Lengo ni kununua gazeti au kupata taarifa? Kama magazeti hayana taarifa unazotaka walinunua la nini. Mimi sinunui magazeti lakini kwa ulimwengu wa sasa taarifa zooote muhimu napata.
 
Back
Top Bottom