Sio kosa langu #8

Sio kosa langu #8

samnas

Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
35
Reaction score
1
,''Kweli dokta umepima vizuri??'' aliuliza karima kwa mshangao,
''Ndio dada vipimo vyetu hua havisemi uongo kabisa!!'' Alimhakikishia nesi. Ilikua ni vigumu kwa karima kuamini kwa kile alichokisikia baada ya kupata vipimo vya mimba na kukutwa ana mimba ya wiki kadhaa. Alitumbua macho mithli ya mjusi aliyebanwa na mlango, tayari alikua na maswali yaliokosa majibu,, atamwambia nini Muro akirudi kutoka japan??, na muda si mrefu atarudi kutoka alipokua. Tayari idriss alirudi kazini kwake, huko keko ndipo ilipokua ofisi yake huku akimiliki gari tatu za mafuta ya pertoli pamoja na gari moja la dizel(diesel), maisha yake yalimnyookea, hakuamini alipopokea barua na kuambiwa kwamba karima ana mimba ya mwezi mmoja kasoro siku chache tu.
Zilikua ni habari zilizomfurahisha na kumhuzunisha sana Idrissa, kwa upande mmoja alifurahi kupata mtoto na mwanamke aliempenda zaidi maishani mwake, pia alifurahi kupata mrithi wake na msaidizi wake, lakini kilichomtia wasiwasi na kukosa raha ni pale muro atakapotambua kua mimba haikua yake. Tayari alishayaweka maisha yake matatani.
''Mh!! Kwa hyo nitafanya nini jamani?'' Aliuliza sana maswali hayo Idrissa bila ya kupata jibu na kushindwa kuelewa afanye nini, ilim bidi amuombe ushauri na msaada chuga, naye alimhakikishia kumsaidia kivovote vile madhali wao ni marafiki walotoka mbali sana, husaidiana na kupendana katika hali zote.
Wiki moja baadae mzee muro aliwasili nchini akisindikizwa na msafara mkubwa wa wananchi pamoja na maaskari, ilikua ni kipindi cha uchaguzi mkuu, hivyo madhali ilikua ni dhamira yake kugombania nafasi ya uraisi mwaka huo basi tayari alishaomba usajili na kuandaa kampeni akisaidiwa na wasaidizi wake kadhaa kupanga mikakati yake ili iende sawa. Wengi walimhakikishia kumteua mzee huyo kwa siasa yake safi. Karima hakua na furaha ya aina yoyote, kichanga alichokua nacho kilimtesa tumboni na kumpa maswali yaliokosa majibu, hakujua aiweke sura yake wapi baada ya mzee huyo kuutambua ukweli, aliamini kwa hasira alizokua nazo mzee huyo angeweza hata kumchoma kisu na kumuulia mbali, hakutaka karima yote yatokee hayo, alijilaumu sana kwa kitendo alichokifanya cha kuichafua ndoa yake na mzee muro, maisha aliyaona machungu na hakujua nini afanye.
Miezi mitatu baadae mimba ya karima tayari ilidhihirika, muro alipatwa na wasi wasi sana japo hakumuelezea mkewekipi kinamtia waswasi , karima aliliitambua hilo mda tu na akamtumia idrissa ujumbe kumuelezea wasi wasi alokua nao mzee muro dhidi ya ujauzito alokua nao karima. Hilo lilimkosesha raha karima pamoja na muro mwenyewe japo hawakudhihirisha hilo walipokua wanakutana wakiongea au wakila.
Muda mrefu mzee muro alijishughulisha kufanya kampeni na kusafiri mikoani kwaajili ya kampeni zake ili aweze kupata kura nyingi zaidi. Baada ya mwezi mmoja matokeo yalikua wazi na mzee huyo aliibuka kua makamo wa raisi nchini Tanzania. Ilikua ni siku ya furaha kwa familia hiyo, walijumuika na kufurahika pamoja kwa mudaa mrefu.
Miezi nane baadae tayari mimba ya karima ilishapevuka,hakuchoka kutia mguu kwenye klinik za kina mama kila siku.
''Mme wangu tumbo linaniuma sana na nahisi kizunguzungu kweli yan....''
Karima alimwambia muro,, mzee huyo alielewa nini kinamsumbua..na haraka sana alimuamuru dereva wake wampeleke muhimbili haraka sana.
''vipi dokta??,,anaendeleaje mke wangu??..'' aliuliza makamo wa rais baada ya kukaa muda mrefu akisubiri majibu ya mkewe.
''Hongera sana mheshimiwa rais, mkeo Kafanikiwa kajifungua mtoto wa kiume salama..'' makamo wa rais mheshimiwa muro hakusita kufurahi, alikaribishwa kwenye chumba cha leba,,, hakuamini alichokiona mbele yake na kubaki akimshangaa mkewe, hali iliyowabakisha madaktari na wauguzi katika kitendawili kisichoteguka.
..
***************
..

...
Kipi kilimshtusha makamo wa raisi, na je angelitambua kua mtoto si wake nini angefanya?? Uskose kufatilia mkasa huu wa kusisimua sehemu ya #9
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom