Sio kweli kwamba CHADEMA haijitangazi vijijini

Sio kweli kwamba CHADEMA haijitangazi vijijini

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
3,108
Reaction score
2,553
Kumekuwa na uvumi kwamba CHADEMA imekuwa haijitangazi vijijini na badala yake imejikita maeneo ya mijini tu jambo ambalo si la kweli.Dhana hii ingeweza kukubalika kwa CHADEMA ya miaka mitano iliyopita lakini si CHADEMA ya sasa hasa baada ya kumalizika uchaguzi wa ndani wa chama hivi karibuni.

Miaka ya nyuma CHADEMA haikuwa na viongzi wa ngazi za chini kuanzia misingi,matawi,kata na hata baadhi ya majimbo,wilaya na mikoa uongozi ulikuwa dhaifu sana.Wakati ule chama kilionekana kipo vijijini pale wanapofanya ziara viongozi wa kitaifa hususani mwenyekiti Mbowe,katibu mkuu Slaa na viongozi wengine maarufu kama Lissu,Mnnyika,Mdee,Heche n.k na kwa kiasi fulani MSALITI Zitto (huyu alikuwa anafanya ziara kwa maslahi yake na si ya chama).

Hivi sasa chama hakitegemei ziara za viongozi wa kitaifa kujitangaza na badala yake kila kiongozi anafanya kazi kubwa ya kukieneza na kikitumikia chama katika ngazi yake aliyochaguliwa.

Mfano mimi mwenyewe ni mwenyekiti wa chama wa kata fulani huku Moshi na mjumbe wa kamati ya utendaji ya jimbo lakini mimi na viongozi wenzangu wa kata,matawi na misingi hatutegemei kiongozi yeyote wa kitaifa aje akitangaze chama kwenye kata yetu bali tunawajibika wenyewe tena kwa bidii kubwa.

Hivyo vijana wa Lumumba msikariri kwamba CHADEMA ni Mbowe na Slaa tu kama mnavyofikiri CCM ni Kinana na Nape tu mpaka kupelekea viongozi wengine kukalia benchi hapo Lumumba huku Kinana na Nape wakipuyanga mikoani kila kukicha, au vijana wa Mwandiga mnavyodhani ACT ni Zitto kiasi hata mnashindwa kufanya uchaguzi mpaka Zitto ajiunge rasmi.

CHADEMA ni taasisi yenye viongozi kila ngazi kwa mujibu wa katiba yake na viongozi wake hasa vijijini wako kwenye harakati kubwa hivi sasa za kusimika wagombea ngazi ya mitaa,vijiji na vitongoji.

Baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa tutaheshimiana tu.
 
Usiwafumbue macho kamanda, hawa walishalala usingizi wa pono!
 
mkuu hakuna haja ya kuwastua waache waendelee kujilia elfu 7 zao , huku kwetu KYELA , VIJIJI VYA LUBELE , MBAKO , KILASILO , IBUNGU , NJISI , BODA , ISAKI , KABANGA NA KATUMBASONGWE NI CHADEMA TUPU !
 
Unaweza kutupa matokeo ya Ubunge Jimbo la Kalenga na Chalinze.
 
Unaweza kutupa matokeo ya Ubunge Jimbo la Kalenga na Chalinze.

Kwa akili zenu fupi mnadhani kalenga na chalinze ndio tz! Vp kuhusu 4:0 za arusha? Au kile kichapo tulichowapa magamba hapa Magu Ktk Uchaguzi Wa SM?
 
Mlichakachua km kawaida yenu.chama cha mafisadi
 
Unaweza kutupa matokeo ya Ubunge Jimbo la Kalenga na Chalinze.
Nyie si mwajulikana can u imagine Mijigamba ati imeijiibia yenyewe hadi kura za kupitisha Katiba kaazi kweli kweli.Kalenga kulikuwa na daftari jipya la wapiga kura ambalo lilifanyiwa na Miccm aibu yenu.
 
Viongozi wa cdm waanze oparesheni nchi nzima kama wanavyofanya kinana na nape! Chama hujengwa kwa mikutano ya hadhara na sio vinginevyo.
 
Unaweza kutupa matokeo ya Ubunge Jimbo la Kalenga na Chalinze.

Kumbe mtoa kwa kusema mnakariri yu sahihi! Kwa karenga alikuwa anagombea mtoto wa mbunge aliyekuwa amekufa bila kwa kifo cha ccm (kwa vipi utajaza). Ccm walihamishia serikali yote huko. Chalinze 1. Inakutwa mkoa wa pwani ambako hadi leo kila watu 95% ni ccm na 95% nimaskini wa kutupa. Kilimanjaro na Arusha 95% ni cdm na maskini wa kutupa ni 5%. 2. Aliye kuwa anagombea ni mtoto wa rais aliyeko madarakani. Baba, malkia na serikali vilihamia huko. Mwisho mtoa mada yu sahihi. Mimi hapa ni mwenyekiti wa kata cdm Muleba. Sasa hivi tunaenda ktk uhakiki na uwekaji sawa wagombea wa kijiji fulani. Kwa ccm sijawaona wakijishughulisha. Tuamini cda mtaijua baada ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom