Sintofahamu ya Mtandao kuzimwa Uganda: Kauli za Waziri zazua Mjadala mkubwa

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Katika hali iliyoshangaza wengi, Waziri wa Vijana nchini Uganda ametoa ufafanuzi wa kutatanisha kuhusu sababu za kukatika kwa huduma ya mtandao wakati huu wa mchakato wa uchaguzi mkuu nchini humo.

Soma pia: Uganda yatangaza kuzima Intaneti kuanzia leo Januari 13 ili kupisha Uchaguzi Mkuu


Your browser is not able to display this video.


Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha taifa (UBC), Waziri huyo alibainisha kuwa awali Kamisheni ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) ilitangaza kuzima mtandao kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiusalama, lakini akashangaza wengi kwa kuongeza madai mapya kuwa hitilafu hiyo inatokana na sababu za kiufundi. Waziri alidai kuwa amepata taarifa kuwa meli iliyokuwa ikipita katika pwani ya Mombasa nchini Kenya ilikata kebo kuu ya mtandao vipande viwili, na hivyo kusababisha nchi nzima kukaa gizani kidijitali.

Licha ya mwandishi wa habari kuhoji kuhusu uhalali wa taarifa hizo na uhusiano wake na mchakato wa uchaguzi, Waziri alisisitiza kuwa mafundi wako kazini usiku na mchana kujaribu kuunganisha kebo hiyo, akitabiri kuwa huduma hiyo inaweza kurejea ndani ya wiki moja au mbili.

Katika kile kilichoonekana kama dongo kwa vijana, Waziri aliwataka raia kuwa na subira na kumwamini Rais, akidai kuwa kiongozi huyo ndiye aliyeleta teknolojia hiyo nchini na ndiye atakayeirejesha. Alimalizia kwa kuwakosoa vijana kwa kutumia muda mwingi kwenye mtandao wa TikTok badala ya kusikiliza jumbe za kiongozi wa nchi, huku akiwakumbusha kuwa enzi za nyuma nchi ilikuwa ikijiendesha bila mtandao, hivyo hali ya sasa isichukuliwe kama jambo la ajabu.
 
Waziri alidai kuwa amepata taarifa kuwa meli iliyokuwa ikipita katika pwani ya Mombasa nchini Kenya ilikata kebo kuu ya mtandao vipande viwili, na hivyo kusababisha nchi nzima kukaa gizani kidijitali.
Hahaha aah kumamakezake !
 
kwa sababu za kiusalama,
kuzima mtandao ni hatua muhimu zaidi japo huwakera mno mamluki wa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi. Sababu nyingine za ziada zianaweza kua na maana pia katika kuzima mtandao ili kudhibiti usalama wa nchi.

Hongera rais Yoweri Kaguta Museven kwa kuaminiwa tena na watu wa Uganda kuongoza taifa hilo
 
Nchi nyingi za kiafrica zina viongozi wajinga sana!, sababu za kuzima mtandao hazina kichwa wala miguu.
Sio wajinga, wanajua hatuna uthubutu.

Ndio maana huwa wanazungumza maneno ya kutia hasira lakini wananchi hakuna hatua wanachukua.

Kitendo cha mwanasiasa kuzungumza mambo/maneno ambayo msikilizaji unaweza kuona hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kusema, sio kwamba huwa ni bahati mbaya.

Huwa wanafanya hivyo ili kutukomaza katika uvumilivu wa ujinga (psychological)

Hata siku akifanya kitu gani cha kijinga au cha ajabu, kwa kuwa tulishazoea tutaishia kuongea tu na jambo litaishia hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…