Sio kosa langu #9

Sio kosa langu #9

samnas

Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
35
Reaction score
1
Miezi mitatu sasa tangu Hashir aanze kazi kwa mzee ochu, mshahara wa hapo ulimfurahisha sana Hashir mpaka alijikuta akifungua genge kwa bibi yake huko magomeni. Maisha kwao yalianza kua mazuri baada ya Mungu kuwamulikia Nuru yake na kutambua shida waliokua nayo. Chakula hakikuwapa tabu tena wawili hao na kujikuta wakiishi maisha ya raha sana, japo waliondokewa na mtu muhimu sana maishani mwao. Tayari hashir alishakata tamaa juu ya wazazi wake na kujikuta akitekwa akili na jasmin mschana alitokea kuvutiwa nae sana na kujenga mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu. Kwa mapenzi aliyokua nayo jasmin kwa hashir aliamua kumnunulia hashir simu ya mkononi ambayo wangeweza kuwasiliana kupitia simu hyo. Hashir hakukataa kupokea zawadi hyo . Tayari wawili hao walikua kwenye mapenzi motomoto huku wakiekeana ahadi ya kuoana. Kiukweli hashir alitokea kumpenda sana jasmin, kwa yote aliyomtendea hakujua nini amsaidie, na hali mbaya ya kimaisha aliyokua nayo hashir bado jasmin alivutiwa na kijana huyo na kuwashawishi wazazi wake kumlipia ada mpaka alipomaliza darasa la saba. Na ugumu alokua nao hashir hakusita kumsaidia jasmin alipopata tatizo, yote aliyokua na uwezo nao hakusita kumfanyia, na aliposhindwa alikua muwazi. Tabia yake ya kumjali ilimvutia sana jasmin na kushindwa kujua ampe nini kama shukran kwake.
Hashir kijana aliepevuka na aliyekata mvua 19, alikamilika kiasi ya kwamba angeweza kum bebesha ujauzito mtoto wa watu. Tayari alishazoea taabu na shida za maisha, kukosa chakula kwake ilikua ni kitu cha kawaida.

Ilikua ni siku ya alhamis siku ya wapendanao, hashir akielekea anapofanya kazi kwa mzee ochu.. akiwa njiani mawazo tele kichwani alibahatika kuonana na kipenzi wake, jasmin, sura zao zilionekana zikisheheni mapenzi na furaha ya hali ya juu pindi wanapokutana. Ni kama vile waliumbwa kwa jozi maalum, walipendana sana kiasi kwamba mmoja wao akipatwa na shida basi huiona shida hyo ni ya kwao wote.

'' ooh hashir jamaniiii....maaambo??'' Jasmin akiwa na furahavya hali ya juu kumuona kipenzi wake alimsalimu.
''Poaa....hujambo wewe mtoto mzuri?''
''Mi mzima wa afyaa, hof kwako tu''
''Wala usiwe na hofu maana nko poa mbona, sana tu....umependeza lakinii jamani''
''Ooh jamni asanteeee....''
'' umetoka wapi mda huu naona umependeza mpaka bas''
'' nlikua kwa shangaz yangu hapo mtaa wa nyuma, tunatoka leo kutembea kidgo,si unajua tena''
''Yah kweli kabisa...basi tutawasiliana vizuri mi naelekea kazini kidogo..''
'' ooh sawa kua makini lakini jamni..''
''Usijali njiwa wangu ntakua makini..''
Walicheka wote wawili na kukumbatiana. Hashir alimshika jasmin kiuno na kumbusu kichwani kuonesha ishara ya upendo, hakuamini macho yake jasmin baada ya muda mrefu kutekwa akili na aliyempenda , hashir aliagana na jasmin huku akielekea kazini. Alitamani sana siku hyo ya wapendanao watoke pamoja wakajivinjari, lakini aliogopa sana kumkorofisha bosi wake. Na pia wapi angelipata hiyo pesa ya kuchezea wakati huo? Ni kweli alimpenda sana jasmin na alitamani sana wawe pamoja wakati wote.
Dakika 15 baadae tayari hashir aliwasili nyumbani kwa ochu tayari kwa kufanya kazi. Mandhari ya nyumbani hapo kwa siku hiyo yalimshtusha kidogo,na kujikuta akitabasamu kwa furaha. Nyumba siku hyo ilipambwa vizuri kanakwamba kulikua na harusi nyumbani hapo. Hakujua nini kinaendelea . Baada ya kuingia ndani katika jumba hilo la kifahari alimkuta mke wa ochu bi zuwena akiwa amelewa, jambo lililomshtua sana hashir na kumfanya atake kujua nini kilimsibu mama huyo mpaka akanywa pombe na kulewa. Zuwena bila kusita alimfata hashir huku akiwa anayumba yumba, alimshika mkono na kumvuta kifuani mwake. Jasho jembamba lilimtoka hashir, moyo ulimwenda mbio mithli ya mtu alietaka kutokwa roho. Hakujua afanye nini na aseme nini, hakuwa mtu wa mambo hayo. Bi zuena tayari alishachanganyikiwa na yale majibu ya daktari aliyopewa siku nyingi nyuma. Mumewe hakurudi nyumbani kwa siku sita mfululizo. Zuwena hamu ya kufanya mapenzi ilimpanda na wala hakutaka kufikiria kama ni mke wa mtu,akili yake tayari ilishavurugika. Aliipamba nyumba kwa sababu ya mfanya kazi wake tu ambae ni hashir. Mwili wa zuwena ulioumbika na uliojaa juu na chini haikua rahisi kwa mwanaume rijali kubanwa na mwanamke huyo kwa kutaka kufanya mapenzi kisha akakataa. Hashir alijikuta ni mtu asiyejua la kufanya na kushindwa kukataa kile bosi wake alichomtaka afanye,aliogopa sana kupoteza kazi yake na mshahara mkubwa aliokua akiupata. Hivyo kwa kuliogopa hilo alitenda lile aliloamriwa kulifanya.
Mwili mzima ulimsisimka na kujikuta akitolewa nguo moja moja na kufanya mapenzi na mama huyo. Wote wawili hawakujuana na ilikua ni vigumu kutambuana. Tangu zuwena anamtupa hashir chini ya daraja alikua yu kichanga hajui lolote, hakuijua sura ya mama yake wala hakuweza kufikiria anafananaje.
Hamu ya mapenzi iliwajaa wawili hao huku zuwena ikimjia fikra labda mumewe alikua na matatizo na sio yeye, hivyo alitamani sana kupata ujauzito. Walipeana penzi zito huku wakibebana mpaka chumbani na huko wakijikuta katika penzi zito. Kwa mara ya kwanza hashir alijilaumu na kujutia . Hakuweza kulifikiria hilo mwanzo kwa hamu aliyokua nayo kufanya mapenzi. Alijua labda bosi wake alipitiwa..lakini kwanini aliipamba nyumba kabla? Je alishapanga muda kufanya hiko kitendo.? Maswali hayakukauka kichwani mwa hashir. Hali hyo ya bosi wake kumtaka kimapenzi na kumpa tunda ilifululiza kwa muda wa wiki nzima na kujikuta ni mtumishi wa mapenzi na sio tena kazi za ndani. Hashir jambo hilo lilimuumiza sana moyo na kujikuta akivunja ahadi waliyoahidiana na mpenzi wake jasmin. Na pia aliogopa sana kupoteza kazi yake iliyomfanya apate chochote kitu na kuweza kuishi. Wapi angelipata kazi nyengine wakati hakua na cheti chochote cha shule? Siri hiyo aliificha hashir na kuahidi kutomwambia mtu yeyote.
..
.
. ******************

.
.
... Nini kingetokea baada ya wawili hao kutambuana kua ni mama na mwana? Je zuwena angeliweza kumuangalia mtoto wake aliyemfanya kijakazi wa mapenzi kwa kipindi kirefu? .. usikose kuifatilia riwaya hii ya kusisimua sehemu ya # 10
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom